Naishauri serikali Kesho isije Ikatumia mabavu, iache CHADEMA wafanye maandamano yao kwa Amani

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Nimeona nami kwa nafasi yangu hata kama ni ndogo, niishauri serikali kuhusu haya maandamano ya hawa ndugu zetu wa CHADEMA.

Hakuna haja ya kutumia mabavu na ubabe kuzuia CHADEMA kuonyesha hisia za Maumivu ya ndugu zao waliouawa na kutekwa. Ni wanachama wenzao.

Haitakuwa HAKI.
Nilikuwa najaribu kujishawishi kuwa Wanachadema wasifanye maandamano na niwe upande wa serikali lakini nimeona Sina hoja ya kupinga maandamano hayo.

Ikiwa lengo kweli ni kuomboleza, kukemea na kuitaka serikali ichukue hatua kwa HAKI za wanachama wao na Watanzania wengine waliotekwa na kuuawa na kutojulikana walipo, sioni tatizo la maandamano.

Mimi napinga Kauli ya "Samia Must Goo" kwani hiyo ni nje ya utaratibu wa sheria zetu. Hiyo wasubiri Mwakani 2025.

Wanahaki kwa sababu:

1. Waliotekwa na kuuawa ni wanachama wenzao. Kutochukua hatua zozote itaashiria kuwa chama chao hakiwezi kupigania Haki za Wanachama wenzao.

Hata hivyo ilitakiwa maandamano haya yafanywe na wananchi wote wa Tanzania.
Lakini kwa vile sisi sio kitu kimoja hiyo haitawezekana.

2. Wanahaki kwa Sababu wenye wajibu ambao ni serikali imeshindwa kufanya sehemu yake kutafuta wanaofanya hayo matukio u mauaji na UTEKAJI.

Hii inawafanya wao wenyewe kutetea haki za wanachama wenzao. Hii itamaanisha kuwa kuwa mwananchi wa chama cha Demokrasia Hauna Haki na hata ukiuawa hautakuwa n tofauti na sungura au panya Buku. Tena Bora sungura huko TANAPA wanalinda wanyamapori.

NINI KINAJENGEKa IKIWA SERIKALI HAITACHUKUA HATUA STAHIKI NA IKITUMIA MABAVU;

1. Chuki na Visasi vitajengeka.
Chuki baina ya wanachama wa CHADEMA na serikali(CCM) itazidi kukua.

Mtu anaweza kusamehe Makosa mengi lakini kosa la kumuua mzazi wake au Mtoto wake ni kosa ambalo kikawaida halitakiwi kusamehewa. Ni kosa la kulipa Kisasi. Na ni HAKI Kisasi kilipwe ikiwa Haki ya kawaida haikutendeka.

Inaweza kuwa, kwa vile wanaotendewa hayo wakadharauliwa kwa sababu ni Wachache na hawana nguvu lakini mambo ya Haki hayaendagi hivyo. Tusifanye watu waichukie nchi yao na wananchi wao.

Kwa sababu kama wananchi watakaa kimya wakati watu wenzao wanauawa itahesabika kuwa waliungana na WAUAJI kufanya uhalifu huo.

Hiyo ni sababu ya matendo mabaya ya kigaidi yanayoendelea Duniani. Ni hatari sana.

2. Nchi kupasuka na kukosa utulivu.

Matendo haya kikawaida hayawezi kufurahisha viongozi wote waliopo kwenye vyombo vya Dola.
Wapo viongozi ambao huweza kuingia na moyo wa Imani na Kuona kinachoendelea sio chema. Hii hupelekea Dola kupasuka na nchi kukosa utulivu.

Tunaona nchi kama Libya kwa Hayyati Gadafi, Iraq kwa Sadamu Hussein. Yanapotokea matukio ya ukandamizaji wa kundi Fulani ni rahisi kwa adui kuivuruga nchi.

Kwa sisi watibeli tunajua, matokeo ya uovu.

Yuda alipomsaliti Yesu akamuuza kwa vipande vya fedha baadaye aligundua kuwa Ile fedha Haina maana yoyote, matokeo yake akaona airudishe kisha akaenda kujiua sababu ya Hatia.

