Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 346
- 522
👉🏾Dar es Salaam, jiji lenye giza na mwanga, limejaa ndoto na fursa zisizoisha. Lakini ni ndoto gani zinazozungumzwa na watu wanaoshindwa kutimiza malengo yao? Jiji hili linapokuja kwenye mandhari ya kibiashara na utamaduni, linatoa picha ya maendeleo, lakini je, kila pembe ya mji inavyoonekana ni ya fahari kama ilivyo katika vichwa vya wengi?
👉🏾Tazama chini ya uso wa jiji hili lenye kasi ya maendeleo, na utaona changamoto zinazojificha msongamano wa magari, tatizo la makazi, mfumuko wa bei hasa ardhi, nk. Hata hivyo, kuna ndoto ya kulijenga jiji lenye nguvu na ustawi kwa kila mmoja, jiji ambalo linatoa fursa kwa mamilioni na kutoa matumaini kwa vizazi vijavyo. Je, jiji hili linaweza kuwa kioo cha mabadiliko?
Ndoto hii inahitaji ushirikiano wa kila mmoja wetu. Tuelekee kwenye mwelekeo mpya wa Dar es Salaam!"
Mwisho napenda kusema Ndoto nzuri hujengwa kwa hatua ndogo, lakini tamaa njema ni kama mbegu inayoota miti mikubwa, ikiwa tu itapandwa kwa bidii na matumaini.
Watu kutoka mikoani wanapokuja Dar es Salaam, wanapoiangalia wanajua ni kama Dubai, lakini wanakubaliana kuwa bado kuna kazi ya kuboresha ili iwe kama ndoto halisi.
~🥂
👉🏾Tazama chini ya uso wa jiji hili lenye kasi ya maendeleo, na utaona changamoto zinazojificha msongamano wa magari, tatizo la makazi, mfumuko wa bei hasa ardhi, nk. Hata hivyo, kuna ndoto ya kulijenga jiji lenye nguvu na ustawi kwa kila mmoja, jiji ambalo linatoa fursa kwa mamilioni na kutoa matumaini kwa vizazi vijavyo. Je, jiji hili linaweza kuwa kioo cha mabadiliko?
Ndoto hii inahitaji ushirikiano wa kila mmoja wetu. Tuelekee kwenye mwelekeo mpya wa Dar es Salaam!"
- Ingekuwa jambo la manufaa ikiwa jiji la Dar es Salaam lingepanuliwa kiutawala na wilaya kama Bagamoyo, Kibaha, na Mkuranga kuwa wilaya ndani ya jiji la Dar Es Salaam.Naamimi itakuwa suluhisho la kudumu la kupunguza msongamano na kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi ,kurasimisha makazi na ujenzi wa makazi bora kwenye viwanja vilivyopimwa !,Urasimu wa ardhi yamkini unaweza punguzwa na kuepuka ujenzi holela wa makazi.
- Ningependa kuona wilaya mpya kama Mbagala na Gongolamboto zikianzishwa ili kuendana na ongezeko la idadi ya watu. Naamini itarahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kama afya, elimu, ardhi, na umeme kwa wananchi, na hivyo kuboresha maisha yao kwa ujumla.
- Serikali imeonesha jitihada kubwa katika kupima ardhi na kurasimisha maeneo ya makazi, lakini bado naona ni muhimu kuweka sheria kali za kuzuia ujenzi katika maeneo yasiyopimwa. Vilevile, natamani iwe ni lazima kila mtu anayepanga kujenga apate kibali cha ujenzi kwanza. Pia Taasisi za serikali kama Tanesco (Umeme) na Dawasco (Maji) zisitoe huduma kwa watu wasio na vibali vya ujenzi na wale waliovunja sheria kwa kujenga katika maeneo kama hifadhi za barabara, mabondeni, na maeneo ya wazi. Naamini tutakuwa na jiji lililoboreshwa sana.
- Iwe ni lazima kwa kila mwananchi mwenye makazi yake kupanda miti ya matunda angalau mitano kwenye eneo lake, ili kusaidia kuboresha mazingira, kupambana na mabadiliko ya tabianchi, na kutoa lishe bora kwa familia.
- Ningependa kuona Wizara ya Ardhi ikipiga marufuku uuzwaji wa viwanja vyenye ukubwa chini ya square meter 400. Ingekuwa bora zaidi ikiwa uuzwaji wa viwanja utaanzia kwenye ukubwa wa square meter 500 (25x25), ili kuhakikisha maendeleo bora na miundombinu thabiti.
- Hongera kwa serikali kwa mafanikio makubwa katika kujenga miundombinu ya barabara za mwendokasi na vituo vya abiria. Hata hivyo, kuna uhaba wa mabasi, jambo linalozuia huduma bora. Ningependa kuona kuanzishwa kwa mfumo wa uendeshaji mseto wa mabasi, ambapo hisa kati ya mwekezaji na serikali zitachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma na kuongeza mapato.
- Bado wafanyabiashara wadogo, licha ya kupatiwa maeneo rasmi ya kufanya biashara, wanakimbilia maeneo yasiyo rasmi na kuanzisha biashara hasa jioni. Serikali inahitaji kufanya utafiti kuhusu maeneo haya wakimbiliayo hawa wafanyabiashara wadogo na kuanzisha biashara kuna nini?, kisha itafute namna na iwajengee masoko ya kisasa na kuwabidhi wafanyabiashara huku ikifuatilia utekelezaji wa taratibu na kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa kitovu cha biashara na mapato.
- Kuhakikisha usafi katika maeneo yetu, miundombinu bora ni lazima iboreshwe, na maafisa afya na kinga wapewe nguvu na usaidizi wa kutosha ili kuzuia uchafu na utiririshaji wa maji taka yasiyohitajika.
- Japokuwa tunatafuta maisha bora na vipato, bodaboda na bajaji zinapaswa kuzuiwa kupita kwenye barabara kuu zote. Badala yake, zifanye kazi katika maeneo maalum, na itakuwa kosa kwao kutumia barabara kuu. Tunapaswa kulinda taswira ya jiji hili; nilikumbuka nilipokuwa Singapore, niliposema natokea Dar es Salaam, waliniambia natokea kwenye 'big village'. Nilishangaa kidogo, kwani sehemu iliyokuwa ndoto yangu ilionekana kama kijiji kwa wengine. Basi, twahitaji kuboresha jiji hili liwe la kuvutia na kupendeza kwa kila mmoja.
- Tuwekeze kwenye teknolojia ya kisasa ili kuepuka mgao wa maji. Tunayo bahari ambayo tunapaswa kuitumia kuvuna maji ya baharini, kuyachuja na kuyatumia kwa mahitaji yetu ya kila siku. Chumvi itakayozalishwa itakuwa bidhaa ya kuuza ndani na nje ya nchi.
Mwisho napenda kusema Ndoto nzuri hujengwa kwa hatua ndogo, lakini tamaa njema ni kama mbegu inayoota miti mikubwa, ikiwa tu itapandwa kwa bidii na matumaini.
Watu kutoka mikoani wanapokuja Dar es Salaam, wanapoiangalia wanajua ni kama Dubai, lakini wanakubaliana kuwa bado kuna kazi ya kuboresha ili iwe kama ndoto halisi.
~🥂