Najishangaa kwanini ninakuwa na hii roho ya huruma kiasi hiki. Najiona mjinga asee

Najishangaa kwanini ninakuwa na hii roho ya huruma kiasi hiki. Najiona mjinga asee

Ngumu sana mkuu, kuna wakati namsaidia mtu wakati unakuta balansi niliyobaki nayo si nyingi sana, ila unakuta mtu ana shida seriuous kabisa.
we kaza tu usijieleze sana sema mambo yamekaa vibaya labda next time na next tine hivo hivo [emoji23]
 
Kuazima kupo Cha Muhimu unaangalia mtu na mtu Kuna watu waaminifu na waelewa sio Kila mtu Wa kumuazima
 
Kuna jamaa Juzi nilimnyima, nitaendelea kumnyima. Haweki mafuta yeye ni kusema ahsante na sio kwamba hana uwezo wa kuweka mafuta au kununua usafiri wake. Aah hapana, kuwa Fala ineishia 2023.
Ndo ivo mkuu tufanyaje sasa,,,ila kuna watu ukiwasaidia huwa haiumi ni watu ukiwasaidia unajisikia proud ya moyo wako ila kuna watu wanakuwa vichomi sana,,,,mimi niko hivi kumsaidia mtu ambaye namuona anapambana ila katika mapambano yake ndo hali yake imefikia apo bado anahitaji msaada huwa nafeel good sana kumsaidia,,,ila kunahawa ni marafiki nyoka unakuta mko na kazi sawa wewe unajibana unanunua kiusafiri ila yeye zake anatumia mwenyewe kwenye vitu binafsi alafu anataka wewe umsaidie hawa nao huwa nawasaidia ila huku nikifikiria kabsa huyu ni rafiki mnyonyaji
 
Eeeh kuna hao watu asee, Nimejitamkia ufala na ujinga wangu unaishia 2023. Mwaka huu ni aheri nionekane mchoyo ila siazimishi.
Mie gari siazimishi aisee maana kila mtu ana uendeshaji wake pia mafuta yamepanda bei mno mm huwa napiga full tank mwisho wa mwezi najua nisipotoboa basi angalau siku 20 hadi 25 zinafika nikiwa sijaishiwa mafuta sasa kuna watu wahuni kweli anakwambia hebu naomba gari yako niende mahali flani ukimpa sehem ambayo angeenda kwa mafuta ya elf 20 yeue anaweka ya 10 elf.
Kingine huwa hawajui kuna tyre wear, oil na vingine yeye anakwambia nitaweka mafuta
 
Jifunze kusema hapana bila kutoa sababu. Huo sio usafiri wa umma. Na Kama una mpa mtu Basi ni Yule wandani kabisa mnae heshimiana kwa sbb anakueshimu na Mali yako ataieshimu.
Nimepokea kiongozi, ninaahidi kufanyia kazi
 
Binafsi, hii kitu inanisunbua sana kwenye harakati hizi za maisha na ukijumlisha na mambo ya kidini haya. Unajikuta unasaidia ila wewe unaumia kwa Bill za matengenezo na mafuta wakati huo uliyemsaidia hata kusema aone sababu ya kukusaidia ili siku nyingine pia aweze kuazima hawafanyi. Ila nimejisemea moyo, ujinga na ufala umeishia 2023.
 
Back
Top Bottom