Mkuu
Pythagoras , japo naunga mkono hoja ya TCRA kutumia professionalism kwenye vyombo vya utangazaji, na siungi mkono ubwabwajaji wenye ill motives behind, lakini mimi ni mtetezi wa haki!. Alichofanyiwa Polepole na TCRA kufungiwa hadi aajiri professional journalist, sio haki, na kulazimisha kila utoaji elimu kufuata misingi ya uandishi wa habari sio haki!.
Duniani kuna professionals mamilioni, bilioni au hata trilioni!, mfano mzuri ni angalia idadi ya waalimu, unapeleka mtoto shule ili kumfuata mwalimu na anafundishia darasani ili kuweka wanafunzi wengi pamoja. Huku kwetu kutokana na umasikini wetu ni lazima umpeleke mtoto shule. Kwa nchi za wenzetu, unaweza kuajiri Mwalimu akaja kwako kukufundishia mwanao. Hata baadhi ya vyuo vikuu, vikiwepo Oxford na Cambridge, sio lazima kila anayejiunga adahiliwe, wengine ni vilaza mpaka basi, akihudhuria lecture anatoka kapa, anafundishwa na ma profesa kwa spoon fed kupitia tutorials hadi anahitimu.
Ujio wa social media umefungua milango kwa mtu yoyote mwenye uwezo wowote, kufungua online class kufundisha chochote, kwa watu wowote bila kuvunja sheria, hivyo online classes kuzilazimisha kufuata misingi ya utoaji habari as news contents, sio haki!, huku sio kuwatendea haki Watanzania!.
Sio kila utoaji elimu mtandaoni ni utoaji habari!. Naunga mkono TCRA, blogs za uhabarishaji ziendeshwe na professional journalists lakini watu wenye professionals nyingine zote nao wawe huru kuendesha madarasa yao ya utoaji elimu mtandaoni kwa uhuru bila kila kitu mtandaoni kugeuzwa ni habari. Madaktari watoe elimu ya tiba, waalimu wawafundishe wanafunzi wao, waganga wa alternative medicine watoe elimu zao, wanasiasa nao waendeshe madarasa yao ya siasa kwa uhuru.
Kitu cha pili cha ajabu sana kuhusu hii TCRA yetu ni hii double standards yake. Yule kichaa aliyekuwa kukashifu na kutukana watu kupitia mtandao wake, mbona hakudhibitiwa?. Mbona hakutakiwa ku balance tuhuma zake na anao watuhumu?, why only Polepole?.
Hongera kwa TCRA kusisitiza professionalism lakini TCRA iwatendee haki Watanzania, kilichofanywa kwa Polepole ni uonevu na sii haki. Sio kila utoaji elimu mtandaoni ni utoaji habari!.
P.