Naishindaje hofu ya kifo inayoniandama?

Naishindaje hofu ya kifo inayoniandama?

Kufaham haya mambo yote ni jambo moja, lakini kukubaliana na huo ukweli ni jambo lingine.

Hatua unayotakiwa kuifanya nikuiambia nafsi yako kwamba kifo kipo, ipo siku utaondoka, utaanza maisha mengine. Hii huzuni tunakua nayo mpendwa wetu akiondoka itakua non of your business siku yako ikifika, wewe utakua unapambana na miamala mingine tofauti kabisa ( hakuna hata mmoja wetu anaejua nini hua kinaendelea huko). Sasa usijitaabishe kwa mambo usiyoyajua.

Kama una imani kwamba ipo hukumu baada ya haya maisha, ishi njia iwapasayo watakaokula pepo huko mbinguni.
Nitakua kila siku asubuhi na jioni najiambia haya maneno.
Ahsante.
 
Mkuu, huo upweke uliyonao ndio chanzo cha mawazo na hofu uliyonayo. Tafuta mtu uishi nae, iwe mpenzi au hata ndugu yako. Maana muda mwingi baada ya kazi utakuwa ukipiga nae story mpaka wakati unasinzia.

Hilo ni tatizo la muda tu na baadae hutoweka
Hii nayo ni point ya muhimu i think.
 
Nitakua kila siku asubuhi na jioni najiambia haya maneno.
Ahsante.

Nakutakia mafanikio mkuu. Pia jiulize kwa utulivu, unaogopa kitu gani hasa? Ni kipi unachokiogopa? Utaanza kuona jinsi ambavyo uoga na hofu inakuzuia kufurahia maisha, na inaweza kukuathiri vibaya sana.

Na siku zote usipende sana kutafakari au kuyawaza mambo mabaya, yananyongonyeza nafsi na mifupa.
 
Mkuu naogopa kufa kwa sababu nitawaacha ndugu na marafiki zangu ninaowapenda, naogopa kufa kwa sababu ukishakufa, unapelekwa kaburini kufukiwa, sijui nini kitaendelea huko, sielewi. Nitakosa ufahamu wa yanayoendelea duniani hapa, nitaacha vitu vyote vizuri vya hii dunia na vitu vyote ambavyo nimevihangaikia maisha yangu yote. Nitalala usingizi wa milele....
 
Wakuu salama?
Hivi karibuni, hasa kwa mwaka huu wa 2021 nimoepoteza watu wa karibu wengi sana tangu huu mwaka uanze; Nimepoteza wazee wangu-baba wakubwa wanne, pia nimepoteza marafiki zangu wale wa inner cycle watatu,akiwemo rafiki yangu mmoja wa karibu sana aliefariki kwa kansa ya utumbo, na jamaa zangu wengine kadhaa (ndugu wa mbali na marafiki).
Pia, kuna vifo viwili vya wana JF vya hivi karibuni ambavyo vimenigusa sana, cha ip_mob na warumi hawa watu nilikua nawakubali sana hapa JF japo sijawahi kukutana nao uso kwa uso.
Hivi vifo kwa huu mwaka vimenifanya nimekua mtu wa hofu sana juu ya kifo; Yaani sasa hivi nawaza sana juu ya kifo na nashikwa na uoga wa kutisha hadi natetemeka. Mara nyingi usiku nakosa kabisa usingizi, nawaza juu ya kifo hadi machozi yananitoka. Saa zingine naogopa hata kulala usiku na kuufukuza usingizi, maana nawaza kuwa naweza nikalala nisiamke tena, nikapotelea usingizini na kuaga dunia. Hii hali naona imeanza kuathiri shughuli za mihangaiko yangu, kwani mchana nakua nimechoka sana na pia inanikosesha amani kabisa naishi maisha ya wasiwasi sana.
Ndugu zangu, nimekuja humu kuwauliza je nyie wenzangu mnatumia mbinu gani kuondoa hofu juu ya kifo au kuwafanya msiwaze au kuogopa kifo?
Nimejaribu kuwa nasali sana na kwenda kanisani kila siku, nimeongea pia na mchungaji na amenifanyia maombi na kunipa nasaha, lakini bado imekua ngumu sana kwa mawazo na uoga huo kunitoka.
Naomba mnisaidie ndugu zangu nawezaje kupambana na hii hali?

