Hauko peke yako ndg yangu, Watanzania wengi sana wanamkubali huyu mama. Hawa wachache wanaokesha wakimtukana na kumdhalilisha ni matokeo ya pepo chafu za Ukanda na udini zilizowavaa pamoja na hofu ya wivu iliyowajaa.....mimi nawaita haters!!
Huyu mama ni mwanasayansi mkubwa mno wa utawala........unahitajika kuwa conscious sana kichwani kuelewa hili. Ukiangalia jinsi anavyowajibu kisayansi wazushi wa hoja ya bandari ndo utakapomkubali, watu wamefura mpaka wamepasuka yeye kama yeye hajawajibu neno hata moja bali ameacha vyombo vyake tu vifanye kazi. That's what we call leadership!!!
Udhalilishaji woooote wanaojaribu kuufanya kwake anaujjbu kwa vitendo tu; maji zaidi ili wasikaukiwe na mate wazidi kutema matusi zaidi na mabarabara zaidi ili wapate kusafiri huku na huko kusambaza matusi yao.
Mama ana utulivu, anapiga kazi kwa amani kabisa bila kuyumbishwa na mashinikizo ya wasiompenda. Nafikiri anajua kuwa uongozi huu ni mtihani maalum kwake kutoka kwa Muumba kama inavyodhihirishwa na matukio haya mawili makubwa;
a) kifo cha JPM bila yeye kutarajia kuwa atakuja kushika kiti chake,
b) Mipango iliyoshindwa ya kujaribu kumzuia asishike kiti cha urais.
Haya matukio mawili yanampa picha, bila shaka, kuwa uongozi wake ni mtihani mkubwa.......pengine kuliko wote na ndo maana anajaribu kuyaepuka majaribu haya kwa umakini kabisa!!