Naipongeza TCRA kwa kumkomesha Polepole and the Likes: Massage sent!

Naipongeza TCRA kwa kumkomesha Polepole and the Likes: Massage sent!

Ukumbuke akiwa mwenezi ndo alikuwa na uwezo wa ku-influence teuzi mbalimbali na kwa katiba yao ni sawa na kusema alikuwa jikoni.Sasa jiko lina wenyewe kwasasa,ndo kelele hizo !
Ulidhani Polepole angedumu kwenye Itikadi na Uenezi hata baada ya kuteuliwa kuwa Mbunge?

Hata Magufuli asingelifariki Polepole angepumzishwa. Ni utaratibu tu wa CCM

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Polepole ajifunze kuheshimu awamu ya sita na nyingine nyingi tu zijazo elimu yake ya ujasiriamali awafundishe wanawe sisi watanzania tumemchoka pia ni mtu kigeugeu
Wakati wa jiwe mlikuwa mnamuona polepole kama Mungu wenu hapo lumumba.
 
Wakizoea kula nyama ya binadamu hawataacha! Leo wamemfumba mdomo Polepole kesho watafumba kila mtu tuwe tayari kupokea matokeo.

Tusimame imara kutetea uhuru wa kujieleza hata kama anayejieleza ni Shetani tumpime kwa hoja zake badala ya rangi yake.

Kama Polepole amefungiwa kwa kukiuka sheria well and good ila tusifurahie kwa kuwa ni Polepole "kakomeshwa" tutakuwa hatuna tofauti na madhalimu.
Wacha wagonjwa wanyweshane uji wenye sumu.

Wametunyanyasa kipindi kirefu sana kwa kujivunia malaika wao.

Sasa wacha na wao waonje madhara ya kunyanyaswa ili akili iwarudie.
 
To be fair sijaona wala kusikia maneno ya kashfa toka kwa bw slow slow. Tuseme tu freedom of speech bado haipo sana wala kivile nchini. Viongozi ni lazima uwasifie. Uwapambe. Uwaogope. Uwaabudu!
Ukikosoa kidogo basi wewe gaidi mchochezi mvuruga amani mamluki msaliti.
Inauma kuendelea kuishi maisha kama hayo huku viongozi wanachaguliwa na raia wakiamini watawakilishwa.
 
Mkuu Pythagoras , japo naunga mkono hoja ya TCRA kutumia professionalism kwenye vyombo vya utangazaji, na siungi mkono ubwabwajaji wenye ill motives behind, lakini mimi ni mtetezi wa haki!. Alichofanyiwa Polepole na TCRA kufungiwa hadi aajiri professional journalist, sio haki, na kulazimisha kila utoaji elimu kufuata misingi ya uandishi wa habari sio haki!.

Duniani kuna professionals mamilioni, bilioni au hata trilioni!, mfano mzuri ni angalia idadi ya waalimu, unapeleka mtoto shule ili kumfuata mwalimu na anafundishia darasani ili kuweka wanafunzi wengi pamoja. Huku kwetu kutokana na umasikini wetu ni lazima umpeleke mtoto shule. Kwa nchi za wenzetu, unaweza kuajiri Mwalimu akaja kwako kukufundishia mwanao. Hata baadhi ya vyuo vikuu, vikiwepo Oxford na Cambridge, sio lazima kila anayejiunga adahiliwe, wengine ni vilaza mpaka basi, akihudhuria lecture anatoka kapa, anafundishwa na ma profesa kwa spoon fed kupitia tutorials hadi anahitimu.

Ujio wa social media umefungua milango kwa mtu yoyote mwenye uwezo wowote, kufungua online class kufundisha chochote, kwa watu wowote bila kuvunja sheria, hivyo online classes kuzilazimisha kufuata misingi ya utoaji habari as news contents, sio haki!, huku sio kuwatendea haki Watanzania!.

Sio kila utoaji elimu mtandaoni ni utoaji habari!. Naunga mkono TCRA, blogs za uhabarishaji ziendeshwe na professional journalists lakini watu wenye professionals nyingine zote nao wawe huru kuendesha madarasa yao ya utoaji elimu mtandaoni kwa uhuru bila kila kitu mtandaoni kugeuzwa ni habari. Madaktari watoe elimu ya tiba, waalimu wawafundishe wanafunzi wao, waganga wa alternative medicine watoe elimu zao, wanasiasa nao waendeshe madarasa yao ya siasa kwa uhuru.

Kitu cha pili cha ajabu sana kuhusu hii TCRA yetu ni hii double standards yake. Yule kichaa aliyekuwa kukashifu na kutukana watu kupitia mtandao wake, mbona hakudhibitiwa?. Mbona hakutakiwa ku balance tuhuma zake na anao watuhumu?, why only Polepole?.

