Hawa jamaa wanadukua taarifa binafsi mfano sms unazotuma , wzup message pia, wanaingia ktk gallery ya picha zako.Basi wakianza kudai siku ya tano usipowalipa siku ya sita saa 12 asubuhi washaanza ikifika saa 7 mchana hujalipa wanaingia gallery wanachukua picha yako wanaandika na maneno ya kishenzi wanakutumia ,wanawatumia pia ulioandika wadhamini na baadhi watu uliwa save ktk contact zako ambao una mawasiliano nao mara kwa mara.Pia wakati wanakupigia bila we kujua wanaunganisha kwa kuwapigia jamaa ulio wa save ktk contact zako huku wanakudhihaki lipa deni jamaa zako wakati huo wameunganishwa wanaskia ! ni udukuzi wa waziwazi huwezi kujua mpaka jamaa yako akupigie simu akueleze mbona nimeskia hivi ?? ni kweli ??
Hawa jamaa ni wadukuzi wa hali ya juu.
Kuna wakati mwingine wanaingia wzup yako wanatafuta kama una message zozote zinazohusiana na mapenzi basi wanazi highlight kwa rangi kama vile kijani then wanakutumia ktk wzup yako ! manake wanakwambia wanajua siri zako ! hivo uwalipe ili wakufichie siri ! Hii ni blackmail ya hali ya juu.Hata wanapokutishia tutawambia ndugu zako wakulipie au tuta kuundia kundi la wzup wakuchangie ni Balck mail ya hali ya juu !
Wakati mwingine wanapokupigia kwa kuwa wanakuwa wengi ktk hizo ofisi zao unawaskia kabisa wanasema huyu lazima alipe leo mbona ana pesa kwenye simu ?? na wengine anawatumia ?? manake wanadukua mpaka mawasiliano yako na kiasi gani unakuwa nacho ktk simu hawa jamaa ni hatari sana !
Wanaangilia ktk contact list yako aidha kama mwanamume wanatafuta wakike walio ktk contact list yako ndo wanawatumia message zao na picha na kama we ni KE wanatafuta wa kiume ambao wanahisi ni wapenzi wako.Au wakijua huyu ni boss wako basi wanae.Yaani wana study contact list yako utadhani ya kwao na wana monitor mawasiliano yako na wakipata tu loop hole wana take advantage.Mfano wakijua huyu ndo mpenzi wako kutokana na mawasiliano ya simu basi watakuandama kumpelekea message zao za kishenzi kuwa we tapeli na mwizi wa mitandaoni.
Kwa hiyo kuweni makini sana.Wana uwezo wa kusoma message unazopokea na kutuma kwa wakati kiufupi wanajua kila kitu unachokuwa unafanya wanapokuwa wanakufuatilia ulipe deni lao.Wanaingia ktk picha galleryy wanatafuta picha ambazo hazifai kuonyesha hadharani wanakutumia kuwa usipolipa watazinclude ktk wzup group watalounda kwa ajili yako.
Mi nashangaa vyombo vya serikali vimekaa kimyaaaa !!
Hata vyombo vya habari kama TV na magazeti vimekaa kimyaa !
Magazeti ya uchunguzi hii ni habari ambayo kama mtaiandika kwa kina jamii itafunguka na serikali itachukua hatua ktk hili janga.Chukueni hatua wakati ni sasa !
NB:Naweza kuandika kitabu kuhusiana na hawa jamaa kwa leo inatosha