Naishauri serikali Kesho isije Ikatumia mabavu, iache CHADEMA wafanye maandamano yao kwa Amani

Naunga mkono hoja,
Hata mimi, kwanza nimeyaunga mkono haya maandamano Kufuatia Umuhimu wa Maandamano ya UKUTA: Nimehamasika, Nitashiriki, Tujitokeze kwa Wingi! Ila...!
na nikalishauri jeshi letu la polisi Jeshi la polisi likifanya vyema, lipongezwe, hongera FFU kusambaratisha maandamano bila virungu, mabomu ya machozi, risasi za moto, bila maafa! na kuwasisitiza polisi wetu Ombi Muhimu Kwa Jeshi Letu Kakamavu na Adilifu la La Polisi."Nyinyi ni Wenzetu, Kwenye Maandamano Yetu, Please Msigeuke. Gestapo au Makaburu!"
P
 

..wakati wote vyama vinawaza kubaki madarakani, na vingine vinawaza kuingia madarakani.

..hivi tunavyozungumza kuna watu wanawa " Samia must stay" , na wengine wanawaza " Samia must go. "

..sasa unaweza kuwazuia watu wasiseme, Je utawazuia kuwaza " Samia must go. "

..Mimi nadhani sio busara hivi tunavyokwenda kupangiana hata nini cha kusema.

..Zaidi nadhani wananchi wakiwa HURU kuzungumza ndivyo ambavyo serikali utajua kama inafanya vizuri, au vibaya.
 

Kuzungumza sio tatizo wala sio kosa.
Lakini kuandamana na kusema Samia Must Goo kidogo haijakaa sawa.
 
Imenibidi nicheke tu baada ya kusoma andiko lako hili.
Sina shaka yoyote huko ndiko unakolalia mwenyewe na kufanya iwe hivyo kwa wingi wa waTanzania.
Wahenga husema," tunda halidondoki mbali na mti ulio lizaa"; sasa sijui kama utauelewa vizuri msemo huu.

Ngoja na mimi nikupe ninapo simamia katika hali hiyo uliyo ielezea wewe mara kwa mara kuhusiana na tabia za waTanzania na viongozi wa aina ya Magufuli.

Siamini hata mara moja kwamba waTanzania walipenda mambo machafu aliyokuwa akifanya Magufuli; lakini naamini walipenda baadhi ya misimamo aliyo kuwa nayo juu ya nchi hii, Tanzania. Ni muhimu kutofautisha hayo mawili.

Ndiyo, hata mimi namtaka sana kiongozi asiyefanya masihala na mambo muhimu ya nchi. Kama watu maofisini ni kufanya kazi na kulipwa haki ya kazi zao, kuna kipi hapo cha kuchekeana na kubembelezana. Ndiyo, kama kiongozi hana uvumilivu na ufujaji wa mali za umma, kwa nini nisimuunge mkono mtu huyo kama anayo yafanya yamo ndani za taratibu zinazofahamika (kisheria). Ndiyo, kwa nini nisimkubali kiongozi ambaye maamuzi yake yanaonekana ni kwa manufaa ya nchi na wananchi wake; na bila kuonyesha kuwa anajitafutia sifa zisizokuwa na msingi wowote?

Nisichotaka kwa kiongozi ni uigizaji, kama huo wa Samia, Makonda, na hata Magufuli katika baadhi ya mambo.. Nataka kiongozi mkweli, anaye tumia akili, za kuchambua anayo shauriwa na wengine. Sitaki kiongozi mpenda sifa kama Magufuli. Sitaki kiongozi mwonevu kwa wengine kwa sababu tu hawakubaliani na baadhi ya mambo yake. Sitaki kiongozi anayetumia madaraka yake vibaya na kujichukulia sheria mkononi kwa sababu tu anayo madaraka na vyombo vya dola

Sasa basi, tuache kuwasingizia waTanzania kuwa na sifa hizo unazo zielezea wewe za kupenda tu kiongozi yeyote mradi anafoka na kukandamiza watu. Hili silikubali hata mara moja.

Kuna sababu muhimu sana kwa nini unafikiri waTanzania wanashindwa kuachana na CCM, pamoja na ubovu ilioufikia nyakati hizi; na kwa nini inakuwa vigumu kwao kukubali vyama vingine kama CHADEMA. Mchambuzi mzuri wa maswala haya anatakiwa aainishe kwa nini hali iko hivyo, siyo kukimbilia tu kuwalaumu waTanzania kirahisi rahisi.
Hata hivyo, ni wazi sasa CCM yenyewe Samia kaimaliza, kama hapatatokea watu makini wa kuirudishia uimara wake iliowahi kuwa nao.
CHADEMA wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuanza kuwavuta waTanzania kama mbadala iwapo kama wataachana na baadhi ya mambo yaliyokuwa yakiwadidimiza siku za nyuma.

Sijui kama nitakuwa na muda tena wa kuendeleza majadiliano haya katika hali hii ya sasa.
 
Jf Waendelee kukupa tuzo ya ujinga tuu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Vibaraka Wameshughulikiwa ipasavyo

View: https://x.com/Kipanga1986/status/1838195046467645818?t=MAu17qF7lsVEEn9Iw90tcQ&s=19
 
Reactions: Tui
Ushauri wako umepuuzwa na utawala wa kidikteta
 

"Njia pekee ambayo Wananchi wataitumia katika kuzungumza au kujadiliana na Watawala wao ambao ni madikteta ili kufikia muafaka wenye maslahi kwa pande zote mbili ni kwa kupitia mtutu wa bunduki."

Jeff's O'Brien.
 
Ndio maana nikaandika watumie AKILI
Kujua na Kuona na kutofautisha nyakati ni sehemu ya AKILI.
Zamani watu walikuwa wanaogopa Polisi siku hizi hawaogopi.

Ninachoandika ni kuweka mambo sawa ili yasiharibike sana
Aya yako ya pili inasemaje,?Wangeandamana waone kama wanatania.Ulete uchochezi wa kuchochea vurugu uachwe.Rwanda walianza hivi hivi kuwakejeli wengine kwa lugha za kichochezi na tunajua kilichotokea.Hakuna kucheka na mchochezi.
 
Aya yako ya pili inasemaje,?Wangeandamana waone kama wanatania.Ulete uchochezi wa kuchochea vurugu uachwe.Rwanda walianza hivi hivi kuwakejeli wengine kwa lugha za kichochezi na tunajua kilichotokea.Hakuna kucheka na mchochezi.

Mambo yameisha kwa utulivu.

Serikali ifuatilie hoja za wananchi wake(hao Wanachadema)
 
Kuzungumza sio tatizo wala sio kosa.
Lakini kuandamana na kusema Samia Must Goo kidogo haijakaa sawa.

..watu wanapoandamana mara nyingi huwa wana jambo lililowakera. Katika mazingira hayo lazima kutakuwepo na kauli zinazo akisi machungu ya waandamanaji.

..Na maandamano ya Chadema chanzo chake ni watu wao kutekwa, kuteswa, na kuuwawa, na watu wanaodhaniwa ni askari Polisi. Sijui kwanini tunashangaa kusikia kauli za kuwalaani Polisi, au Raisi, ambaye ni kiongozi Mkuu wa vyombo vya dola.

..Resilience ktk 4R ni pamoja na kuwavumilia wale wasioridhishwa na utendaji wa Rais Samia wanapoeleza hisia zao. Wanaosema Samia must go wana haki zilezile na sawa na wanaosema Mama anaupiga mwingi, Nani kama Mama,...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…