Ama kweli unanipenda sana, ama kweli unaniwaza sana, ama kweli unanitafuta sana lakini unawaza mbona hunipati? Nimeamua kutoka mafichoni unapo nitafuta nikujie kwa maana kiu yako ni kubwa sana.
Baada ya kuona jitihada zako, leo nimependa nikueleze ukweli wote kwa maana unanipeda sana. Unapenda kutiwa moyo sana kuhusu mimi lakini naona haupewi ukweli wote kunihusu mimi.
Nipo hatua chache tu mbele yako lakini kwa mtazamo ulionao sidhani kama utanipata mimi labda uendelee kumpata ndugu yangu wa mbali aitwaye mshindwa hadi pale utakapo badilisha mtazamo wako.
Naona unavyojitia moyo kwa kiingereza kabisa ukisema kwamba ‘one day yes’. Hivi kwani mimi ukinibadilishia lugha ndipo utanipata? au ukiirembesha lafudhi yako ndipo nitaingia malangoni pako? Nipende kukuambia haka kakizungu hakatakusaidia kitu. Pepesa macho yako tazama wapendao kulitumia neno hili ndio wameendelea kuchakalika na kusota.
Nashangaa unavyosema eti kama ipo ipo tu, haka kamtazamo kameendelea kukujaza giza ndani yako lakini mbona hautaki kushtuka. Haka kamsemo hakana faida yeyote kwako kameendelea kuufanya ubongo wako uendelee kulala usingizi mzito usiamke kunitafuta. Ipo wapi? Ipo lini? Ipo kwa njia gani? Kwa nini usiutafakarishe ubongo wako ili uweze kunishawishi nikujie. Kwa sababu umeendelea kujifariji kwa misemo na maneno itaendelea kuwa asali moyoni mwako na miba mikononi mwako.
Upo kijiweni unapiga soga alafu una matumaini makubwa ya kwamba mimi ni halali yako. Napenda kukuambia utaisoma namba, ndio! tena zile za kirumi. Kinywa chako kimekuwa ni chanzo cha faraja yako lakini akili yako imekuwa ni chanzo cha umaskini wako. Nivumilie tu! Leo nimeamua nikueleze ukweli wote kunihusu mimi kwa maana unafki si mzuri. Funga mkanda wako kiume uendane na mimi kwa kuwa nipo hatua chache tu mbele yako nakusubiri.
Lakini wewe mbona ni mwepesi wa kulaumu na si kujilaumu, na tena mbona ni mwepesi wa kunung’unika na si kushukuru. Kila unaposhindwa unamtafuta mchawi ni nani, kwanini usitafute na mwisho wa siku utajiona ni wewe mwenyewe. Kwani ulivyonavyo si kufanikiwa huko-kujitoa na kufikia malengo si kufanikiwa huko? Je! hio nia na hio jitihada ulioifanya katika hicho kidogo ulichokipata ungeiweka kwenye hayo makubwa unayo yawaza usingenifikia? Laiti ungemaanisha kidogo tu katika hilo unalo liwaza, ningekuganda mikononi mwako kama sumaki iigandavyo chuma safi.
Siachi kusitika juu yako kwa jinsi ulivyo mpenzi wa filamu za kukuhamasisha na machapisho ya jinsi gani ufanikiwe. Nasikitika kwasababu muda wako mwingi umekuwa katika kusikiliza na kusoma kuliko kutenda. Laiti ungeifanyia kazi ile video uliosikiliza na kuiangalia mtandaoni usingekuwa hapo ulipo leo. Lakini ulichokifanya nikutafuta video nyingine ili uhamasike zaidi kimawazo na ushindwe zaidi kimatendo. Hebu jifunze kukifanyia kazi kikuhamasishacho alafu uone kama sitatimiza wajibu wangu wa kukukaribisha na kuwa rafiki yako.
Mwamshe aliyelala ukimuamsha wataamka na wengine. Wewe uliyeamka kuhusu mimi kwanini hauwaamshi wengine nao waamke kama wewe ukiogopa utapitwa na utalala pia. Je! kumwamsha yeye sikuiamsha jamii nzima? Kwa nini unaishikilia misemo ya mababu ambao hawakuwa na nia ya kwenda hatua nyingime ya juu zaidi. Kwani hazina njema si ile ya kujitoa kwaajili ya wengine? Kwa sababu wengi wamekithiri katika tabia hii leo nimejawa na wivu wa kuwaeleza watafutaji wote ya kwamba ukinipanda mimi utanivuna mimi. Nimechoka kukusubiria ninataka kukujia. Panda yafuatayo na we utanifurahia na zaidi utanisherekea.
