Naitafuta muvi hii hata sijui inaitwaje

EvilSpirit

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2017
Posts
10,576
Reaction score
16,644
Muvi hii ni ya kiswahili niliiangalia muda mrefu sio bongo muvi ni zile muvi nadhani zinafadhiliwa na wahisani.nakumbuka sehemu chache sana kwenye hiyo muvi.kuna watoto wawili wa kike na wa kiume mama yao alikufa au aliachwa na baba yao,baba akawa akaoa mwanamke mwengine, yule mwanamke akawa anawatesa wale watoto mwishowe wakakimbilia mitaani.yule wa kike baadae alipata kazi ya uhausigeli kwa mama mmoja,lakini mume wa yule mama akawa anataka kumrubuni yule mtoto afanye nae mapenzi.

Mama yule mwenye huyo mume siku alimfuma mmewe akivutana na yule mtoto,yule mama akamfukuza yule mtoto,na mtoto akarudi mtaani,kuna sehemu yule mtoto anaonekana yuko na makahaba.Mwishoni mwa muvi kaka yake na huyu msichana alikamatwa na polisi kwa kujihusisha na uwizi dada yake akawa analia.Ni sehemu hii tu ndio nakumbuka.Katika muvie hii kuna wimbo wanaimba "maisha,maisha,maisha".sijui hii muvi inaitwa neria au?sina uhakika.
 
Watoto waliitwa tatu na juma[emoji23][emoji23][emoji23] TVT miaka ya 98 na 99. Wamefika mjini wameshuka kwenye train wakapita sehem jamaa anauza maji ya kandoro eti yule wakike akaomba jamaa kamtoa mbio
 
Hahahaaa,ingia you tube andika sarafina full movie
 
Kama nilishawahi kuiona ila na mie jina limepotea
 
Ata pia mi nimeshaiyona hii? Yule jamaa wa kiume alikuwa alibaki na wana kitaa wakawa wanapiga mishe za ukonda mwishowe wakamfundisha kuvuta bangi, yule mtoto wa kike alichukuliwa na mmama alikuja kuchukua samaki sokoni akaondoka nae,
 
Dah aisee ndio hiyo mkuu jina unalikumbuka
 
Ata pia mi nimeshaiyona hii? Yule jamaa wa kiume alikuwa alibaki na wana kitaa wakawa wanapiga mishe za ukonda mwishowe wakamfundisha kuvuta bangi, yule mtoto wa kike alichukuliwa na mmama alikuja kuchukua samaki sokoni akaondoka nae,
Ndio hiyo hiyo mkuu
 
Hiyo Movie nilishaiona Hao watoto Walitokea Morogoro... Mjomba wao au baba nadhani alipanda Abood bus from morogoro tu dsm kuwasaka Watoto akaenda ferry kuulizia waosha magari... Sikuhiyo nilichezea remote nikakutana nayo nikajisemea wacha niitizame... Walijitahidi kuigiza fresh tofauti na Movie za kijinga za Bongo Movie.. Mwishoni niliona ilidhaminiwa na Shirika furani either ya haki za Watoto au Danida or Something! Nenda Maktaba za TBC au Channel Ten hivi kama sikosei
 
Ndio hiyo hiyo,tatizo Jina lake ndio sikumbuki
 
Kijana alikuwa analala ndani ya pipa .toka mdogo hadi anakuwa mkubwa. Pia wakati wanatolewa kijijini waliwekewa alama kwenye mikono yao
 
Watoto waliitwa tatu na juma[emoji23][emoji23][emoji23] TVT miaka ya 98 na 99. Wamefika mjini wameshuka kwenye train wakapita sehem jamaa anauza maji ya kandoro eti yule wakike akaomba jamaa kamtoa mbio
Dah una kumbukumbu mpaka majina ya wale watoto unayakumbuka
 
Mkiipata hiyo nitafutieni na ile ya safari... kapili na mwenzie
 
Kijana alikuwa analala ndani ya pipa .toka mdogo hadi anakuwa mkubwa. Pia wakati wanatolewa kijijini waliwekewa alama kwenye mikono yao
Mkuu hapo umeongia chaka, hakuna kipande cha mtu kulala kwenye pipa mle,lakini sijui labda kipo maana nimeicheki kitambo mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…