Naishi kwenye Nyumba ya kupanga mwenye nyumba alifariki ghafla na ndugu hawaijui hii nyumba

Kwa dunia ya leo hamna kitu kama hicho, kwamba hakuna hata waliomuzia huyo boss marehem kiwanja? hakuna hata watu wachache aliowahi kuja nao kutembelea hicho kiwanja? Kwamba hakuna hata fundi aliyejenga hiyo nyumba kuanzia msingi mpaka finishing? Ikiwa umepata bahati ya kuishi kwa muda ishi lakini usidhani kama iko siku utamiliki hiyo nyumba.
 
Kama ipo bagamoyo hiyo nyumba tunaijua na nyingine ipo mwanza kwa mchepuko wake pamoja na fremu zake. Na kuna gari yake pia mule..
 
Huu mbona kama wivu aisee
 
Hii habar kama ni ya kweli,ningekuwa mimi kwanza ile hela ya kodi ningekuwa naiweka bank kana kwamba namlipa mwenye nyumba,huku nafanya jitihada za kumpata mmliki wa nyumba hiyo

Siku wakipatikana nawaambia nadaiwa miezi kadhaa na hela yenu ipo niliihifadhi,hakika utakuwa umetenda haki mbele ya Mungu wako,na kwa neema ya Mungu huenda hata kodi iliyopita wahusika wakakusamehe kwakuwa ungekuwa na uwezo wa kuwadhulumu lkn hukufanya hivyo

Ila vyovyote itakavyokuwa haki ya mtu huwa haipotei,ipo siku tu kwa namna usiyotarajia unajikuta wenyewe hawa hapa
 
Taratibu za kufungua mirathi hadi kukamilika ni miezi 8 au siyo?
Hilo Mimi sijui wanajua wao ila nimekuambia nimesikia fununu Sasa wewe unaforce kwamba miezi 4 wanagawanaje Mali wakati nimesema mzee kafa mwezi wa 4 mpaka Leo mwezi wa 12 naona kimya na nimesikia fununu ndio maana nikakuambia kichwani kwako Kuna shida ya kupiga hesabu
 
Umesema kweli kabisa Hata asipowapa kodi akabidhi nyumba yao
 
Kwahiyo hiyo miezi 8 ndiyo inatosha kugawana mali? wapi nimeforce miezi minne? tuache minne je nane ndiyo inatosha?
 
Mimi naona nimeokota sababu niliizindua mimi na yeye alikuja mara moja baada ya Mimi kuhamia nikasikia kafariki baada ya kupata taarifa kutoka Kwa maboss wenzie

Sasa ndugu siwajui na yeye alikua anasema ni Siri anataka awafanyie suprise
Punguza utoto.
 
Ndio maana mi sitaki mambo ya siri kabisa
Ni mabay sana basi watu hawajui tu,baba yetu naye alikuwa na mambo kama hayo,kuna mashamba na viwanja alidhulumiwa kwa kupenda usiri usiri

Binafsi sitakuja kufanya haya mambo,mimi ni nafsi mda wowote nipo safarini kwa mola wangu
 
Kama unajua amefariki lazima utajua msimba ulipo au alipozikwa majiran wenzie walojenga pamoja wanamjua
 
Epuka laana /balaa vitu vya namna hiyo mwisho wake ni mmbaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…