Nitamani zaidi na onyesha nia zaidi
Ina maana hauutumii tena moja ya msemo wako pendwa uliokaririshwa shule ya msingi-Penye nia pana njia. Kunielezea tu moyoni mwako jinsi utakavyonipata bila ya kuonyesha nia ya dhati ni kama kuwafukuza inzi jalalani, kwa maana hautaweza. Natambua na naona unavyojifurahisha kwa mawazo mazuriii ya namna utayapata matunda yangu. Naona unavyo nong’ona moyoni ya kwamba nitafanya hivi na hivi na sijui kwanini unafurahi kwelikweli. Sisikitiki kukuambia kwamba jirani yangu anipingaye anayeitwa kushindwa anakunyemelea usipoonyesha nia madhubuti ya kuyafanya hayo unayo yafikiri kwa shauku kubwa hadi kukunyima usingizi.
Thubutu
Kwanini unasita? Kwanini unaogopa? Kwanini unahofu? Ule ujasiri uliokuwa nao ulipo kuwa mtoto mdogo umekwenda wapi? Nikutie moyo wa kweli na si wa kinafki-anza sasa na matunda yangu utayaona, anza tu na matokeo utayaona. Uoga umekuwa ndio chanzo kikuu cha wewe kuwa ulivyo jinsi ulivyo leo, kwani kwasababu ameshindwa yeye nawe utashindwa pia? kwani njia alizozitumia yeye ndizo njia utakazozitumia?. Lahasha! Yeye ni yeye na wewe ni wewe kuwa wewe usiwe yeye. Nakuambia thubutu sasa na matunda yangu utayaona.Baada ya kuona jitihada zako, leo nimependa nikueleze ukweli wote kwa maana unanipeda sana. Unapenda kutiwa moyo sana kuhusu mimi lakini naona haupewi ukweli wote kunihusu mimi.
Nipo hatua chache tu mbele yako lakini kwa mtazamo ulionao sidhani kama utanipata mimi labda uendelee kumpata ndugu yangu wa mbali aitwaye mshindwa hadi pale utakapo badilisha mtazamo wako.
Naona unavyojitia moyo kwa kiingereza kabisa ukisema kwamba ‘one day yes’. Hivi kwani mimi ukinibadilishia lugha ndipo utanipata? au ukiirembesha lafudhi yako ndipo nitaingia malangoni pako? Nipende kukuambia haka kakizungu hakatakusaidia kitu. Pepesa macho yako tazama wapendao kulitumia neno hili ndio wameendelea kuchakalika na kusota.
Nashangaa unavyosema eti kama ipo ipo tu, haka kamtazamo kameendelea kukujaza giza ndani yako lakini mbona hautaki kushtuka. Haka kamsemo hakana faida yeyote kwako kameendelea kuufanya ubongo wako uendelee kulala usingizi mzito usiamke kunitafuta. Ipo wapi? Ipo lini? Ipo kwa njia gani? Kwa nini usiutafakarishe ubongo wako ili uweze kunishawishi nikujie. Kwa sababu umeendelea kujifariji kwa misemo na maneno itaendelea kuwa asali moyoni mwako na miba mikononi mwako.
Upo kijiweni unapiga soga alafu una matumaini makubwa ya kwamba mimi ni halali yako. Napenda kukuambia utaisoma namba, ndio! tena zile za kirumi. Kinywa chako kimekuwa ni chanzo cha faraja yako lakini akili yako imekuwa ni chanzo cha umaskini wako. Nivumilie tu! Leo nimeamua nikueleze ukweli wote kunihusu mimi kwa maana unafki si mzuri. Funga mkanda wako kiume uendane na mimi kwa kuwa nipo hatua chache tu mbele yako nakusubiri.
Lakini wewe mbona ni mwepesi wa kulaumu na si kujilaumu, na tena mbona ni mwepesi wa kunung’unika na si kushukuru. Kila unaposhindwa unamtafuta mchawi ni nani, kwanini usitafute na mwisho wa siku utajiona ni wewe mwenyewe. Kwani ulivyonavyo si kufanikiwa huko-kujitoa na kufikia malengo si kufanikiwa huko? Je! hio nia na hio jitihada ulioifanya katika hicho kidogo ulichokipata ungeiweka kwenye hayo makubwa unayo yawaza usingenifikia? Laiti ungemaanisha kidogo tu katika hilo unalo liwaza, ningekuganda mikononi mwako kama sumaki iigandavyo chuma safi.
