Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Tatizo la kujenga nje ya mji hata ukisema upangishe hiyo nyumba huwezi pata mpangaji,we unafikiri nani akapange kilomita zaidi ya 35 kutoka town ni ngumu. Bei tunazonunulia viwanja dsm ni bora ukaenda mkoani utapata kiwanja karibu kabisa na mjini unajenga nyumba yako safi na ukiipangisha hukosi kodi ya 200k au 150k kwa mwezi. Mfano mkoa kama Tanga ukiwa na million 6 au 7 unaweza kupata kiwanja within 15 kilomita kutoka mjini, ukijenga nyumba nzuri kupata mpangaji ni uhakika. Kodi utakayopata mkoani unaitumia kupanga sinza au magomeni
Kweli Mkuu hapo nina Mkopo benki moja ya Wahindi riba 21% toka 2016
 
Tatizo la kujenga nje ya mji hata ukisema upangishe hiyo nyumba huwezi pata mpangaji,we unafikiri nani akapange kilomita zaidi ya 35 kutoka town ni ngumu. Bei tunazonunulia viwanja dsm ni bora ukaenda mkoani utapata kiwanja karibu kabisa na mjini unajenga nyumba yako safi na ukiipangisha hukosi kodi ya 200k au 150k kwa mwezi. Mfano mkoa kama Tanga ukiwa na million 6 au 7 unaweza kupata kiwanja within 15 kilomita kutoka mjini, ukijenga nyumba nzuri kupata mpangaji ni uhakika. Kodi utakayopata mkoani unaitumia kupanga sinza au magomeni

Kweli kila mtu anawaza ajuavyo yeye...yaan nipewe laki 2 kwa mwezi??hapana...!ila kuna biashara kichaa sana...labda ujenge nyumba ukopee mkopo mzuri benk...mwee huyo laki 2 mm naipata kwa siku 1!nah!
 
Yaani ukishazoea gari jamani kurudi kwenye daladala inabid wito haswa!
Kama mtu ni educated anaweza hata kutembea kwa mguu, ila kama ameenda shule lakini hakuelimika itakuwa ngumu. Maisha wengi yanawashinda kwa kutokuwa na ujasiri wa kujishusha wakati hali inakushusha. Wewe unan'ang'ania juu mpaka tawi linakatika unadondoka ndii. Kama ni kijana let say 30s au 40s anaweza kununua kapikipiki kadogo kakamtoa huko kerege hadi Tegeta nyuki, anakawekesha anapanda daladala yake hadi town. Ila kuamka ni saa 11 kama ameajiriwa
 
Labda sikueleweka..ishu hapa sio jirani akiniona nimeshika chuma la eicher atasemaje .ishu ni yale mazoea mzee baba!hapa hakuna cha elimu ya kujitmbua wala nn...!kuna kaulemavu kapo sana ukizoea kutembelea gari!wenyewe wanakajua!
 
Utaishije nje ya mji kwa kigezo cha kukimbia gharama wakati usafiri wa daladala tu unakucost 150000 kwa mwezi na ukiforce kuendesha gari unatumia laki 4 kwa mwezi?.
Bora upange apartment city centre,nyumba weka mradi wa mifugo na nyumba yako akae msimamizi kama hakuna wapangaji
 
acha usiwafuate waswahili wanaopenda Mjini.
Hapo Kerege patajakuwa Mjini kati kabisa, mwaka 1979 Sinza Makaburini ndio palikuwa mwisho wa Mji wa DSM linafuata pori hadi UDSM
Leo Kibaha ni Mjini kabisa ngoja hiyo njia 6 ya Highway km hukona mwendo kasi halishii Kimara
Ardhi ni mali huwezi linganisha Ardhi yenye ukubwa sawa kwa Miji ya Tanga, Dodoma au Mwanza
Tafuta wenyeji, Mkiti au Mjumbe wakutafutie wapangaji hiyo ni Rasilimali kubwa kuliko kupanga km Mhindi Mjini, Shika ardhi popote km Elimu kwani ni utajiri kuliko hao wezi wa leo tu
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya KEREGE sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee NAJUTRAAA maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya Nyumba Sinza (400,000/=). Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini Nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini Sana.
FUNZO: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Nina maoni haya: Kujenga na kuishi sehemu ya mbali na mji kama hiyo yako kwangu mimi ni jambo zuri sana. Na zaidi niseme sehemu za Kerege ni nzuri sana na kuna hewa safi na mtu unakuwa mbali na rabsha za mjini. Na kingine ni kuwa una uhuru wa kufanya mambo mengi kama bustani na ufugaji. Changamoto yake kubwa ni security. Maeneo kama hayo yanakuwa hatari hasa wakati wa usiku kwa sababu hakuna watu wengi. Kuishi maeneo kama hayo inatakiwa mtu uwe na uwezo mkubwa. Vitu kama gharama za usafiri visiwe issue, na uwe na ulinzi madhubuti (japo majambazi wakidhamiria wanakuwa huru zaidi kwa sababu ya kukosekana msaada wa haraka). Miaka ya nyuma kuna jamaa mmoja alijenga karibu na shule ya Bunju B. Watu wengi walikuwa wanamcheka na kusema amehamia porini. Leo hii hakuna anayemcheka na eneo limekuwa mji. Ushauri wangu: Hayo maeneo ni mazuri na siyo muda mrefu sana kutakuwa mji wenye watu wengi. Kama huna shida sana usiuze. Tafuta mbinu nyingine tu za kujikwamua na baadae utaona faida yake.
 
