Kwa Dar kwa mfanyakazi wa kawaida kutaka ujenge nyumba kiwanja utapata kilomita 40 au zaidi nje ya mji ujenge.
Mbaya zaidi ofisi nyingi ziko posta hivyo itakulazimu uwe unaamka sa 9 ili kufika ofisini sa 2, na kurudi nyumbani ukitoka sa 11 unafika sa 3. Hii sababu ni moja tu ya miundombinu mibovu kwa hapa Dar es salaam, barabara ya kuja na kutoka mjini ni zile zile hakuna njia mbadala na kama zipo ni za hovyo sana.
Mimi Dar siwezi kujenga, ni hasara tupu, ggharama za usafiri kutoka kwako hadi kazini ni zaidi ya 200,000 kwa mwezi, hujaja chakula, uusumbufu mwingine alafu niwe najisifu tu eti kisa nakaa kwangu.
Nenda kinyerezi, mbezi makabe, goba, mabwepande na kwenda huko Mapinga, mbweni, kitopeni, nk watu wametelekeza nyumba nzuri kule kwa sababu ya adha ya usafiri.
Bora upange jirani na mjini uishi kwa raha kuliko kua na kwako huku unaishi kwa shida kisa unaishi kwako. Kuna mshikaji wangu kajenga huko kimara porini imebidi akimbie nyumba, akapange apartment kariakoo.
Mimi nimepanga jirani tu na kazini kwangu, kilomita 8, hata sa 1:30 natoka kwangu na nafika kazini kabla ya ya 2:00 na maisha ni matamu sana.
Maisha ni hesabu, ukifanya miscalculation maisha yako yatakua magumu sana.