Najiandaa kuondoka nyumbani, nimeamua kwenda kupanga. Je, kuna ushauri?

Najiandaa kuondoka nyumbani, nimeamua kwenda kupanga. Je, kuna ushauri?

Hayo ndio madhara ya kutoka familia za kishua,miaka 32 upo kwa wazaz halafu umeoa pia (tuna assume upo na mkeo kwenu),okey sio kesi kapange akili ikomae hapo lazima uapply kila aina ya calculations za BAM & PURE
 
habari wadau

Mimi ni kijana wa umri miaka 32, naishi DAR miaka yote hiyo nipo kwa wazazi na nimeoa ila bado sijazaa ndoa yangu bado changa ila natumai soon nitaitwa faza kabla stori haijawa ndefu niseme tu wiki hii nimekuwa na mawazo ya kuhama home hiovyo natarajia miezi 3 mbele niende kupanga japo fedha inanipiga chenga lakini nafsi inaniambia mafanikio yapo ukihama hivyo najitutumua wadau nianza kufanya maendeleo before 40.

Napokea ushauri.
Lengo la kwenda kupanga ni nini?

Hapo nyumbani kuna kero labda toka kwa ndugu ama wazazi wako unazipata?

Kwa nini malengo ya kujitegemea usiyakamilishe ukiwa hapo nyumbani?

Changamoto za kuishi 'mapangoni' unazielewa?

Maana ninavyoelewa na namna ulivyojitambua namna hii, malengo yako utayapeleka vizuri sana bila stress ukiwa unaishi hapo nyumbani, kuliko utavyoyapeleka ukiwa ghetoni.

Ama unafuata mikumbo inayosema mtoto wa kiume akizidi miaka 18 hautakiwi kuendelea kuishi home, au unapenda tu kwenda kufanya tafiti za changamoto za maghetoni?

Siioni faida kuliko hasara.
 
Acha kuingia gharama zisizo na msingi wewe! Mimi nakushauri ubaki hapo hapo kwa wazazi wako. Siku ikitokea tu Mwenyezi Mungu kawapenda zaidi; hiyo nyumba inakuwa mali yako.
Mwanzo umeshauri vizuri, lakini mwisho umevurunda mkuu.

Kwani kifo kina haki miliki ya umri?

Je akitangulia yeye kudanja, ataacha nini kwa mke na kakijacho kake?

Kundelea kuishi hapo nyumbani kuwe kwa faida ya kujijenga kiuchumi bila stress na kusiwe na nia ovu ya tamaa ya fisi kumfuata nyati hai akitegemea atadondoka muda wowote ili amle.
 
Lengo la kwenda kupanga ni nini?

Hapo nyumbani kuna kero labda toka kwa ndugu ama wazazi wako unazipata?

Kwa nini malengo ya kujitegemea usiyakamilishe ukiwa hapo nyumbani?

Changamoto za kuishi 'mapangoni' unazielewa?

Maana ninavyoelewa na namna ulivyojitambua namna hii, malengo yako utayapeleka vizuri sana bila stress ukiwa unaishi hapo nyumbani, kuliko utavyoyapeleka ukiwa ghetoni.

Ama unafuata mikumbo inayosema mtoto wa kiume akizidi miaka 18 hautakiwi kuendelea kuishi home, au unapenda tu kwenda kufanya tafiti za changamoto za maghetoni?

Siioni faida kuliko hasara.
ni dhamira yng toka nilvokuw na age ya 18
 
Me ntakuwa ka muarabu au mubindi kutoka nyumban no wazazi wataniachia hii nyumba kikubwa uwe na hela ya maisha tu nyumba sio ishu na mjin kikubwa uwe na pakulala tu me home sitok
Kwenu hapo nyumbani, wewe ni mtoto wa kipekee kwa wazazi wako, yaani umezaliwa peke yako?
 
ni dhamira yng toka nilvokuw na age ya 18
Takribiani nusu ya age hiyo ya miaka32, kwanini umeimaliza ukiwa unawaza jambo moja bila ya kufikia muafaka?

Mi nionavyo, fanya mambo yako yakamilike kwanza ukiwa hapo nyumbani na siku unaondoka hapo ni safari ya kwenda kwako ulikojenga.

Fanya hima ukamilishe makazi yako, maana kupanga ni kwenda kwenye makazi kwa njia ya kulipia, hapo gharama zitaongezeka na kasi ya maendeleo kushuka.

Ila kama hauna malengo wala mpango wa kujenga makazi yako kwa sasa, hama hapo nyumbani fasta kapange mkuu, mana unamnyima mkeo uhuru wa kupika na kupakua na kula akitakacho hadi apate maelekezo 'kutoka juu'!

Na wewe utabakia na maisha ya kuexpose mambo yako na mkeo kwa wazazi ama nduguzo hadi lini?

Ukiisha kuoa, nyumbani kwenu ishi kwa malengo hasa ya kujitegemea.

Mke anahitaji faragha na uhuru wa mambo yake hasa akiwa kwake?
 
Mkuu acha papara ya maisha,ugali wa home mtamu fanya hivi subiria Hadi mwanao akianza kujitegemea ndio nawe unatoka
 
Back
Top Bottom