acha usiwafuate waswahili wanaopenda Mjini.
Hapo Kerege patajakuwa Mjini kati kabisa, mwaka 1979 Sinza Makaburini ndio palikuwa mwisho wa Mji wa DSM linafuata pori hadi UDSM
Leo Kibaha ni Mjini kabisa ngoja hiyo njia 6 ya Highway km hukona mwendo kasi halishii Kimara
Ardhi ni mali huwezi linganisha Ardhi yenye ukubwa sawa kwa Miji ya Tanga, Dodoma au Mwanza
Tafuta wenyeji, Mkiti au Mjumbe wakutafutie wapangaji hiyo ni Rasilimali kubwa kuliko kupanga km Mhindi Mjini, Shika ardhi popote km Elimu kwani ni utajiri kuliko hao wezi wa leo tu
Nina ushuhuda: Pale Sinza, miaka ya nyuma kulikuwa ni pori. Chuo kikuu enzi hizo wakachukuwa eneo kubwa na kuwagawia ma-lectrurers wao. Kuna waliokataa wakasema ''huku porini kwenye madimbwi ya maji ni nani atakuja kukaa huku. Leo hii Sinza imegeuka na kuwa eneo tofauti kabisa. Hapo ulipozunguzumzia Sinza makaburini na maeneo yote ya karibu yalikuwa na pori na ndiyo kisa cha kuyafanya yawe sehemu ya kuzikia.
 
Sawa ardhi ni mali lakini malengo yake ya kukwepa kodi ya pango mjini hayajatimia kwa sasa. Kaenda kununua mbali mno haimsaidii. Labda kama angenunua huko kwa malengo ya kufuga lakini si makazi wakati shughuli zake mwenyewe ziko posta mpya. Hivyo mimi namshauri eneo hilo alifanye la mifugo ajipange atafuta karibu apange baadaye anaweza kuja kupauza kwa bei nzuri tu
acha usiwafuate waswahili wanaopenda Mjini.
Hapo Kerege patajakuwa Mjini kati kabisa, mwaka 1979 Sinza Makaburini ndio palikuwa mwisho wa Mji wa DSM linafuata pori hadi UDSM
Leo Kibaha ni Mjini kabisa ngoja hiyo njia 6 ya Highway km hukona mwendo kasi halishii Kimara
Ardhi ni mali huwezi linganisha Ardhi yenye ukubwa sawa kwa Miji ya Tanga, Dodoma au Mwanza
Tafuta wenyeji, Mkiti au Mjumbe wakutafutie wapangaji hiyo ni Rasilimali kubwa kuliko kupanga km Mhindi Mjini, Shika ardhi popote km Elimu kwani ni utajiri kuliko hao wezi wa leo tu
 
Sawa ardhi ni mali lakini malengo yake ya kukwepa kodi ya pango mjini hayajatimia kwa sasa. Kaenda kununua mbali mno haimsaidii. Labda kama angenunua huko kwa malengo ya kufuga lakini si makazi wakati shughuli zake mwenyewe ziko posta mpya. Hivyo mimi namshauri eneo hilo alifanye la mifugo ajipange atafuta karibu apange baadaye anaweza kuja kupauza kwa bei nzuri tu
Duuh
 
Tofautisha ardhi na nyumba. Thamani ya nyumba ni ardhi. Mbweni pale viwanja vya milioni 3 ulikuwa unakatiwa na halmashauri ya jiji.
Watu waliokuwa na hekari 10 Mbweni, wamepata faida sana.
Mleta mada kaongea point sana. Usijenge bila kujipanga. Nunua ardhi, subiri.
 
Back
Top Bottom