Hatia ndio huifarakanishaga watawala. Linazuka tuu kundi linaona yanayoendelea sio sawa na jingine linaona sawa alafu Kuna kuwa na uwiano wa kinguvu. Mwishowe nchi inapasuka au kuchafuka.

3. Wasio na vyama ambao ni sisi nasi tutachoka Kuona kundi Fulani likiumizwa.

Watanzania wengi hawana vyama lakini hiyo haimaanishi hawafuatilii siasa. Hatutaki chama au kundi Fulani lionewe. Makundi na vyama vyote vipewe HAKI sawa.
Hatutaki Dini Fulani ionewe au ipendelewe tunataka Dini zote na wasio na Dini wapewe HAKI sawa.

Sisi tusio na upande ambao ndio wengi tunataka mfanye mambo yenu bila kuoneana na kufanyiana dhulma.

Hatutaki nchi yetu ichafuke. Hatutaki nchi yetu ipasuke vipande vipande au kugawanyika kama Sudan kaskazini na Sudani Kusini.

Tunataka nchi Moja. Na nchi Moja ni Ile ambayo Kuna usawa na Haki baina ya watu na makundi yao. Hakuna chama chenye mamlaka au Haki zaidi ya vyama vingine.

Kukosekana umoja na kundi linalotaka kujipendelea na kukandamiza makundi mengine ndilo litahesabika kama linaloivuruga Amani ya nchi hii. Kila kundi linalohaki ya kujilinda na kutetea HAKI zake ikiwa litaona kuwa linaonewana kudhulimiwa.

Serikali, mambo haya hayahitaji nguvu na mabavu. Hatutaki Kuona watu wanapigana na kumwagana Damu na ubongo bila sababu ya msingi.

Akili kazi yake ni kutafuta suluhu kwa njia isiyoumiza. Akili hizo ninaamini viongozi mnazo sema mnataka kufanya Makosa ya kiufundi kwa kutumia nguvu zisizohitajika.

Wewe kiongozi utakayezuia maandamano kabla hujafanya hivyo lazima ujiulize;

Wewe Baba yako au Mtoto wako ndio angekuwa ameuawa au kutekwa na hajulikani alipo usingeandamana?
Yaani assume hao watoto wako ambao wako salama au huyo Babaako unayempenda aliyesalama angetokea mtu akamuua kwa kifo cha kikatili au akatekwa usingeandamana?

Au fikiria wewe ndio umeuawa, au umetekwa uko matekani kwa watesi wako. Alafu ukasikia watoto na watu wanaandamana kwaajili yako ungejisikiaje? Ungewachukuliaje Wananchi wenzako?
Ungeionaje nchi yako?

Hata kama ungekufa au usiporudi ungefarijika na ungekufa kwa amani kwa kuhisi kuwa watu wa nchi yako walikuwa wanakupenda, taifa lako lilikuwa linakupenda.

Tunahitaji haya mambo kuyaweka Sawa kabla maji hayajazidi UNGA.

Tunaushahidi wa kutosha kuwa ubabe haujawahi kuwa suluhu linapokuja swala la mambo ya uhai. Tunaona huko Gaza.

Chondechonde SERIKALI na vyombo vya Dola. Shughulikieni hilo jambo kwa akili, UPendo, na HAKI.

Soma Pia:

Mambo ya kusema sijui ubabe sijui nani mkubwa hiyo haitasaidia nchi yetu. Zaidi sana tutawapa adui zetu nafasi. Adui tunaowajua na wale tusiowajua.

Mimi acha nipumzike Sasa. Tutasimama upande wenye HAKI.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Cdm watakuwa wajinga sana kukaa kimya huku wafuasi wao wakiendelea kuuwawa na vyombo vya dola. Watu wataogopa kujiunga na cdm maana wataona hawako salama kwa kujiunga na chama hicho. Na njia hizi za machafuko ndio zitafanya nchi yetu kupata mabadiliko ya kweli.
 
Umeeleweka ,lini utakuja ngelengele TUNU nguo ,huku tayari kumejengwa ofisi ya halimshauri morogoro DC ,uje ndg yangu ikifika hapa uwanjani nambie
 
Sasa Bunge la kijani linaweza chukua hatua ipi Kwa sa100?

