Naishindaje hofu ya kifo inayoniandama?

amini kwamba piga ua ipo siku utakufa, then endelea na shughuli zako. Acha kuogopa kitu ambacho ni PIE kwako
 
Ahsante mkuu.... Ulichokisema ni sawa kabisa.
Sasa mimi inanitokea tu mawazo ya hofu ya kifo yanatawala akili yangu, japo nafahamu yote uliyoandika hapo.... Sasa nitumie mbinu ipi kuyafukuza hayo mawazo au kuzuia yasije?
Puuzia !! Usiwe serious sana na maisha yenyewe, enjoy kila unapopata nafasi ya kufanya hivyo
Kufa ni lazima mkuu , i hate the idea ya kwanini tunazaliwa na kuja kufanya struggles zote hizi huku kifo kinatusubiri muda wote.
 
Hakuna asiyeogopa kifo wote tunapenda uhai.


Lakini elewa kifo ni kama chafya ikifika siku huwezi zuia. Ukiwa na afya pamoja nguvu basi fanya yatakayoufurahisha moyo wako ilimradi usikwaze watu, Mungu wala Jamhuri.
 
Kufa ni lazima, ukishajua hivyo hutakiwi kuwaza tena juu ya kifo, jua tu kwamba kuna siku utakufa, utazikwa na watu wàtakuacha peke yako kaburini. Kitakachotokea huko ndani hakuna anayejua.

Relax and enjoy life, life is for the living...
 
Pole sana jitahidi kujichanganya na watu mbalimbali, kifo kipo hakiepukiki cha muhimu ni maombi kwa sana na kumshukuru Mungu kila iitwapo leo.
 
Usijali Mkuu uwaze au usiwaze punishment iko palepale. Muhimu cha kukushauri kaa katika Imani yako ya Kiroho Uliyonayo kwa Udhabiti. Ili siku ya siku ikifika Imani Yako ikitetee..
 
Mkuu wewe unasumbuliwa na hofu kubwa..ni ugonjwa huo wa akili...ukiweza tafuta mwanasaikolojia akushauri..la tumia mbinu zifuatazo: jiepushe kukaa bure na pekeyako..jitahidi kujichanganya na marafiki wanaongea mambo tofauti na kifo, fanya mazoezi utokapo kazini maana mwili utachoka na hvo ukilala utalala fofofo.
Usichukulie poa hali hii...usipokuwa makini utajikuta ushapata uchizi kabisaa
 
Huo uoga unaitwa Thanatophobia kwa kizungu. Unaweza ukagoogle uone wanasaikolojia wanavyoshauri jinsi ya kuuepuka huo uoga.

Lakini mkuu kuna vitu ni bora kuvikubali tu kwenye maisha. Kifo ni experience ambayo ni lazima kuipitia.

Binafsi kwenye kufa kama kufa huwa siogopi. Ila ambacho huwa kinaniogopesha ni maumivu nitakayoyapitia kabla ya kufa. Imagine ufe kifo cha kuungua na moto, I always feel it to be painful as a human being.
 
Hali hii ilinifika pia ,nilichofanya nikakubali kwamba kifo ni haki yetu! Yan nitakufa tu! Nikaanza kufuatilia documentaries mbalimbali kuhusu kifo !! Jinsi mortuary palivyo ! Watu wanavoandaliwa mpaka kwenda kuzikwa ! Kuna hadi watu wanafanya hadi make up kwenye miili iliyojeruhi vibaya ili iweze kuagwa! Ooh mpaka nikawa addicted kabisa. Hofu inaisha ,lakini uchungu wa kuondokewa na mpendwa wako ni kawaida.
 
Kwanza pole sana ,pili nikuambie tuu kuwa hii hali inatokea sana kadili unapokuwa mtu mzima kwa maana kuongezeka umri , sababu ni majukumu tulionayo na matamanio ya ndoto zetu ,sasa isikupe shida chakufanya iambie nafsi yako kwamba juzi nliogopa kufa na sikufa hali kadhalika jana pia sikufa na leo sifiii apo tuu , nasema hivi kwasabu mimi mwenyewe imenitokea hii kitu na ndio mbinu nlio tumia ,lakin jitaid kusali binafsi usitegemee sana kuombewa omba mwenyewe ivoo tuu mkuu.
 
Ahsante sana kwa ushauri.
Hofu ni mbaya sana aisee.
 
Soma Zaburi 34:4 na Mathayo 11:28

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Zaburi 34:4
"Nilimwomba Mwenyezi-Mungu naye akanijibu, na kuniondoa katika hofu zangu zote."
Mathayo 11:28
"Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha."
Shukrani sana mkuu kwa mstari hii, imenipa faraja. Nimeiandika kwenye notebook yangu, nitakua naipitia mara kwa mara.
 
Ukweli mchungu.
 
Natumaini na mimi hiyo hali itaisha pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…