EvilSpirit
JF-Expert Member
- Jun 15, 2017
- 10,576
- 16,644
Muvi hii ni ya kiswahili niliiangalia muda mrefu sio bongo muvi ni zile muvi nadhani zinafadhiliwa na wahisani.nakumbuka sehemu chache sana kwenye hiyo muvi.kuna watoto wawili wa kike na wa kiume mama yao alikufa au aliachwa na baba yao,baba akawa akaoa mwanamke mwengine, yule mwanamke akawa anawatesa wale watoto mwishowe wakakimbilia mitaani.yule wa kike baadae alipata kazi ya uhausigeli kwa mama mmoja,lakini mume wa yule mama akawa anataka kumrubuni yule mtoto afanye nae mapenzi.
Mama yule mwenye huyo mume siku alimfuma mmewe akivutana na yule mtoto,yule mama akamfukuza yule mtoto,na mtoto akarudi mtaani,kuna sehemu yule mtoto anaonekana yuko na makahaba.Mwishoni mwa muvi kaka yake na huyu msichana alikamatwa na polisi kwa kujihusisha na uwizi dada yake akawa analia.Ni sehemu hii tu ndio nakumbuka.Katika muvie hii kuna wimbo wanaimba "maisha,maisha,maisha".sijui hii muvi inaitwa neria au?sina uhakika.