Maandamano ni njia ya wazi na direct ya kuonyesha kutaka HAKI na mabadiliko.

Ndio maana Mimi sijayapinga na nimeishauro serikali nini chakufanya, kutoa HAKI

Ila Maandamano yanayohamasisha kuangushwa kwa serikali hayo napinga kwa sababu hayapo kisheria. Yaani sidhani kama kuna sheria inaruhusu serikali kuangushwa kwa maandamano.

Kama Samia hafai Mwakani sio mbali, wapige Kura. Kama atashindwa sawa. Kama atashinda sawa. Kama ataiba kura hiyo tutaipinga. Kama mpinzani atashinda kwa kuiba kura tutaipinga
 
Akili kazi yake ni kutafuta suluhu kwa njia isiyoumiza. Akili hizo ninaamini viongozi mnazo sema mnataka kufanya Makosa ya kiufundi kwa kutumia nguvu zisizohitajika.
Mkuu, ni vizuri kusoma maandiko yako; lakini wakati mwingine yana chekesha kidogo hata kama ni kuhusu mambo yasiyo hitaji kucheka.

Simama upande wa hao hao unao wasema humu, na jaribu kujua msukumo unao wafanya wafanye haya. Ni dhahiri kuna mambo wanayaogopa na wanajaribu kuzuia kwa kila njia yasitokee.

Hawa siku nyingi wame faidika na njia hizo hizo za mabavu. Nafasi wanazo shikilia sasa hivi ni matokeo ya mabavu hayo hayo wanayo jaribu kuyatumia, bila ya kujali kama safari hii yataendelea kuwa hakikishia mafanikio yale yale.

Njia hizo zimefanikiwa, hadi sasa, lakini kumeanza kuonekana usugu kwa hao wanao tishiwa; kwamba liwalo na liwe na wawo hawatarudi nyuma. Hali ndiyo hiyo sasa
'Who is going to blink'?
 
Cdm watakuwa wajinga sana kukaa kimya huku wafuasi wao wakiendelea kuuwawa na vyombo vya dola. Watu wataogopa kujiunga na cdm maana wataona hawako salama kwa kujiunga na chama hicho. Na njia hizi za machafuko ndio zitafanya nchi yetu kupata mabadiliko ya kweli.

Ni kweli Kabisa.
Hata Watanzania na watawala wapenda Haki hawatakubali Kuona kundi Fulani miongoni mwa Watanzania linakandamizwa alafu wakakaa kimya
 
Mkuu, ni vizuri kusoma maandiko yako; lakini wakati mwingine yana chekesha kidogo hata kama ni kuhusu mambo yasiyo hitaji kucheka.

Simama upande wa hao hao unao wasema humu, na jaribu kujua msukumo unao wafanya wafanye haya. Ni dhahiri kuna mambo wanayaogopa na wanajaribu kuzuia kwa kila njia yasitokee.

Hawa siku nyingi wame faidika na njia hizo hizo za mabavu. Nafasi wanazo shikilia sasa hivi ni matokeo ya mabavu hayo hayo wanayo jaribu kuyatumia, bila ya kujali kama safari hii yataendelea kuwa hakikishia mafanikio yale yale.

Njia hizo zimefanikiwa, hadi sasa, lakini kumeanza kuonekana usugu kwa hao wanao tishiwa; kwamba liwalo na liwe na wawo hawatarudi nyuma. Hali ndiyo hiyo sasa
'Who is going to blink'?

Ndio maana nikaandika watumie AKILI
Kujua na Kuona na kutofautisha nyakati ni sehemu ya AKILI.
Zamani watu walikuwa wanaogopa Polisi siku hizi hawaogopi.

Ninachoandika ni kuweka mambo sawa ili yasiharibike sana
 
Ndio maana Mimi sijayapinga na nimeishauro serikali nini chakufanya, kutoa HAKI

Ila Maandamano yanayohamasisha kuangushwa kwa serikali hayo napinga kwa sababu hayapo kisheria. Yaani sidhani kama kuna sheria inaruhusu serikali kuangushwa kwa maandamano.

