Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Kujiuliza ni muhimu maana katika demokrasia ya vyama vingi lazima tujenge uvumilivu wa kuwasikiliza wanaotukosoa.
Ni wiki tu imepita na yaliingia magari ya ving'ora, magari ya washa washa na polisi defender kem kem kutoka sehemu zote za Tanzania.
Vijana wamekula posho kwa kusikmama kwenye makutano ya karibu barabara zote kubwa huku wapipigwa jua siku nzima.
Kwa wananchi wengi wa Dr hiki kilikuwa kituko, kwa wale wenye uchungu na fedha yao wakasema ni matumizi mabaya ya fedha zetu.
Raha ya watu wa Dra ni moja tu, kama halimhusu atakutazama kwajicho la pembeni na kwenda zake.
Najiuliza hivi nchi ilitaka kupinduliwa, kulikuwa na jaribio la uvamizi wa Dar. au kuna mabomu yameteguliwa mahali.
Habari za intelijensia zinasemaje?
Mwisho wa siku mtu unajiuliza, je wangeruhusiwa kuandaman hao kina Mbowe, kungekuwa na tofauti gani na sasa tulivyo?
Matumizi makubwa ya polisoi , was it really necessary?
Halafu mtaweza kweli kukaa meza moja na kujadiliana mustakabali wa nchi hii inaitwa Tanzania?
Nafikiri tu!