Najaribu kuwaza Jakaya Kikwete aliwezaje kuajiri Walimu na Madaktari wote katika kipindi chake wakati Hayati Magufuli hata mwaka mmoja alishindwa

Upewe kazi afu uje kulalamika kikokotoo? Private sector Kuna mafao?

Hela zenyewe ni za Serikali
 
Mimi ni mwalimu ambaye niliajiriwa kipindi Cha kikwete lakini najuta kuajiriwa kipindi hicho maana kulikuwa na mfumuko wa bei kiasi kwamba mshahara wote uliishia kwenye mahitaji.mshahara ulikuwa mdogo sana yaani ilikuwa hakuna tofauti na jobless angalau kipindi Cha Magufuli mfumuko wa bei ulitulia na sisi walimu tukawa tunatembea vifua mbele maana mshahara ulitosha Kwa mahitani yetu.
 
Unaropoka Kwa vile umepata kazi.
 
Kipimo cha Watanzania wengi hawana akili ndio hichi..mtoa mada hajui uanzishwaji wa shule za kata ilihitaji walimu wengi,mtoa mada hajui huanzishwaji wa vituo vingi vya afya na mahospitali vilihitaji watumishi wengi wa kada hiyo..Baada ya watumishi kujitosheleza unaaanza kuajiri tokana na uhitaji....
 
Miradi inakula Sana hela

Kama umewahi kujenga nyumba utaelewa kuwa ujenzi unatumia gharama kubwa Sana

Sasa jpm alizidiwa imbalance ikatokea.
Mwananchi wa kawaida haelewi kuwa ile miradi mikubwa kama JNHPP, SGR, Madaraja yanakula fedha nyingi sana ambazo huwa hatuna uwezo wa kuzipata. Walikuwa wakiambiwa fedha zetu za ndani na wao wanashangiria, sasa hapa ndiyo tumepatikana sote kwa pamoja.
 
Jambo lepesi kama hili si ungemuuliza tu shemeji hapo nyumbani akakupa majibu kama akili yako imeshindwa kukujibu.
 
Mtu alikaa miaka 10 na mwingine 5 kashajifia zake na bado wakipambanishwa hata na mtoto wa primary bado mwendazake atamfunika tu,
 
JPM alikuwa na roho mbaya, pia alipeleka hela zote mahali alipokuwa anapata teni pasenti, mfano SGR na mengine kama bwawa la umeme.

JK aliona kuliko ajenge reli mpya wakati ya zamani ipo, akaamua aajiri, aliona kuliko nchi ikope kupata byanzo vya umeme, akatafuta wazungu na hela zao wakaja kuwekeza kwenye umeme wa gesi, bila nchi kutoa hata mia, stiglers tumekopa trilions, kwa hiyo madeni tele.

Alijenga daraja la kigongo busisi ili awakoge ukweni, kwa karibu trilioni
 
Kipi kizuri kwako, ufe ili upate maendeleo ukiwa hujulikani ulipo au uapate neema na uhakika wa kula halafu uinjoy marndeleo. By the way maendeleo ni kuwa na uhakika wa kuishi na kula kwa kupata kipato. Hilo jk alilijua vyema.
Kikubwa nchi ikae kwenye mstari,,,kuna haja gani kuachiwa kupata hio buku 10 wakati ukiminywa haki zako kuna mtu anatoa elfu 50 anakukandamiza,,,hapo bora wote tupate 0 hata likitokea jambo la kutumia haki wote mnamsikiliza pilato badala ya mwenye noti nyingi kupenyeza kitu....huo ni mfano mmoja tu..........JK kakuachia upate huyo swala ila wenzio wanabeba nyati na wala nyati wanakuja kuwanyanasa hao wala swala bora tuwe na njaa wote tuanze moja
 
Maza ameajiri ni nini sasa? Magu aliua sekta binafsi
 
Ni hivi. Kwa sababu ya ubovu wa CCM, kila uchao ni afadhali ya jana yake. Aliajiri (japo siyo wote kama unavyosema) kwa sababu tulikuwa hatujafikia saturation point ya sasa hivi. Kadiri siku zinavyoenda ndivyo ajira zitazidi kuwa ngumu. Je unakumbuka zile bajaji na boda boda za mwanzo mwanzo? Zilikuwa zinapata wateja wengi. Sasa hivi je? Wateja wamepungua kwa sababu zimekuwa nyingi, na hii hali inaendelea kuwa mbaya kila siku. Kwa hiyo tatizo ni CCM kutokuwa na planning. Nchi inatakiwa ijue miaka 10, 20, 30 ijayo kutakuwa na population kiasi gani, zitahitajika hospital ngapi na madaktari wangapi angalau kwa makadirio. Huwezi kukurupuka na kuanzisha vyuo feki vya udaktari na ukasalimika. Wahitamu ni lazima watakosa ajira na hata wakitaka kutoka nje ya nchi hawatakuwa na soko kwa sababu ni vilaza.
 
JMK
JPM


Mkuu huoni kama kunatofuti hapo.

Mzee wa kutabasamu ni MASTER
 
Maza ameajiri ni nini sasa? Magu aliua sekta binafsi
Hawa watu hawajui kuwa kadiri siku zinavyokwenda ndiyo nchi inavyozidi kuwa ngumu. Watu hawajui kuwa hata wanaopiga kelele sasa hivi wanaitakia nchi salama siku zijazo. CCM haina tena ujanja sasa hivi imebaki ku-hang up kama timu inayojihami dakika za mwisho isifungwe goli. Tatizo ni kuwa huu ''mpira'' wa CCM vs wananchi hauishi. Siku nchi itakapolipuka kwa fujo za watu kuchoka na maisha magumu kila mtu ataathirika na kujuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…