Kama Samia hafai Mwakani sio mbali, wapige Kura. Kama atashindwa sawa. Kama atashinda sawa. Kama ataiba kura hiyo tutaipinga. Kama mpinzani atashinda kwa kuiba kura tutaipinga
Yaani utekaji uendelee Hadi uchaguzi ufike?

Kipi Rahisi, Yeye kueafuta KAZI IGP na Masauni, au awaache wamgharimu?
 
Leo jioni nimepishana na polisi wengi mmoja kabeba mguu wa mtu begani alafu inavyoonekana wameukata muda siyo mrefu
 
Kwema Wakuu!

Nimeona nami kwa nafasi yangu hata kama ni ndogo, niishauri serikali kuhusu haya maandamano ya hawa ndugu zetu wa CHADEMA.

Hakuna haja ya kutumia mabavu na ubabe kuzuia CHADEMA kuonyesha hisia za Maumivu ya ndugu zao waliouawa na kutekwa. Ni wanachama wenzao.

Haitakuwa HAKI.
Nilikuwa najaribu kujishawishi kuwa Wanachadema wasifanye maandamano na niwe upande wa serikali lakini nimeona Sina hoja ya kupinga maandamano hayo.

Ikiwa lengo kweli ni kuomboleza, kukemea na kuitaka serikali ichukue hatua kwa HAKI za wanachama wao na Watanzania wengine waliotekwa na kuuawa na kutojulikana walipo, sioni tatizo la maandamano.

Mimi napinga Kauli ya "Samia Must Goo" kwani hiyo ni nje ya utaratibu wa sheria zetu. Hiyo wasubiri Mwakani 2025.

Wanahaki kwa sababu:

1. Waliotekwa na kuuawa ni wanachama wenzao. Kutochukua hatua zozote itaashiria kuwa chama chao hakiwezi kupigania Haki za Wanachama wenzao.

Hata hivyo ilitakiwa maandamano haya yafanywe na wananchi wote wa Tanzania.
Lakini kwa vile sisi sio kitu kimoja hiyo haitawezekana.

2. Wanahaki kwa Sababu wenye wajibu ambao ni serikali imeshindwa kufanya sehemu yake kutafuta wanaofanya hayo matukio u mauaji na UTEKAJI.

Hii inawafanya wao wenyewe kutetea haki za wanachama wenzao. Hii itamaanisha kuwa kuwa mwananchi wa chama cha Demokrasia Hauna Haki na hata ukiuawa hautakuwa n tofauti na sungura au panya Buku. Tena Bora sungura huko TANAPA wanalinda wanyamapori.

NINI KINAJENGEKa IKIWA SERIKALI HAITACHUKUA HATUA STAHIKI NA IKITUMIA MABAVU;

1. Chuki na Visasi vitajengeka.
Chuki baina ya wanachama wa CHADEMA na serikali(CCM) itazidi kukua.

Mtu anaweza kusamehe Makosa mengi lakini kosa la kumuua mzazi wake au Mtoto wake ni kosa ambalo kikawaida halitakiwi kusamehewa. Ni kosa la kulipa Kisasi. Na ni HAKI Kisasi kilipwe ikiwa Haki ya kawaida haikutendeka.

Inaweza kuwa, kwa vile wanaotendewa hayo wakadharauliwa kwa sababu ni Wachache na hawana nguvu lakini mambo ya Haki hayaendagi hivyo. Tusifanye watu waichukie nchi yao na wananchi wao.

Kwa sababu kama wananchi watakaa kimya wakati watu wenzao wanauawa itahesabika kuwa waliungana na WAUAJI kufanya uhalifu huo.

Hiyo ni sababu ya matendo mabaya ya kigaidi yanayoendelea Duniani. Ni hatari sana.

2. Nchi kupasuka na kukosa utulivu.

Matendo haya kikawaida hayawezi kufurahisha viongozi wote waliopo kwenye vyombo vya Dola.
Wapo viongozi ambao huweza kuingia na moyo wa Imani na Kuona kinachoendelea sio chema. Hii hupelekea Dola kupasuka na nchi kukosa utulivu.

Tunaona nchi kama Libya kwa Hayyati Gadafi, Iraq kwa Sadamu Hussein. Yanapotokea matukio ya ukandamizaji wa kundi Fulani ni rahisi kwa adui kuivuruga nchi.

