Mkuu hata kama kuna uhaba wa kazi tujitahidi kuwa fair kwa watu tunaowaajiri, ni kweli utampata na atafanya kwa ajili ya shida ila kiubinadamu sio sawa.
Nikupe experience nina biashara kama yako pia ya restaurant na ninaifanya kwa masaa 24, wadada wanakuja kwa shift yule atakaekuja saa 1 asubuhi ikifika saa 12 jioni amemaliza kukusanya pesa anaondoka na ninamlipa 5000 kwa siku sawa na yule anayeingia usiku saa 1 akatoka saa 12 asubuhi.
Kuna mmoja akajiongeza anakuja asubuhi saa 1 ikifika saa 12 anapika chakula anaenda kuuza stendi mpaka saa 4 au usiku kiukweli nilikuwa nampa 7000 kila siku mpaka siku nyingine 10000. Nao wanapata moyo wa kufanya kazi na atakupa idea za kuendeleza biashara yako.
Sent using
Jamii Forums mobile app