Hongera kwa TCRA kusisitiza professionalism lakini TCRA iwatendee haki Watanzania, kilichofanywa kwa Polepole ni uonevu na sii haki. Sio kila utoaji elimu mtandaoni ni utoaji habari!.
P.
Ila nikukumbushe tu, wakati Sheria habari , mswaada wake wa hati ya dharura na miswaada mingine ya mabadiliko ya Sheria yanawasilishwa Kwa hati za dharura, awamu iliyopota, wapo watanzania waliona hatari iliyokuwa mbele Yao, wakapiga kelele mno, wapo walioelewa, wapo waliokebehi, wapo waliounga mkono mabadiliko ya Sheria Kwa hati ya dharura, kwakuwa TU zililenga kuwanyamazisha wakosoaji wa awamu Ile, Sasa zimeaanza kuwatafuna wote, hata waliocheka na kufueahia wanalia🤔.
 
Unapokomenti jambo punguza munkali,umechanganya mambo sana kama una chuki na mtu binafsi mrekebishe kwa upole,umekuja na povu la bluu na macho yamekutoka vipi bhana.ehe haya Anza upya.
 
Ktk vitu ambavyo intelijensia haijachukulia mzaha ni pamoja na swala la Polepole. Hata kama mlichelewa kumfumba mdomo lakini atleast mmejaribu.

Huyu Polepole tungemchekea mwisho wa siku tungevuna mabua

Waswahili husema ukimchekea sana Mbwa itakuja siku atakufata msikitini. Haiwezekani mtu yuleyule aliyeaminiwa na mamlaka akapewa nafasi za uongozi ktk ngazi kubwa za utawala akaanza kubwabwaja hovyo huku akikejeli mamlaka iliyoko madarakani kwa kujidai ati anaishauri

Ni jambo gani alishindwa kushauri serikali wakati akiwa ni kiongozi wa juu ambalo ataweza sasa??

Ktk siasa za duniani kuna kitu kinaitwa Disloyalty, Ni kitu hatari sana. Kikiachwa kikamea kinaweza kuiangusha nchi na taifa kwa ujumla.

Hebu tujiulize maswal kidogo, Kama Polepole alikuwa anaushawishi kati ya watanzania wengi kiasi hiki kwa kutoa maoni na taarifa za uongo tunajuaje kama vile vyombo vingine pia havimwamini na kumfata??

Je vile vyombo vikigawanyika na upande wenye nguvu ukamuunga mkono( vikawa Loyal) mnajua nini kinaweza kutokea..

Political loyalty aliyotaka kuzalisha ilikuwa kwanza kugain Support kutoka kwa Wananchi( civic loyalty) huku chini ya kapeti aki creat( ku-renew) Political Loyalty kutoka kwenye vyombo vyenye nguvu.

TCRA ni wakupongezwa. Tukumbuke kikinuka hakuna atayebaki salama.

Hongera TCRA kwa kazi nzuri. Ujumbe umefika.

Umewakata viromo romo.
Aajiri waandishi na wahariri ili watu wapate kazi

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Pythagoras , japo naunga mkono hoja ya TCRA kutumia professionalism kwenye vyombo vya utangazaji, na siungi mkono ubwabwajaji wenye ill motives behind, lakini mimi ni mtetezi wa haki!. Alichofanyiwa Polepole na TCRA kufungiwa hadi aajiri professional journalist, sio haki, na kulazimisha kila utoaji elimu kufuata misingi ya uandishi wa habari sio haki!.

Duniani kuna professionals mamilioni, bilioni au hata trilioni!, mfano mzuri ni angalia idadi ya waalimu, unapeleka mtoto shule ili kumfuata mwalimu na anafundishia darasani ili kuweka wanafunzi wengi pamoja. Huku kwetu kutokana na umasikini wetu ni lazima umpeleke mtoto shule. Kwa nchi za wenzetu, unaweza kuajiri Mwalimu akaja kwako kukufundishia mwanao. Hata baadhi ya vyuo vikuu, vikiwepo Oxford na Cambridge, sio lazima kila anayejiunga adahiliwe, wengine ni vilaza mpaka basi, akihudhuria lecture anatoka kapa, anafundishwa na ma profesa kwa spoon fed kupitia tutorials hadi anahitimu.

Ujio wa social media umefungua milango kwa mtu yoyote mwenye uwezo wowote, kufungua online class kufundisha chochote, kwa watu wowote bila kuvunja sheria, hivyo online classes kuzilazimisha kufuata misingi ya utoaji habari as news contents, sio haki!, huku sio kuwatendea haki Watanzania!.