Naomba mnisaidie wadau.
Ahsanteni.
Nenda kwa bishop Mkandamizaji akuombee hofu yote itapotea, wahi sasa
 
Post traumatic stress disorder ukienda hospital itakuwa poa sana kabla hali haijawa mbaya sana maana unakoelekea utavurugwa
 
Njoo inbox nitakusaidia Bro Cha kufanya
Hofu inatoka Kwa shetani
 
Kwanza pole kwa hali hiyo na hongera kwa kuwa muwazi.

Kwa hali yako kuna mawili, na nitayagusia yote hapa iwe msaada kwa wengine pia;

• Kwanza unaweza ukawa unasumbuliwa na hiyo hali kutokana na hayo uliyoyapitia ya kupotelewa na watu wako wa karibu kwa kipindi kifupi, kwahiyo imekupa death anxiety ( hofu ya kifo) akilini mwako kitaalamu inaitwa Thanatophobia

•Pili unaweza pia ukawa unasumbuliwa na gastroesophageal reflux disease ( GERD ) au Gastritis, au ulcers. Haya magonjwa pia hupelekea mgonjwa kupata hali kama ya kukata roho, kuona anaishiwa pumzi wakati mwingine as if anaenda kufa. Stress, ulaji mbaya unaeza ukachangia hii hali.

Solution:

• Kama unahisi una dalili nyingine pia za kuumwa tumbo au tumbo kujaa gesi na constipation then likely hii ndo sababu ya tatizo lako na uende hospital mapema

• Kama sio sababu ya kwanza hiyo then ni death anxiety.

Kwa kuanzia nikutoe hofu mkuu, siku zote anayekufa hajui kwamba sasa nakufa, ikitokea mtu akajua haitaambatana na hofu.
Yaani ukiona unahisi kufa jua huwezi kufa hata siku moja, kifo ni siri na huja bila mtu kuwaza au kujua, ndo maana utasikia nilikuwa naye tu hapa akaniambia nakuja ila ndo akaenda moja kwa moja.

Sasa basi popote ukiisikia hiyo hali iambie nafsi yako mwenyewe maneno haya, Kifo ni Siri aijuaye Mungu, ukiona unahisi kufa huwezi kufa kweli maana ni siri anayeijua Mungu, hivyo kufa kwako itakuwa kama uliweza kuona future kitu ambacho sio kweli ( kwa lugha nyepesi huwezi kupiga chabo kitakachotokea baadaye ) kwa namna hii endelea kujiambia kila mara mpaka ile anxiety na hofu zitapungua na kuisha.. Hii njia kitaalam inaitwa Exposure Therapy, lakini vile vile usali kwa imani yako

Vile vile usikae sana peke yako, kaa hata kwenye vijiwe vya michezo au chochote unachoweza kuenjoy na watu wengi au fuatilia vipindi vya kukukeep busy.

Pole sana chief, ukizingatia hayo hiyo hali itaisha mapema hata wewe mwenyewe utasahau
 
COVID 19 + MAGUFULI= FAILURE.
Biashara zilizoanza kipindi cha MAGUFULI nyingi zimekufa.
Hata Mimi niliacha biashara baada ya kuona inaleta stress tu.
 
Amini kwamba kifo ni tukio la asili,halikwepeki, lisubiri kama unavyosubiria mwaka mpya au X- mas. Kuwa tu na matendo mema ili ukumbukwe kwa mema sio mabaya
 
Post traumatic stress disorder ukienda hospital itakuwa poa sana kabla hali haijawa mbaya sana maana unakoelekea utavurugwa
Kwa hiyo unanishauri niende hospitali mkuu? na nikifika kwa daktari nimwambie shida yangu mimi nina hofu sana ya kifo? Nitasaidika?
 
Kwanza pole kwa hali hiyo na hongera kwa kuwa muwazi.

