Najiuliza tu, ile nguvu kubwa kuzima maandamano was it really necessary?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594



Kujiuliza ni muhimu maana katika demokrasia ya vyama vingi lazima tujenge uvumilivu wa kuwasikiliza wanaotukosoa.
Ni wiki tu imepita na yaliingia magari ya ving'ora, magari ya washa washa na polisi defender kem kem kutoka sehemu zote za Tanzania.
Vijana wamekula posho kwa kusikmama kwenye makutano ya karibu barabara zote kubwa huku wapipigwa jua siku nzima.
Kwa wananchi wengi wa Dr hiki kilikuwa kituko, kwa wale wenye uchungu na fedha yao wakasema ni matumizi mabaya ya fedha zetu.
Raha ya watu wa Dra ni moja tu, kama halimhusu atakutazama kwajicho la pembeni na kwenda zake.

Najiuliza hivi nchi ilitaka kupinduliwa, kulikuwa na jaribio la uvamizi wa Dar. au kuna mabomu yameteguliwa mahali.
Habari za intelijensia zinasemaje?

Mwisho wa siku mtu unajiuliza, je wangeruhusiwa kuandaman hao kina Mbowe, kungekuwa na tofauti gani na sasa tulivyo?

Matumizi makubwa ya polisoi , was it really necessary?
Halafu mtaweza kweli kukaa meza moja na kujadiliana mustakabali wa nchi hii inaitwa Tanzania?


Nafikiri tu!
 
Mleta mada kwenda zako maandamano yalikuwa yafanyike kwa kiswahili wewe kwenye kichwa cha maada unaweka vingereza vyako nenda kaandamane uingereza huko na vingereza vyako
 
Wamewapa promo tu kina Lisu, habari zilitangazwa dunia nzima , nilishangaa mpaka vyombo vya India vimeripoti😆😆😆
Anyway, Mbowe and his family took advantage of the free publicity na wakaitumia vizuri. Na sisi wenye magari yetu ya washa washa, angalau tuliyatoa nje yafanye mazoezi.
So yes, it was necessary in a way😆😆😆😆
 
Mleta mada kwenda zako maandamano yalikuwa yafanyike kwa kiswahili wewe kwenye kichwa cha maada unaweka vingereza vyako nenda kaandamane uingereza huko na vingereza vyako
Mkuu kama umesoma Kayumba hilo litabaki kuwa tatizo lako.
Sakata hili la majaribio ya maandamano yameonwa dunia nzima, siyo ninyi waswahili tu.
 
Kuna unuhimu wa Kamati za siasa zinazomshauri Rais, wakae chini na kutathmini uharibifu wa sifa ya nchi kimataifa kama a free democratic society.
 
Mimi nadhani kuna ajenda ya siri yakumchafua mama, ila nadhani ameyataka mwenyewe kwasabu watu wote waligokuwa wanatuhumiwa kwa mambo ambayo siyo mazuri serikali ya awamu ya tano wote kawapandisha vyeo, jinsi mfalme alivyo ndi vyo na watu wake walivyo. Wasingekubali wao wawe na matope alafu aliye wateuwa abaki msafi walijua saa yoyote huyu anaweza kutugeuka kwahiyo na yeye lazima tumsilibe matope afanane na sisi. Ni mshauri tu ajitahidi kujinasua kwenye huu mtegokabla mambo hayajamwendea kombo zaidi. Bado anamda mzuri wakujikosha CDM kinazidi kupata nguvu kila siku huku chawa wakimrubuni kwa mkkakati isiyo na tija.
 
Kuna unuhimu wa Kamati za siasa zinazomshauri Rais, wakae chini na kutathmini uharibifu wa sifa ya nchi kimataifa kama a free democratic society.
Kaulize Kenya kikichowakuta maandamano yakiharibu sifa ya nchi hadi balozi za nje zikashauri raia wake wasiende kutalii Kenya

Na utalii ukashuka biashara zikafungwa zikiwemo za wawekezaji, ndege zikapungua kutua Jomo Kenyatta airport sababu waandamanaji walikuwa wakielekea Airport na kuzuia waenda Airport wasiende nk safari za kimataifa watu wakashindwa kusafiri sababu ya barabara kufungwa na waandamanaji

Tanzania nchi dume kuzomewa tunna jumuiya ya kimataifa sababu vibaka hawakuandana ni kitu kidogo kuliko kama kungetokea uharibifu kama kenya
 
Sidhani kama soo hili limekiinua chdema. Ila ulimwengu umemjua mama for what she is.
Busara ingetumika zaidi kuliko ilivvo dhihiri.
 
Kenya na Tanzania kisiasa ni mbingu na nchi.
Kenya kuna landless destitutes, wakifa barabarani they have very little to lose.
Tanzania mwanasiasa anaandamana Mbeya anakimbilia hekaluni kwake Moshi.
 
Wanadai eti upinzani umekufa, mara wapinzani hawanitishi, mara hakuna mpinzani wa kuongoza nchi, wakitishiwa maandamano kdg wanatumia nguvu za ajabu, yaani munawadharau halafu upande wa pili MUNAWAOGOPA.... Ukweli ni huu Chadema wana nguvu sana sana sana, hebu wapeni haki zao muone, lkn musisahau Mungu yupo.
 
Wamemtia hofu ya kijinga Rais Ili wajiletee drama ya hovyo kuwa wao ndio walinzi wake wakubwa.
 
Kama ukihudhuria
Tupe mrejesho na mns unajua jibu lake..
Kama ujahuduria ulishiriki via mtandaoo
Napitatu
 
Badala yake police ndio wakaandamana😂
 
Badala yake police ndio wakaandamana😂
Ni zoezi la gharama kwa serikali, mis use of resources.
Lazima kuna njia nzuri zaidi kushughulikia matatizo katika jamii, 4R sijui kama imetumika hapa.
 
Ulitakiwa uandamane ndio ungejua ilikuwa necessary au hapana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…