Najaribu fani ya uchekeshaji ila watu hawacheki kwanini?

Nimekuwa nikiamini najua kuchekesha sana ila watu wananikataa.
Juzi nimeenda Coco beach na nikakusanya watu ili kuwachekesha ila hawakucheka.

Haiwezekani mimi nawachekesha watu ila wao hawacheki. Ni dharau?

Unadhani hao watu wana shida gani? Na nitawasaidiaje waelewe?
Jitie dole, wallah vile watacheka
 
Nimekuwa nikiamini najua kuchekesha sana ila watu wananikataa.
Juzi nimeenda Coco beach na nikakusanya watu ili kuwachekesha ila hawakucheka.

Haiwezekani mimi nawachekesha watu ila wao hawacheki. Ni dharau?

Unadhani hao watu wana shida gani? Na nitawasaidiaje waelewe?
kuchekesha ni aina ya sanaa

sanaa ni aina ya ufundi, na ufundi, mtu anajifunza ama anaufanyia mazoezi ama kuutafutia uzoefu ili kuwa mtaalamu mbobezi wa ufundi husika

mtu anaweza kuwa na kipaji cha sanaa fulani ila akawa sio fundi wa sanaa hiyo

ndio maana kwa mfano msanii kama Diamond, alikuwa na kipaji cha kuimba ila alipoanza kutoka alikuwa na uzoefu mdogo, ufundi wake ulikuwa mdogo ila ufundi wake sasa umekuwa mkubwa kwasababu ya uzoefu na kujifunza

inawezekana una kipaji cha sanaa ya kuchekesha ila ukakosa ufundi wa sanaa hiyo

sasa ili uupate huo ufunde kaa chini na ujifunze magwiji wa tasnia hiyo wanafanyaje sanaa yao

sanaa ikiwemo uchekeshaji sio kitu rahisi, ama ujingaujinga, ni ufundi, ndio maana si kila mtu anaweza
 
Kuchekesha bila ya KUWA na nianya kuchekesha ndio unafanya kazi KWA urahisi kuliko KWA kukusudia.
 
Nimekuwa nikiamini najua kuchekesha sana ila watu wananikataa.
Juzi nimeenda Coco beach na nikakusanya watu ili kuwachekesha ila hawakucheka.

Haiwezekani mimi nawachekesha watu ila wao hawacheki. Ni dharau?

Unadhani hao watu wana shida gani? Na nitawasaidiaje waelewe?
Hahahaaaaa katika pilikapilika za maisha nilijikuta najiingiza kwenye sanaa ya uchekeshaji.

Kuna siku nikaenda pale peacock Hotel (kkoo) kulikua na show, ilipoisha nikamfuata mshkaji mmoja kati ya wale waliopafomu nikamuelekeza kwamba ninakipaji cha kuchekeza anishike mkono .

Mshkaji mpaka leo ni staa mkubwa tu wa comedy(akisoma hapa atakumbuka) jamaa hakuna na noma, tukabadilisha contact kisha akanipa mwaliko show inayofuata masaki.

Siku ilipofika saa moja tu jioni nimeshafika, tukaonana na jamaa akanipa ratiba, jina langu lipo kwenye list wachekeshaji.

Muda ulipofika nikapanda jukwaani, kutazama nyomi sio poa, hapo hapo nikaingiza baridi, piga joke ya kwanza holllllaaaawatu wamenuna, piga joke ya pili watu kimya ,piga jokes mfululizo watu bado wamenuna(halafu pale mbele vip zimekaa pisi kalikali na washua kama wote)

Mpaka Mc anakuja kunishusha sikufanikiwa kuchekesha hata sisimizi 😄 🤣 😂 , nikashuka jukwaani noma kichizi.

Kurudi backstage wale wachekeshaji wenzangu wooote hawana mbavu wananicheka, atleast nikapata moyo nimewachekesha hata wao
 
yani kwa maelezo yako tu hapa, haujawahi kufanya mazoezi, hauna uzoefu wa kuchekesha watu jukwaani, yani hauna mbinu, utindu wala ufundi wowote, hata kama ukiwa na kipaji bado unahitaji mazoezi n uzoefu, ingekuwa rahisi wauza machungwa wote, makondakta wote wangjiingiza kwenye uchekeshaji, ila sio rahisi
 
Back
Top Bottom