Naishauri serikali Kesho isije Ikatumia mabavu, iache CHADEMA wafanye maandamano yao kwa Amani

Ndio maana nikaandika watumie AKILI
Kujua na Kuona na kutofautisha nyakati ni sehemu ya AKILI.
Zamani watu walikuwa wanaogopa Polisi siku hizi hawaogopi.

Ninachoandika ni kuweka mambo sawa ili yasiharibike sana
Naelewa unacho fanya. Hakuna mTanzania mwenye akili sawa, anayependa nchi hii anafurahishwa na haya yanayo tokea sasa.
Wezi, wadokozi, majambazi wote huanza taratibu na kupata uzoefu katika kazi hiyo hadi kufikia hatua ya kujisahau na kujimaliza wenyewe.
Mfano huo hauna tofauti kubwa na hawa viongozi tulio nao sasa.
 
Maandamano ya amani ni haki ya kikatiba, chadema wana haki kimsingi kuandamana kuonyesha hisia zao kwa wanachama wao waliouwawa.

Tatizo la autocracy, tatizo la nchi za Afrika, tatizo la nchi yetu na tatizo la ccm.
 

Ndio maana kwenye andiko langu nikasema, hatutaki nchi yetu kukosa utulivu au kupasuka vipande vipande.

Baadhi ya watawala wasiofikiri vyema huweza Kuona ni jambo gumu lisilowezekana lakini huo ni upofu tuu wa madaraka
 
Maandamano ya amani ni haki ya kikatiba, chadema wana haki kimsingi kuandamana kuonyesha hisia zao kwa wanachama wao waliouwawa.

Tatizo la autocracy, tatizo la nchi za Afrika, tatizo la nchi yetu na tatizo la ccm.

Lazima tubadilike
 
Kwa hiyo wewe unatakaje?
Au unashauri jambo gani?
Hapa tulipo fikia sidhani kuwa kuna ushauri tena.
Ninachoweza kusema bila ya woga wowote ni kwamba CHADEMA na raia wote wanao itajkia mema nchi yetu hawana tena cha kupoteza. Acha hao wanaolinda maslahi yao wafanye lolote wanalotaka kufanya. Saa ya ushauri ilisha pita muda mwingi sana ulio pita.

Na kwa namna fulani ni kama kuwaongezea muda wa kuendelea kuyumbisha taifa hili.
 

Bado hatujafika hapo ila hatupo mbali kufika.
 
Sikiliza wewe pimbi, maandamano marufuku.Period.
 
Sasa nikuombe tena.
Tusitafute njia za kuwasaidia kuendeleza maovu yao; pengine kwa kutojua/
Lakini usije ukawa unawapa 'comfort' bila kujua unafanya hivyo. Nia yako njema inaweza kutumika kuwapa ahueni wao.

Sitaki watu waumie hasa wanyonge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…