Kenya 2022 Nairobi: Ruto ashinda Kura kituo walichopiga Kura familia ya Uhuru Kenyatta

Kenya 2022 Nairobi: Ruto ashinda Kura kituo walichopiga Kura familia ya Uhuru Kenyatta

Kenya 2022 General Election

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Licha ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kuwataka Wakenya wasimpe kura mgombea urais wa Kenya Kwanza na Naibu Rais, William Ruto bali wampe kura hizo mgombea urais wa Azimio la Umoja, Raila Odinga ameshindwa kumbeba mgombea huyo katika kituo alichopigia kura.

======

Matokeo ya kura za urais ya uchaguzi mkuu, uliofanyika jana nchini humo, yanaonyesha katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya msingi Mutomo katika jimbo la Gatundu Kusini ambako Rais Kenyatta na familia yake (mama yake Ngina Kenyatta na mkewe Margareth Kenyatta) walipigia kura yanaonyesha Ruto amepata kura mara mbili zaidi ya alizopata Odinga huku kura tatu zikiharibika.

Matokeo hayo pia yameonyesha kuwa mgombea wa urais wa chama cha Agano, Waihiga Mwaure amepata kura nne huku mgombea urais wa chama cha Roots, George Wajackoya amepata kura tisa.

Katika kura zilizopigwa na kuhesabiwa kituoni hapo zinaonyesha kuwa Ruto amepata kura 983 huku Odinga amepata kura 464

Waliojiandikisha kupiga kura katika kituo hicho walikuwa ni wapigakura 2,164 lakini waliojitokeza ni 1,460.
 
Kudos kwa Kenyans, damu iliyomwagika haikumwagika bure, mmeonyesha ukomavu na ingieni kwenye kundi la wanademocracia wa kweli, Tanzania ni unyumbu, ukunguru, uzuzu, ujinga, upumbavu waendelee kusubiri miujiza
 
Kudos kwa Kenyans, damu iliyomwagika haikumwagika bure, mmeonyesha ukomavu na ingieni kwenye kundi la wanademocracia wa kweli, Tanzania ni unyumbu, ukunguru,uzuzu, ujinga,upumbavu waendelee kusubiri miujiza
Hahahaha! 2025 Lowassa anarudi Tena mzee kugombea SS itakuaj....ila TZ nyie
 
Hahahaha! 2025 lowassa anarudi Tena mzee kugombea SS itakuaj....ila TZ nyie
Looo mkuu kwani wewe ni mganga wa kienyeji kututabiria hivyo kuhusu Mr. Lowassa? But welldone kwa Kenyans kwa kutuonyesha uchaguzi huru na haki, kila mtu anapata matokeo live!,sio kura zibebwe kutoka Namtumbo hadi Dar kuhesabiwa
 
Odinga kwisha! astaafu siasa wakenya bado wanamisimamo mikali ya ukabila.
 
Kituo alichopigia Kura Martha Karua pia aliyeongoza ni Ruto, kwa kifupi Mt. Kenya wame vote against Uhuru kenyatta,
 
Most likeky Ruto atashinda. Strong hold za Raila zikoje?
Sijaangalia kwa Nyanza, ila kwa Western ambapo Raila alikua na Strong hold pia Maji yanaelekea kuzidi unga.

Ukiangalia kwa Kura Milioni 6.5 zilizohesabiwa na Kituo cha Nation TV, Ruto anaongoza kwa 51.67%

yuko mbali a bit! very sad for raila anyway! I wanted him to win
 
Back
Top Bottom