Najishangaa kwanini ninakuwa na hii roho ya huruma kiasi hiki. Najiona mjinga asee

Ngumu sana mkuu, kuna wakati namsaidia mtu wakati unakuta balansi niliyobaki nayo si nyingi sana, ila unakuta mtu ana shida seriuous kabisa.
we kaza tu usijieleze sana sema mambo yamekaa vibaya labda next time na next tine hivo hivo [emoji23]
 
Kuazima kupo Cha Muhimu unaangalia mtu na mtu Kuna watu waaminifu na waelewa sio Kila mtu Wa kumuazima
 
Kuna jamaa Juzi nilimnyima, nitaendelea kumnyima. Haweki mafuta yeye ni kusema ahsante na sio kwamba hana uwezo wa kuweka mafuta au kununua usafiri wake. Aah hapana, kuwa Fala ineishia 2023.
 
Eeeh kuna hao watu asee, Nimejitamkia ufala na ujinga wangu unaishia 2023. Mwaka huu ni aheri nionekane mchoyo ila siazimishi.
 
Jifunze kusema hapana bila kutoa sababu. Huo sio usafiri wa umma. Na Kama una mpa mtu Basi ni Yule wandani kabisa mnae heshimiana kwa sbb anakueshimu na Mali yako ataieshimu.
Nimepokea kiongozi, ninaahidi kufanyia kazi
 
Binafsi, hii kitu inanisunbua sana kwenye harakati hizi za maisha na ukijumlisha na mambo ya kidini haya. Unajikuta unasaidia ila wewe unaumia kwa Bill za matengenezo na mafuta wakati huo uliyemsaidia hata kusema aone sababu ya kukusaidia ili siku nyingine pia aweze kuazima hawafanyi. Ila nimejisemea moyo, ujinga na ufala umeishia 2023.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…