Kwa sisi watibeli tunajua, matokeo ya uovu.

Yuda alipomsaliti Yesu akamuuza kwa vipande vya fedha baadaye aligundua kuwa Ile fedha Haina maana yoyote, matokeo yake akaona airudishe kisha akaenda kujiua sababu ya Hatia.

Hatia ndio huifarakanishaga watawala. Linazuka tuu kundi linaona yanayoendelea sio sawa na jingine linaona sawa alafu Kuna kuwa na uwiano wa kinguvu. Mwishowe nchi inapasuka au kuchafuka.

3. Wasio na vyama ambao ni sisi nasi tutachoka Kuona kundi Fulani likiumizwa.

Watanzania wengi hawana vyama lakini hiyo haimaanishi hawafuatilii siasa. Hatutaki chama au kundi Fulani lionewe. Makundi na vyama vyote vipewe HAKI sawa.
Hatutaki Dini Fulani ionewe au ipendelewe tunataka Dini zote na wasio na Dini wapewe HAKI sawa.

Sisi tusio na upande ambao ndio wengi tunataka mfanye mambo yenu bila kuoneana na kufanyiana dhulma.

Hatutaki nchi yetu ichafuke. Hatutaki nchi yetu ipasuke vipande vipande au kugawanyika kama Sudan kaskazini na Sudani Kusini.

Tunataka nchi Moja. Na nchi Moja ni Ile ambayo Kuna usawa na Haki baina ya watu na makundi yao. Hakuna chama chenye mamlaka au Haki zaidi ya vyama vingine.

Kukosekana umoja na kundi linalotaka kujipendelea na kukandamiza makundi mengine ndilo litahesabika kama linaloivuruga Amani ya nchi hii. Kila kundi linalohaki ya kujilinda na kutetea HAKI zake ikiwa litaona kuwa linaonewana kudhulimiwa.

Serikali, mambo haya hayahitaji nguvu na mabavu. Hatutaki Kuona watu wanapigana na kumwagana Damu na ubongo bila sababu ya msingi.

Akili kazi yake ni kutafuta suluhu kwa njia isiyoumiza. Akili hizo ninaamini viongozi mnazo sema mnataka kufanya Makosa ya kiufundi kwa kutumia nguvu zisizohitajika.

Wewe kiongozi utakayezuia maandamano kabla hujafanya hivyo lazima ujiulize;

Wewe Baba yako au Mtoto wako ndio angekuwa ameuawa au kutekwa na hajulikani alipo usingeandamana?
Yaani assume hao watoto wako ambao wako salama au huyo Babaako unayempenda aliyesalama angetokea mtu akamuua kwa kifo cha kikatili au akatekwa usingeandamana?

Au fikiria wewe ndio umeuawa, au umetekwa uko matekani kwa watesi wako. Alafu ukasikia watoto na watu wanaandamana kwaajili yako ungejisikiaje? Ungewachukuliaje Wananchi wenzako?
Ungeionaje nchi yako?

Hata kama ungekufa au usiporudi ungefarijika na ungekufa kwa amani kwa kuhisi kuwa watu wa nchi yako walikuwa wanakupenda, taifa lako lilikuwa linakupenda.

Tunahitaji haya mambo kuyaweka Sawa kabla maji hayajazidi UNGA.

Tunaushahidi wa kutosha kuwa ubabe haujawahi kuwa suluhu linapokuja swala la mambo ya uhai. Tunaona huko Gaza.

Chondechonde SERIKALI na vyombo vya Dola. Shughulikieni hilo jambo kwa akili, UPendo, na HAKI.

Soma Pia:

Mambo ya kusema sijui ubabe sijui nani mkubwa hiyo haitasaidia nchi yetu. Zaidi sana tutawapa adui zetu nafasi. Adui tunaowajua na wale tusiowajua.

Mimi acha nipumzike Sasa. Tutasimama upande wenye HAKI.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Hawa chadema wakiandamana chonde chonde wasije kutumia nguvu kuwaumiza watu itakua shida zaidi maana itapanda mbegu mbaya sana.
 
Back
Top Bottom