Mpigadili Tz
JF-Expert Member
- May 4, 2015
- 1,093
- 2,046
Fanya ibada sana, utaamini Kifo kipo na ipo siku utakufa ila hutoogopa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahahahaha...!! umenifurahisha mkuu.Ushauri wako usiguse pesa yake tafadhali.
Maana kuna watu washaanza kuimezea mate laki 8 yake
Ahsante kwa ushauri mkuuFanya ibada sana, utaamini Kifo kipo na ipo siku utakufa ila hutoogopa
Natamani na mimi nifikie hatua yako angalau.Mkuu unahofu kwamba ukilala pengine utafia usingizini usiamke kesho - kwangu mie kungekuwa na kuchagua aina ya kifo ningechagua hiki.
Process ya kuteseka kwa kuugua, na pengine kwa muda mrefu, na kuwa tegemezi kwa kutojiweza, ndiyo tishio.
Tafuta mke uoe, au tumia mtandao kukuweka bize kama youtube n.k ingawa pia ni gharamaMara nyingi nikitoka kwenye mihangaiko yangu, narudi ghetto kwangu ambapo naishi peke yangu, so mida ya kuanzia saa moja usiku kuendelea most of the time huwa nakuwa peke yangu.
Hiyo ya kusurf mitandaoni huwa naifanya, ila sasa mwisho wa siku huwa najikuta na huko mitandaoni tena naanza ku-google habari za kuhusu kifo, kusikiliza miziki ya kuomboleza... Mfano ule mziki wa Dr. Remmy wa "Kifo hakina huruma" yaani upo kwa playlist yangu youtube, nimeusikiliza sana mwaka huu, huwa nausikiliza hadi machozi yananitoka... So hiyo mbinu ya kushinda kwenye internet inaishia kuleta matokeo yale yale nisiyoyataka.Tafuta mke uoe, au tumia mtandao kukuweka bize kama youtube n.k ingawa pia ni gharama
I hope na mimi nitafikia hatua hii aiseeMe siogopi kitu,kama nitakufa poa tu.Siku hizi nakula nitakacho na kunywa kwa sana tu.Itajulikana mbele ya safari huko
Hahahahahahaha.....!! Unadhani hicho ndo kiini cha tatizo mkuu?Tafuta demu mkuu
Wakristo hawaziki, wanafukia. Waislam wao wanazika hasa.. na sheria zao ni watu kuingia kaburini kwa namba isiyogawanyika kwa 2 na watu wasiozidi 7. Ndani kaburini mnapokea maiti ikiwa imefunikwa sanda tu mnaibeba na kuiweka ndani ya mwanandani taratibu na kwa hali ya unyenyekevu, hali hii huchukua hadi dk 10 na ushee, kama ni ndugu yako yaana unampokea kama tu mtu aliyehai maana mwili wake unakuwa na sanda pekee, mnamweka vizuri kisha mnafunika na miti/mbao/vimawe vya kuchonga nk. Mkimaliza mnatoka ili kuruhusu wafukia udogo wafukie kaburi vizuri. Hali hii hukupa ujasiri hutokaa uupate duniani.Mimi ni mkristo yes mkuu, ila nimewahi kuingia kaburini mara mbili kuzika jamaa zangu wa karibu. Tena mara moja ni mwaka huu, huyo rafiki yangu wa karibu sana niliemzungumzia kwenye post yangu aliefariki kaa ambae pia nilikua nashirikiana nae kwenye biashara yeye alikua muislam, na nilishiriki kuuuingiza mwili wake kaburini. Ilikua siku ngumu sana kwangu, lakini bado haikusaidia kuiondoa hii hofu kabisa mkuu.
On bed mnashonana unakumbuka kuhusu kifo mtarimbo unalala doro:Tafuta demu mkuu
Mkuu suluhisho lako ni kuhakikisha kwamba most of the times hauwi pekeyako, hupaswi kukaa au kulala pekeako.Hiyo ya kusurf mitandaoni huwa naifanya, ila sasa mwisho wa siku huwa najikuta na huko mitandaoni tena naanza ku-google habari za kuhusu kifo, kusikiliza miziki ya kuomboleza... Mfano ule mziki wa Dr. Remmy wa "Kifo hakina huruma" yaani upo kwa playlist yangu youtube, nimeusikiliza sana mwaka huu, huwa nausikiliza hadi machozi yananitoka... So hiyo mbinu ya kushinda kwenye internet inaishia kuleta matokeo yale yale nisiyoyataka.
Hilo la kuoa nalifanyia kazi soon mkuu.
Soma Zaburi 34:4 na Mathayo 11:28Wakuu salama?
Hivi karibuni, hasa kwa mwaka huu wa 2021 nimoepoteza watu wa karibu wengi sana tangu huu mwaka uanze; Nimepoteza wazee wangu-baba wakubwa wanne, pia nimepoteza marafiki zangu wale wa inner cycle watatu,akiwemo rafiki yangu mmoja wa karibu sana aliefariki kwa kansa ya utumbo, na jamaa zangu wengine kadhaa (ndugu wa mbali na marafiki).
Pia, kuna vifo viwili vya wana JF vya hivi karibuni ambavyo vimenigusa sana, cha ip_mob na warumi hawa watu nilikua nawakubali sana hapa JF japo sijawahi kukutana nao uso kwa uso.
Hivi vifo kwa huu mwaka vimenifanya nimekua mtu wa hofu sana juu ya kifo; Yaani sasa hivi nawaza sana juu ya kifo na nashikwa na uoga wa kutisha hadi natetemeka. Mara nyingi usiku nakosa kabisa usingizi, nawaza juu ya kifo hadi machozi yananitoka. Saa zingine naogopa hata kulala usiku na kuufukuza usingizi, maana nawaza kuwa naweza nikalala nisiamke tena, nikapotelea usingizini na kuaga dunia. Hii hali naona imeanza kuathiri shughuli za mihangaiko yangu, kwani mchana nakua nimechoka sana na pia inanikosesha amani kabisa naishi maisha ya wasiwasi sana.
Ndugu zangu, nimekuja humu kuwauliza je nyie wenzangu mnatumia mbinu gani kuondoa hofu juu ya kifo au kuwafanya msiwaze au kuogopa kifo?
Nimejaribu kuwa nasali sana na kwenda kanisani kila siku, nimeongea pia na mchungaji na amenifanyia maombi na kunipa nasaha, lakini bado imekua ngumu sana kwa mawazo na uoga huo kunitoka.
Naomba mnisaidie ndugu zangu nawezaje kupambana na hii hali?
Naomba mnisaidie wadau.
Ahsanteni.
Umenena kwa usahihiUkiogopa sana utakufa, usipokua na hofu hali kadhalika utakufa, usipoogopa utakufa, na hauwezi kufanya chochote kuzuia kufa.
Kikubwa shukuru kila iitwapo leo kwamba umepata nafasi ya kuifurahia siku. Ni kitu adimu na tunapewa tu sio kwamba unafanya jitihada yeyote kustahiki.
Siku ukifa, wanaopata shida ni hawa unaowaacha, yanini kujisumbua na huzuni wakati wewe utakua kwenye hali tofauti kabisa na hautaweza kufanya chochote kuhusu hawa uliowaacha?
Hapo ndio unaona kumbe hofu kubwa haisaidii kitu wala kubadili hali halisi kwamba maadam tumezaliwa, kifo hatuwezi kukiepuka.
Ndipo nalimkumbuka Mtume Paul aliposema kuishi ni Kristo, kufa ni faida.