Friends and our Enemies
Katika muendelezo wa kumshukuru Allah muumba wa mbingu,ardhi na vyote vilivyomo naendelea kuipongeza serikali inayoongozwa na Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kudumisha amani,umoja,mshikamano na utulivu huku wananchi wazalendo tukiendelea kulipa kodi na kujenga nchi,Ahsante sana Dr Samia.
Hivi karibuni kanisa katoliki limeingia kwenye mgogoro na vita ya kurushiana maneno pamoja na waumini wake huku kanisa hilo likikomaa katika kusimamaia msimamo wa kuwakashifu na kuwatukana waumini hao na kuacha kujibu hoja za msingi za waumini wao.
Badala yake kanisa kupitia vijana wake wamehamisha mjadala na kulia huku wakisaga meno na kusema eti kwamba hao siyo waumini wa katoliki halisia,mara wakisema ni waumini njaa na wavaa vijora.
Katika yote hayo wanayosema kanisa wamepuuza kabisa kama siyo kukwepa kujibu hoja za waumini hao na badala yake hivi sasa wanatuma lawama kwamba vikundi hivyo vinapangwa na CCM na Serikali yake.
Kitu wanachoshindwa kudadavua kanisa ni kwamba ndani ya CCM na Serikali kuna wafuasi wao pia kwahiyo kusema hivyo ni kuzidi kujichimbia shimo wao wenyewe na kujitukana zaidi.
Kwa hayo yanayoendelea napenda sana kuipongeza serikali kwa kupuuza kuingia kwenye fitina ya kuwajibu wala kubishana nao na badala yake wameamua kuwapuuza na kuendelea na shughuli zake za kujenga taifa na kudumisha amani na utulivu nchini.
Ukimya huo ni jibu tosha kwa wote wanaojaribu kutengeneza fitina na kusaga sumu ili kutaka kuligawa taifa na kutengeneza mgawanyiko usio na msingi ndani ya taifa letu.
Nami binafsi kama Kiranja wa jamii nachukua nafasi hii kuwapongeza viongozi wa Kanisa Katoliki kwa kuwa imara na kutoonyesha ukondoo kwa hizi senema zinazochezwa na serikali ya Samia na chama chake cha CCM
Viongozi wamekuwa imara na shupavu kujibu kila shambulizi linalolenga kanisa. Hakika kiongozi shupavu ni yule anayelinda na kutetea maslahi ya taasisi anayoiongoza. Hili liko wazi kwa viongozi na Mababa wote wa kanisa takatifu katoliki la mitume
Na shukurani za pekee ziwaendee waumini wote wa kanisa takatifu katoliki la mitume kwa kuwa watulivu, waangalifu na kuishi katika maadili ya imani yao. Hakika utulivu wao ni wa kuigwa na watu wengine
Kwa namna walivyojibu mashambulizi kwa utulivu na umakini, leo tumeanza kuona series mpya ya maigizo ya kuvamiwa na kupigwa yaliyoigizwa na wapaka mikorogo ambao ngozi zao zimekwishajiozea kwa kemikali. Hakika mwaka huu tutayaona mengi
Kanisa takatifu katoliki la mitume, ni kanisa lenye waumini wanaojitambua, wanaotambua msingi wa imani yao kwani wamelelewa kuikiri na kuisadiki imani yao toka wakiwa wadogo. Waumini wa kanisa katoliki wengi si wahamiaji, wamezaliwa humo, wamelelewa humo, wamekulia humo! Hii huwafanya kuwa waaminifu kwa imani yao, kutambua mipaka ya imani yao na wanazifahamu tamaduni na taratibu za kanisa lao ndiomaana huwa hawajibu kwa pupa
Na mwisho kabisa lakini si kwa umuhimu, nikopengeze wewe binafsi kwa kuendelea kusherehesha huu mjadala na kumfaraji aliye nyuma ya haya maigizo.
Wengi tunafahamu, hii unayofanya ni sehemu ya kazi yako nawe unajipatia ujira wako ili angalau tank za choo zihudumie wadudu wanaoishi humo
Hata hivyo, kwa vile kazi mnayofanya ni ngumu na ni ya aibu na kufedhehesha utu wenu, nawashauri msifanye kazi kwa kuahidiwa ujira. Hakikisheni mnalipwa kwanza kabisa ili baadae msije kurudi kulialia mbele ya jamii baada ya kudhurumiana au kupunjwa sehemu ya ujira waliowaahidi maana hao watu hawatabiriki.
Hongera sana kwa kukubali kufanya kazi inayokushushia heshima, inayotweza utu wako, inayokuvua nguo mbele ya watu wanaojitambua na kukuacha uchi mwilini na akilini. Hakika kazi hii haina tofauti na kazi inayofanya na vichaa wale wanaohangaika kusafisha jalala kwa kula mabaki yaliyotupwa. Wale hawana makosa kwasababu ufahamu na akili zao zilipata changamoto inayojulikana kitababu na hata kijamii
Mshangao mkubwa unabaki kwenu nyie mliokubali kufanya kazi zinazowastahili watu waliorukwa na akili ama kwa kuugua ama kwa mihadarati na wengine wamezaliwa hivyo (wakiwa na mtindio wa ubongo).