Naiona hatari huko mbele uteuzi wa wanajeshi walio kazini kushika nyadhifa za kisiasa


Wanajeshi ni wabobezi katika mambo ya ulinzi na usalama, wamesimama katika nafasi nzuri zaidi kuongeza mkoa na wilaya kwa kuwa hawa ndiyo wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama. Mkoa iliyopo mpakani inapendeza zaidi kuongeza na wanajeshi kama wakuu wa mkoa na wilaya.Acha wivu wa kibeberu
 
Ni sawa tu kama ilivyo kuzisoma namba ambavyo hakuchagui kada na asiye kada!!!
Gharama za kukiuka katiba zitalipwa kwa Watanganyika wote hakuna atakayepunjwa.
 
Shetani ni nani?
Umetahadharisha jambo zuri. Ni kwa faida yetu sote watanzania na nchi yetu wakiwemo CCM. Wabongo na upeo mdogo wa kuchambua mambo hawawezi kuona consequenses zake. Waache wakukebehi. Siku yakitufika matokeo yake ndiyo tutajilaumu. Hii halinishangazi sana kwani waafrika matatizo yetu mengi ni sisi wenyewe tunayatengeza.
 
Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama hivo haina shida ni sawa unamtoa samaki ziwani na kumtupa baharini
 
Kuna kitu nahisi baadhi ya wachangiaji ikiwemo G'taxi nahisi hamjakielewaa bado. Anachojaribu kuwasilisha mtoa mada ni kuwa NI HATARI SANA KWA MWANA USALAMA KUZOEA MADARAKA KAMA YA KISIASA MAANA KUNA SIKU TUSIYOIJUA ATATAMANI NA YEYE AKALIE NAFASI ILE ALIYOKALIA YULE ALIYEMTEUA KWA MAANA HAKUNA ASIYEPENDA KUABUDIWA. sasa ukifika wakati huo ndipo tutayashuhudia yale ambayo hatukuwahi kuyawaza. Mhe.Rais anaweza akahisi anakua salama zaidi akiwa na hao wanausalama kumbe labda anajiweka kwenye hatari zaidi kwa maana anawapa nafasi ya kumjua na kujua zaidi kuhusu yale wasiyoyajua.
Hivyo nadhani mtoa mada anaweza akawa mzalendo zaidi kwa hiki alichokiandika kuliko sisi wachangiaji tunaojisifia kuwa ni wazalendo na kusifia kila kitu ambacho mh. JPM anafanya. We all are appreciating to what our Beloved H.E Dr. JPM is serving for the country. But he needs to be more secured .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…