Najuta kuhamia kwangu Kerege

Hongera kwa kujenga itakuja kukuaa hata mbele huko, kama kazi/mishe mjini kati jaribu kupanga maeneo ya karibu yenye bei nafuu ila pawe poa,tena mengi tu. Mafuta na kukesha barabarani utazeeka kabla ya umri wako.
 
Nyie ndo mnatubana bana huku Kerege.
Rudi mjini tuachie shamba.
 
Hujaelewa kumbe... Anaweza kuwa na kiwanja huko lakini sio kukaa huko
yupi sasa ? km ttunayemzungumzia mbona post#1 imejieleza, p/se anza mwanzo ndipo utaelewa mtiririko

post: 33428902 said:
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).
 
jamani tenganisheni UKWELI na UONGO
enzi za Mkwere mwenzako kajenga sasa hali ni ngumu hata mpangaji hapati
Eti wewe una sema leo biashara imechanganya, ni ipi hiyo? maana hata ya kutakatisha pesa, ngada na mashuzi zote HAZITOKI Chinga wote wanalia, wewe ukanunue kiwanja 85m bila taarifa TRA
Tafuta waraka wa fedha kuhusu zaidi ya 10M popote ni lazima uitolee maelezo (huwezi nikubandikie sasa hivi uisome)
wewe unasema mwezi uliopita, hata aliyekuuzia angeshajieleza kwanini KODI hamjalipa
Mleta Mada kasema ukweli tuliobaki ni matajiri nyuma ya keybody
 
Ardhi ni mali Mkuu hata iwe mashambani, wenzetu jirani tu hapo wanaithamini kuliko sisi tunaoona Kerege hapafai
Huko Kaskazini Nchini mwetu sio WEHU mtu anaamka Mwika, Marangu na hata Rombo anafanya kazi KIA au Arusha kwenda na kurudi kwanini asitoke mgombani akapange Sombetini Arusha
Fika huko siku moja uone Mini bus zinavyojaza wakati Treni za umeme hakuna Mkuu, watu hawalali labda hapo Posta Dar hamtaki kuamka
 
Una vimelea vya utumwa na umaskini, niulize nikufundishe kitu
 
nyumba za NHIF [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Tatizo mtu umri ukienda anahisi kudrop vitu vya kumpa starehe ndio kukua eti...wenzetu wazungu wana afya njema muda mwingi sababu wanajua nini maana ya kujipa raha, beach utakuta wazee wa kutosha, club wamoo, ilimradi wanapata furaha...sada bongo ili uonekane umekua ni kujifungia ndani na kuinamisha bichwa chini all the time.
Tusiambukizane lifestyle kwa nguvu
 
Mzee wangu alikuwa anakaa mjini kati.

Wakati nipo kidato cha kwanza akahama mjini anakaenda nje ya mji kisa ng'ombe wake wanakosa majani.

Kimbembe kilianzia hapa;

1. Wakati wa likizo nilikuwa nasoma tuition mchikichini, akawa ananiamsha saa 4:00 alfajiri tunaondoka wakati anaenda kazini ananiacha kkoo majira ya saa 6:30 asubuhi (hapo vibaka wanamalizikia kwenda makwao).

2. Ananiachia na 5000 ya kulipia vipindi, lunch na nauli ya kurudi nyumbani. Hiyo ni kila siku. Kwa siku 5 ni sawa na 25,000/- (hii ni zaidi ya miaka 15 iliopita) na hapo usafiri ulikuwa shida si mchezo. Unapanda magari hata matatu kurudi nyumbani. Au wakati mwingine namsubiri wakati anarudi pale fire nidandie lift.

3. Weekends tulikuwa tunakutana UDSM kwa ajili ya discussion na washkaji. Lazima anipe 5000 ya nauli na chakula.

4. Yeye mwenyewe alikuwa anafanya kazi posta, alikuwa anaweka full tank kila jumatatu.

Nilikuwa nachoka sana na yeye mwenyewe alikuwa anachoka sana.

Hadi namaliza ilikuwa kimbembe. Wakati nahama nikatafuta nyumba katikati ya mji.

Naenda sehemu yeyote, muda wowote.
 
Nina rafiki zangu wawili. Wote hawajaoa.

1. Mmoja ni dokta, anafanya kazi muhimbili na sehemu nyingine kama part time. Amepanga nyumba upanga. Analipa kodi 600,000. Anaenda kazini kwa miguu wakati mwingine na gari. Akiweka full tank anakaa hata week 3 au mwezi kabisa. Weekends ndo anatoka mjini kuja nje ya mji kula bata.

2. Wa pili ni engineer, ofisi ipo posta, wakati wa JK akapiga deal akapata kama 80M. Akakimbilia kununua kiwanja huko mbele ya bunju akajenga fastafasta. Kimbembe kikaja muda anaotumia toka nyumbani hadi ofisini. Anakaa njiani almost masaa 3 hadi 4 kila siku ya ofisi. Anatumia mafuta ya 400,000 kila mwezi. Baada ya mwaka akaifunga nyumba akatafuta apartments za NHC ilala anakaa huko sasa. Ile nyumba anafikiria kuiuza.

Msimamo wangu binafsi; nitakaa nje ya mji kama nataka kustaafu. Mizunguko nimeipunguza zaidi ya 90%.
 
Watanzania tunapoteza muda mwingi kizembe sana ....just imagine huyo anaeishi mlandizi na kufanya shughuli zake kkoo ni muda gani anaupoteza akiwa njiani kila siku?

Ukipiga hesabu unaweza kuta kwa mwaka anatumia miezi mitatu akiwa barabarani.
 
Hiyo ndio nyumba uliyojenga au ni banda LA uani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…