Ikiwa hali itaendelea kua kama ilivyo, huenda likakosa sifa ya kua jimbo la kiimani ndani ya kanisa hilo, kama yalivyo majimbo mengine ya kanisa katoliki nchini.
Kuna zaidi ya ugumu katika kuendesha shughuli za kitume kijimbo, kidekania na kiparokia katika jimbo hilo katoliki la Kondoa.
Hali ya kitume ya watawa wa kike na kiume, inafedhehesha sana na kwakweli inasikitisha sana.
Hayati mhashamu baba Askofu Bernadine Mfumbusa alifanya kazi kubwa na ngumu sana Kondoa, nadhani ipo kazi ngumu zaidi ya kimkakati inatakiwa kufanyika kulisimamia jimbo hilo. Ni muhimu sana TEC kulitazama hili na kuchukua hatua muafaka za makusudi za mapema sana kabla ya hali ya kitume jimboni humo kua mbaya na ngumu zaidi.🐒
Mungu Ibariki Tanzania