Sio kila utoaji elimu mtandaoni ni utoaji habari!. Naunga mkono TCRA, blogs za uhabarishaji ziendeshwe na professional journalists lakini watu wenye professionals nyingine zote nao wawe huru kuendesha madarasa yao ya utoaji elimu mtandaoni kwa uhuru bila kila kitu mtandaoni kugeuzwa ni habari. Madaktari watoe elimu ya tiba, waalimu wawafundishe wanafunzi wao, waganga wa alternative medicine watoe elimu zao, wanasiasa nao waendeshe madarasa yao ya siasa kwa uhuru.

Kitu cha pili cha ajabu sana kuhusu hii TCRA yetu ni hii double standards yake. Yule kichaa aliyekuwa kukashifu na kutukana watu kupitia mtandao wake, mbona hakudhibitiwa?. Mbona hakutakiwa ku balance tuhuma zake na anao watuhumu?, why only Polepole?.

Hongera kwa TCRA kusisitiza professionalism lakini TCRA iwatendee haki Watanzania, kilichofanywa kwa Polepole ni uonevu na sii haki. Sio kila utoaji elimu mtandaoni ni utoaji habari!.
P.
Amevuna alichokipanda,wala TCRA wasingehangaika nae na mashundisho yake,lakini pale unapotumia mashundisho kuikebehi serikali matokeo yake ndio hayo.Huyo mwingine TCRA HAIKUSHUGHULIKA NAE kwasababu alikukuwa analindwa na Jiwe kama yalivyolindwa magenge mengine ya wahuni kama Sabaya.
 
Waswahili husema ukimchekea sana Mbwa itakuja siku atakufata msikitini. Haiwezekani mtu yuleyule aliyeaminiwa na mamlaka akapewa nafasi za uongozi ktk ngazi kubwa za utawala akaanza kubwabwaja hovyo huku akikejeli mamlaka iliyoko madarakani kwa kujidai ati anaishauri
Yaani ombeni Shetani sana asitokee mtu kama Dkt Magufuli, mtajuta nyie kundi la mafisadi. Yaani mtajuta. Maana sasa mnaonekana mmeshinda mnajipongeza.
 
Watu wanafundishwa mpaka staili za kufanya mapenz huko online ila sujawah sikia TCRA ikiwaita
Kiukweli kabisa Polepole ameonewa mwanzo mwisho!.
Zile kanuni za maudhui mitandaoni zinahusu online TV za habari. Ndizo zinapaswa kufuata journalism professionalism. Polepole sio journalist, ana kitu cha Kufundisha, kwanini azuiliwe?. Kuna madarasa mangapi online yanayofundisha mambo mbalimbali?.
P
 
Hii ni aibu sana,wapiga kura wanashindwa kuelewa chadema wanataka nini,wao badala ya kuchukia kitu polepole anachoongea wao wanamchukia muongeaji ,chadema kutoka shimoni sio leo mtasugua sana matako.
 
Waswahili husema ukimchekea sana Mbwa itakuja siku atakufata msikitini. Haiwezekani mtu yuleyule aliyeaminiwa na mamlaka akapewa nafasi za uongozi ktk ngazi kubwa za utawala akaanza kubwabwaja hovyo huku akikejeli mamlaka iliyoko madarakani kwa kujidai ati anaishauri
Mzee wa quotations kazini ha ha ha..
 
Aajiri waandishi na wahariri ili watu wapate kazi

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Kwani kazi anayofanya ni u-anahabari?? zile porojo tu. Sema TCRA walikuwa hawana namna ya kumnyamazisha wakatia kwenye nyavu ya kanuni za maudhui ambayo inajikita kwenye professionalism kama akivyofanfanua nguli Pascal Maalla
 
Umeandika mengi kishabiki Lakini Polepole si tatizo pekee. Polepole ni tone tu katika maji machafu. Ameshiriki kutunga sheria na kanuni kamdamizi ambazo Leo zimemrudi mwenyewe na ambavyo huyo unayesema anakosa loyality kwake ameshiriki katika maovu hayo hayo. Mfumo CCM ndio tatizo la yote haya nchini, watu wengi wameumia kwa sababu ya Uhuni wa CCM ambao nyie mnaita utii kwa mamlaka kumbe mnaumiza watu.
Alishiriki wapi kuziandika hizo sheria kamanda? alukuwa anaziandika kama nani? maana ubunge kapewa juzi na Samia.
 
Yaani ombeni Shetani sana asitokee mtu kama Dkt Magufuli, mtajuta nyie kundi la mafisadi. Yaani mtajuta. Maana sasa mnaonekana mmeshinda mnajipongeza.
Hehehee Huyo atakayekuja atakuwa zaidi ya Magufuli??
 
Back
Top Bottom