Kwa hali yako kuna mawili, na nitayagusia yote hapa iwe msaada kwa wengine pia;

• Kwanza unaweza ukawa unasumbuliwa na hiyo hali kutokana na hayo uliyoyapitia ya kupotelewa na watu wako wa karibu kwa kipindi kifupi, kwahiyo imekupa death anxiety ( hofu ya kifo) akilini mwako kitaalamu inaitwa Thanatophobia

•Pili unaweza pia ukawa unasumbuliwa na gastroesophageal reflux disease ( GERD ) au Gastritis, au ulcers. Haya magonjwa pia hupelekea mgonjwa kupata hali kama ya kukata roho, kuona anaishiwa pumzi wakati mwingine as if anaenda kufa. Stress, ulaji mbaya unaeza ukachangia hii hali.

Solution:

• Kama unahisi una dalili nyingine pia za kuumwa tumbo au tumbo kujaa gesi na constipation then likely hii ndo sababu ya tatizo lako na uende hospital mapema

• Kama sio sababu ya kwanza hiyo then ni death anxiety.

Kwa kuanzia nikutoe hofu mkuu, siku zote anayekufa hajui kwamba sasa nakufa, ikitokea mtu akajua haitaambatana na hofu.
Yaani ukiona unahisi kufa jua huwezi kufa hata siku moja, kifo ni siri na huja bila mtu kuwaza au kujua, ndo maana utasikia nilikuwa naye tu hapa akaniambia nakuja ila ndo akaenda moja kwa moja.

Sasa basi popote ukiisikia hiyo hali iambie nafsi yako mwenyewe maneno haya, Kifo ni Siri aijuaye Mungu, ukiona unahisi kufa huwezi kufa kweli maana ni siri anayeijua Mungu, hivyo kufa kwako itakuwa kama uliweza kuona future kitu ambacho sio kweli ( kwa lugha nyepesi huwezi kupiga chabo kitakachotokea baadaye ) kwa namna hii endelea kujiambia kila mara mpaka ile anxiety na hofu zitapungua na kuisha.. Hii njia kitaalam inaitwa Exposure Therapy, lakini vile vile usali kwa imani yako

Vile vile usikae sana peke yako, kaa hata kwenye vijiwe vya michezo au chochote unachoweza kuenjoy na watu wengi au fuatilia vipindi vya kukukeep busy.

Pole sana chief, ukizingatia hayo hiyo hali itaisha mapema hata wewe mwenyewe utasahau
Ahsante sana mkuu.... Nadhani shida yangu ni hiyo namba moja, maana sina issue yoyote mwenye tumbo. Nitaifanyia kazi hii EXPOSURE THERAPY. Pia, nitaongeza kujichanganya nisiwe nakaa sana peke yangu kama ulivyoshauri. Nawaza jioni niwe naenda gym nakamua zoezi hata hadi mida ya saa tatu nne hivi, nikitoka hapo ndo niende ghetto.
 
Kwa namna yoyote ile wewe ni mkristo yes wewe ni mkristo kwa maana kama ungekuwa ni muislam lazima msiba mmoja au miwili kati ya hiyo ungeingia kaburini kumzika ndugu yako, na katika hatua hiyo hutokaa uogope kufa maisha yako yote. Utaratibu wa kiislam unafanya watu wajiandae na kifo bila hofu.
 
Kwa hiyo unanishauri niende hospitali mkuu? na nikifika kwa daktari nimwambie shida yangu mimi nina hofu sana ya kifo? Nitasaidika?
Yaah ukienda hospital ambayo ina kitengo cha matatizo ya akili itakuwa poa zaidi maana utakutana na madaktari wa vitu kama hivyo
 
Kwa namna yoyote ile wewe ni mkristo yes wewe ni mkristo kwa maana kama ungekuwa ni muislam lazima msiba mmoja au miwili kati ya hiyo ungeingia kaburini kumzika ndugu yako, na katika hatua hiyo hutokaa uogope kufa maisha yako yote. Utaratibu wa kiislam unafanya watu wajiandae na kifo bila hofu.
Mimi ni mkristo yes mkuu, ila nimewahi kuingia kaburini mara mbili kuzika jamaa zangu wa karibu. Tena mara moja ni mwaka huu, huyo rafiki yangu wa karibu sana niliemzungumzia kwenye post yangu aliefariki kaa ambae pia nilikua nashirikiana nae kwenye biashara yeye alikua muislam, na nilishiriki kuuuingiza mwili wake kaburini. Ilikua siku ngumu sana kwangu, lakini bado haikusaidia kuiondoa hii hofu kabisa mkuu.
 
Back
Top Bottom