Najichukia kwa hili tatizo langu la ngozi, nimekosa mwenza

weka picha tuone hiyo ngozi jinsi ilivyo tukupatie njia ya kutibu tatzo
 
Hapana sijazaliwa nayo
Dada hebu jibu vizuri hilo swali kwa kirefu, usijibu kwa kuchokachoka;
Specifically hilo tatizo la kubaki na kovu ukijikuna lilianza lini (miaka mingapi iliyopita?)
Kuna logic ktk swali hilo, kwamba km lilianzia ukubwani je ilikuwa ni ktk wakati ambao style yako ya maisha ulikuwa umeibadilisha? (km kuanza matumizi ya vipodozi tofautitofauti) n.k
 

Shida inakuja kwa cc binadamu tatizo la kiroho tunatibu kimwili na la kimwili tunatibu kiroho, nenda hospt kwa mabingwa wa magonjwa ya ngozi baada ya hapo fuata hatua nyingine japo kuokoka sio vibaya kama hujaokoka lakini tunalenga tatizo sio kuzunguka tatizo.
 
Mungu anaweza kuponya magonjwa. Mimi mwenywe niliponywa magonjwa mazito sana, pia nimeokoka. Hospitali zilishindwa lakini nilipomwamini Mungu aliniponya. Dada (mwenye ugonjwa) ukiwa na akili nzuri utagundua kwamba ushauri wangu haulengi kukupoteza kama mtu mwingine asiyemwelewa anavyoona.
 
Sijachunguza vizuri kuanzia lini ila miaka 3 nyuma nilianza kunotice na sasa imekua severe,kuna sehem nilijikwaruza kidogo tu miaka 3 nyuma hadi leo huo mstari upo.
Halafu maisha yangu yote napaka vaseline
 
Kuokoka ni muhimu lakini ni uchanga wa kiroho,udini na upotoshaji kusema waliookoka wanapatikana kwenye baadhi ya madhehebu machache kama hayo uliyoyataja,Mungu hana mipaka ya kidhehebu pole.
 
Nenda kapime hosptal
Tatizo lako hujikubali kama ulivo ndo mana unajichukia jipende kwanza hata kama ukoje, afu ndo utapata wa kukupenda
 
Kuokoka ni muhimu lakini ni uchanga wa kiroho,udini na upotoshaji kusema waliookoka wanapatikana kwenye baadhi ya madhehebu machache kama hayo uliyoyataja,Mungu hana mipaka ya kidhehebu pole.
Nimetumia neno "kama" (like) si "only" kipindi nikielezea makanisa hayo. Ungekuwa mpagani isingekusumbua lakini ukiwa na dini, lazima udini ukutese
 
Wewe ni Professor wa nini ... ?!

Lakini wewe pia ni "mdini" ..., extremist ... !

Mungu hapewi masharti na wanadamu wala wakristo , au walokoke kuwa hamponyi MTU wake mpaka eti AOKOKE au akasali huko ulikotaja ... !

"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" ...
 
Siwezi kumfundisha kipofu kuchora.
 
Pole Sana Dada yangu... natumai utapata ufumbuzi wa tatizo lako

Mungu wetu ni mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…