Najichukia kwa hili tatizo langu la ngozi, nimekosa mwenza

Najichukia kwa hili tatizo langu la ngozi, nimekosa mwenza

Wokovu siyo dini mbona unamshauri aende TAG au EAGT, unajua anakosali leo? mbona hujamshauri aende kwa mch lusekelo? maana na yeye ameokoka na anahubiri wokovu, na kuponya watu kwa maombezi, ni kweli yesu anaponya akimukiri na kujitenga na uovu na kumtegemea yeye kwa kila jambo atapata faraja na huo uponyaji anaoutaka, yesu ni mwema.
Sikuja kuhubiri dini au dhehebu bali kumsaidia huyu dada. Ningepende kusikia maoni yake kuliko maoni ya mtu yeyote asiyehusika
 
Dada hilo ni tatizo dogo sana kwa MUNGU WA ELIYA (1 Falme 18:21-40), sasa ili upone hakikisha kila unapotoka kuoga jipake mafuta ya mzeituni siku zote na utaiona ngozi yako ikipona na kuwa nzuri kipita hata mwanzo au ulivyozaliwa.
Hayo mafuta usichanganye na kitu chochote.( Kutoka 30:26-31).
Kama una swali karibu!
Hayo mafuta yanapatikana wapi ndugu?
 
Utakua na alegy na kitu na bado hujajua ni kitu gani, ni mbaya sana hio. jaribu kwenda kwa madaktari wa ngozi watakusaidia tatizo lako
 
Utakua na alegy na kitu na bado hujajua ni kitu gani, ni mbaya sana hio. jaribu kwenda kwa madaktari wa ngozi watakusaidia tatizo lako
sawa asante...ila mara nyingi hua wanasema ni vigumu kujua ni allergy ya nini
 
Hayo mafuta yanapatikana wapi ndugu?

Mafuta ya mizeituni (olive oil) yanapatikana kwenye maduka ya dawa na maduka ambayo yapo karibu na makanisa, kariakoo . Na maeneo mengi tu yanapatikana kwa bei nzuri tu kwa ujazo wa aina tofauti.
 
Mafuta ya mizeituni (olive oil) yanapatikana kwenye maduka ya dawa na maduka ambayo yapo karibu na makanisa, kariakoo . Na maeneo mengi tu yanapatikana kwa bei nzuri tu kwa ujazo wa aina tofauti.
nilisha wahi sikia nitayatafuta
 
Umenikumbusha hadith ya Chaupele na ile ya Cinderella.

Chaupele kumbe ile ngozi alikuwa anaivaa tu na akiivua usiku hung'ara kama almasi... Mdada tafuta dawa ni kweli Wanaume wakiona Mdada ana tatizo fulani kubwa husepa fasta ila Jaribu kula vyakula vyenye virutubisho vingi pia pima kama una areji vya vitu kadhaa mwilini mwako haswa Nyama zote jiepushe nazo kula uone kama pesa ya vipimo huna
 
Njia nyingine ya uhakika kwa wenye uhakika.

Amua kuokoka kweli kutoka moyoni, nenda kwenye kanisa la watu waliookoka KWELIKWELI kama T.A.G au E.A.G.T kisha wambie watumishi UNATAKA KUOKOKA, kisha watakuongoza kupokea wokovu.

NB: Si kila tatizo linaweza kutibiwa kwa dawa. Mengine yanasababishwa na nguvu za giza hivyo JINA LA YESU PEKEE LINAWEZA KUKUOKOA.

Kama kweli umeamua kuokoka kutoka moyoni, wambie wakuombee tatizo lako la ngozi, watakuombea utapona kama una imani kwamba Mungu anaweza pia kama umemaaishisha kumfata Mungu/kudumu katika wokovu mpaka mwisho wa maisha yako.

NB: Usiende kuokoka kama unakwenda kujaribu utapona au la! Bali nenda kaokoke kwa kumfata Mungu bila kujali kama atakuponya au hatakuponya. Kwani Wokovu utakupeleka mbinguni. Pia Ukiokoka Mungu anaweza kukuponya magonjwa na matatizo yako yote.

Wokovu si dini, bali ni mabadiliko ya NAFSI yanayofanywa na Mungu kwa yeyote anayempokea Bwana Yesu ili amuokoe na dhambi na jehanamu ya moto.
Masada BUTU alikuambia hajaokoka au anataka Tiba Imani Za MZEE WA upako A. K. A bapa ni shida
 
Mamboz,jamani kama mnakumbuka nilikua natafuta mchumba na hali yangu niliyonayo,wengi walijitokeza wakidhani natania labda,walihisi mimi ni mzuri sana ila natania.

Kusema ukweli nipo kama nilivyosema,na nimerudi tena kuomba msaada kwa anaejua dawa ya makovu tafadhali,sio ya ajali yani yanatokea tu hata nikijikuna kovu linabaki,pia nikiumwa na mdudu lazima kovu libaki,nikijikwaruza kidogo bas kovu hilo.

Wanaume pia hawaniangalii hata mara mbili,niko mpweke,sina hata mwenza.

Nachukia sana ngozi yangu na sijui shida ni nini,naomba tafadhali kwa anaejua dawa ambayo itanifaa...

Wanawake wenzangu nisaidieni,kina baba,kina kaka naombeni mnitajie dawa itakayoondoa makovu haya jamani.

Bio oil nimejaribu haifanyi kazi,aloevera hua napaka sioni matokei,limao pia hakuna kitu.

Najisikia vibaya sana,mda mwingine hua nikijiangalia nalia tu,why me?
Msaada wenu ndugu zangu tafadhali.
Weka picha ili tuamini, tusijue unatania.
 
Back
Top Bottom