lets think straight for a second here......
middle east wana import sana kahawa na majani chai.... kukaa kujipiga kifua kwamba bila sisi (exporter) middle east hawajanywa chai ni ujinga. zaidi zaidi ni kutumia nafasi hiyo hata kutengeneza matangazo yanayo sisitiza flani manufaa ya chai thereby utaongeza watumiaji na in the long run maximum profits.
nikirudi kwenye post yako, wewe na watanzania wengi tunachofanya ni kujipiga kifua kwamba bila sisi wakenya hawali which is rather stupid in my view.
Nchi ya kenya ni kame kwa asilimia zaidi ya sabini, wananchi wanazidi kuongezeka na mahitaji ya chakula pia yanaongezeka, hili ni soko zuri sana kwetu sisi tuliejaliwa asilimia kubwa ya nchi ina rotuba na mvua za kutosha kustawisha mazao yote, sasa je ipi bora, kufanya kilimo cha kisasa, kuiongezea thamani kwa kupakia vizuri na kuexport as finished/processed foodstuff, au kukaaa miaka yote kujipiga kifua kwamba bila Tanzania wakenya wanakufa njaa wakati hao wakulima bado ni masikini kama walivyokua miaka 20 iliopita???
Kwenye nyekundu umesema, "ng'ombe yanavyo ingia Kenya,". Leo hii, kama mtumiaji wa sausage, naamini ushakutana na sausage za farmers choice au Halal corned beef (kitu safi sana!) kwenye supermarket, hata kama wewe hutumii ila wapo watanzania wanaotumia na faida inaenda kenya, huku wewe unajipiga kifua kupeleka ng'ombe kenya.
Mashudu unayoongelea wanatengenezea lisho la hao ng'ombe na mwisho wa siku unakutana na maziwa ya brookside, UHT, na KCC kwenye shelf za supermarket kwa bei sawa au tofauti ya sh100 na azam/tanga fresh za hapa hapa.
Kiukweli inafaa tuamke, our standards are so low, tunaridhishwa na vitu vidogo vidogo sana. tukisharidhika ni wendo wa kupiga vifua na kupost picha za kibera na kuponda chochote kizuri! jamani!!!!!...