Siachi kusitika juu yako kwa jinsi ulivyo mpenzi wa filamu za kukuhamasisha na machapisho ya jinsi gani ufanikiwe. Nasikitika kwasababu muda wako mwingi umekuwa katika kusikiliza na kusoma kuliko kutenda. Laiti ungeifanyia kazi ile video uliosikiliza na kuiangalia mtandaoni usingekuwa hapo ulipo leo. Lakini ulichokifanya nikutafuta video nyingine ili uhamasike zaidi kimawazo na ushindwe zaidi kimatendo. Hebu jifunze kukifanyia kazi kikuhamasishacho alafu uone kama sitatimiza wajibu wangu wa kukukaribisha na kuwa rafiki yako.
Mwamshe aliyelala ukimuamsha wataamka na wengine. Wewe uliyeamka kuhusu mimi kwanini hauwaamshi wengine nao waamke kama wewe ukiogopa utapitwa na utalala pia. Je! kumwamsha yeye sikuiamsha jamii nzima? Kwa nini unaishikilia misemo ya mababu ambao hawakuwa na nia ya kwenda hatua nyingime ya juu zaidi. Kwani hazina njema si ile ya kujitoa kwaajili ya wengine? Kwa sababu wengi wamekithiri katika tabia hii leo nimejawa na wivu wa kuwaeleza watafutaji wote ya kwamba ukinipanda mimi utanivuna mimi. Nimechoka kukusubiria ninataka kukujia. Panda yafuatayo na we utanifurahia na zaidi utanisherekea.
Nitamani zaidi na onyesha nia zaidi
Ina maana hauutumii tena moja ya msemo wako pendwa uliokaririshwa shule ya msingi-Penye nia pana njia. Kunielezea tu moyoni mwako jinsi utakavyonipata bila ya kuonyesha nia ya dhati ni kama kuwafukuza inzi jalalani, kwa maana hautaweza. Natambua na naona unavyojifurahisha kwa mawazo mazuriii ya namna utayapata matunda yangu. Naona unavyo nong’ona moyoni ya kwamba nitafanya hivi na hivi na sijui kwanini unafurahi kwelikweli. Sisikitiki kukuambia kwamba jirani yangu anipingaye anayeitwa kushindwa anakunyemelea usipoonyesha nia madhubuti ya kuyafanya hayo unayo yafikiri kwa shauku kubwa hadi kukunyima usingizi.
Thubutu
Ning’ang’anie nami sitakuaibisha
Achana na kusuasua, njia yangu sio nyepesi kama unavyoifikiria. Mipango uliyoianza leo usiifanye tamati kesho, mikakati uliyoanza nayo leo dumu nayo kesho. Njia yangu inahitaji kujitoa na kuvumilia. Je! mbivu aliyoambiwa ataila mvumilivu si mimi? na je! kibaba alichoambiwa atakijaza mwenye haba akiendelea kuweka haba si mimi? Basi mtu mwerevu na anielewe kwa maana nipo njiani ninakujia! Usikubali kukatishwa tamaa ng’ang’ana mpaka mwisho nami sitakawia.
Imani yako ndio ushindi wako
Utafanikiwaje kama hauamini kufanikiwa? Utawezaje kama hauamini kuweza? Nikuambie tu Imani yako ndio njia yangu niitumiayo kukufikia. Yapo mambo matatu napenda kukujuza; ukiniamini kidogo nitakuja kidogo, ukiniamini sana nitakuja sana, na vivyo hivyo usiponiamini kabisa itabaki kuwa nadharia. Jifunze kuwa na Imani kubwa ili ufanye mambo makubwa katika maisha yako na kwa jamii yako. Jua katika safari ya kunipata mimi kuna kuanguka na pia kuna kusimama. Uwe na moyo mkuu ukianguka simama tena kwa maana nipo hatua chache tu mbele yako nakusubiria.
Nisiwachoshe kwa maneno mengi kwa maana hata mimi sipendi muwe nayo sana ili niweze kuwakaribishe kwenye hazina yangu njema. Enyi watafutaji achaneni na maneno mengi kwa kuwa hii ni ishara ya mashaka mengi, bali jifunzeni kuwa na maneno machache na matendo mengi. Nawaandikia enyi vijana, kwanini mnaiga maisha ya wengine? Nawaeleza enyi wamama, kwanini mnasita kutenda? Nanyi wababa, kwanini hamuitutumui tena misuli yenu ya imani? Basi niwasihi itendeni mipango yenu kwa Imani kubwa nami nitawajalia kwa viwango vikubwa!
Upvote
4