Naishindaje hofu ya kifo inayoniandama?

Mkuu unahofu kwamba ukilala pengine utafia usingizini usiamke kesho - kwangu mie kungekuwa na kuchagua aina ya kifo ningechagua hiki.

Process ya kuteseka kwa kuugua, na pengine kwa muda mrefu, na kuwa tegemezi kwa kutojiweza, ndiyo tishio.
Natamani na mimi nifikie hatua yako angalau.
 
Mara nyingi nikitoka kwenye mihangaiko yangu, narudi ghetto kwangu ambapo naishi peke yangu, so mida ya kuanzia saa moja usiku kuendelea most of the time huwa nakuwa peke yangu.
Tafuta mke uoe, au tumia mtandao kukuweka bize kama youtube n.k ingawa pia ni gharama
 
Tafuta mke uoe, au tumia mtandao kukuweka bize kama youtube n.k ingawa pia ni gharama
Hiyo ya kusurf mitandaoni huwa naifanya, ila sasa mwisho wa siku huwa najikuta na huko mitandaoni tena naanza ku-google habari za kuhusu kifo, kusikiliza miziki ya kuomboleza... Mfano ule mziki wa Dr. Remmy wa "Kifo hakina huruma" yaani upo kwa playlist yangu youtube, nimeusikiliza sana mwaka huu, huwa nausikiliza hadi machozi yananitoka... So hiyo mbinu ya kushinda kwenye internet inaishia kuleta matokeo yale yale nisiyoyataka.
Hilo la kuoa nalifanyia kazi soon mkuu.
 
Wakristo hawaziki, wanafukia. Waislam wao wanazika hasa.. na sheria zao ni watu kuingia kaburini kwa namba isiyogawanyika kwa 2 na watu wasiozidi 7. Ndani kaburini mnapokea maiti ikiwa imefunikwa sanda tu mnaibeba na kuiweka ndani ya mwanandani taratibu na kwa hali ya unyenyekevu, hali hii huchukua hadi dk 10 na ushee, kama ni ndugu yako yaana unampokea kama tu mtu aliyehai maana mwili wake unakuwa na sanda pekee, mnamweka vizuri kisha mnafunika na miti/mbao/vimawe vya kuchonga nk. Mkimaliza mnatoka ili kuruhusu wafukia udogo wafukie kaburi vizuri. Hali hii hukupa ujasiri hutokaa uupate duniani.
 
Kuna siku usiku nilipigwa na kichomi kwenye moyo wakati nimelala, aiseeeh nilishtuka na kupiga kelele mpaka wife akashangaa, mapigo ya moto yalienda mbio balaa.

Kuanzai hapo nikawa ni mtu wa kuwazia kifo tu(kama wewe hivyo kabsa) nikawa Sitaki usiku uingie na ukiingia nikiwa kitandani nawaza labda moyo utalipuka upasuke nife,kwahiyo sikuwa kabisa na amani for almost two weeks na baadae mpaka hivi ninavyoandika suogipi chochote pamoja na kwamba bado nakumbuka like pigo la moyo.Nina uhakika 100% kama wewe ni mtu wa kukuchamganya hilo litapita faster tu.

Nakuongezea na hii, Tulikua na rafiki yetu mmoja (wa kufa na kuzikana) tulikuwa tunafanya nae kazi pale GGM, jamaa alikuwa na pesa chafu (alikuwa na kaurafiki JPM), huyu jamaa alianza kusumbuliwa na kisukari miaka ya hivi karibuni alipambana sana lakini siku moja usiku akazidiwa na akafariki.....aiseeh kuna jamaa yangu nae alikuwa na kisukari aliingiwa na hofu ya kifo kiasi kwamba kila mikikaa anawaza kufa tu, anakuuliza kama Benjamin amekufa pamoja na hela zake zile sisi hizi hela tunazotafuta ni za nini Sasa?...Kilichofata sukari yake haikuwa inashuka for almost a week licha ya kwamba anatumia dawa..sukari yake ulikuja kukubali kuwa regulated alipoacha kuogopa kifo.

Maana yangu ni kwamba, chunga sana hofu isizidi kiwango maana kupitia jamaa yangu nimejifunza kwamba hofu ni ugonjwa mwingine unaloweza kukuua.

Hupaswi kujitwika mawazo ambayo daima hautaoata suluhisho lake, utajipa msongo wa mawazo tu. Kifo hakifikiriki kabisa, no matter what tutakufa tu kwahiyo kukiwaza ni kujitia mzigo tu.
 
Mkuu suluhisho lako ni kuhakikisha kwamba most of the times hauwi pekeyako, hupaswi kukaa au kulala pekeako.
 
Soma Zaburi 34:4 na Mathayo 11:28

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Umenena kwa usahihi

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Ha ha ha imenibidi nikoment kufa tumeumbiwa binadamu na mungu alivyo wa ajabu anatusahulisha kabisa kama kuna kifo mpaka usikie Fulani kafa na we ndo unashtuka kumbe kuna kifo acha kuwaza siku ikifika utakufa tu ulale,usilale,usimame,ukae utakufa tuuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…