Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

@nizakale,kwani wenzetu mmajenga nyumba kwa ajiri ya kukwepa kodi au mahali pa kupumzikia baada ya nguvu kwisha(kustaafu)??

maana haiingii akilini unagharamia usafiri binafsi 450k kwa mwezi unaogopa kodi ya 450k kwa mwezi!!huo ni ukichaa.ua kimoja hapo urahisishe maisha.
 
Sawa ardhi ni mali lakini malengo yake ya kukwepa kodi ya pango mjini hayajatimia kwa sasa. Kaenda kununua mbali mno haimsaidii. Labda kama angenunua huko kwa malengo ya kufuga lakini si makazi wakati shughuli zake mwenyewe ziko posta mpya. Hivyo mimi namshauri eneo hilo alifanye la mifugo ajipange atafuta karibu apange baadaye anaweza kuja kupauza kwa bei nzuri tu
sawa lakini asijutie
mm nitamtafuta @ joshua_ok aiuzie maana kuna mdogo wangu mwaka 2010 alinunua pori ndani kilomita 5 kutoka Kibanda cha Mkaa Kimara kabla ya Mbezi Louis wanajiita Makao Mapya, leo kuna Makanisa na Mahoteli, kuna Shule za Bweni nk
Lengo asiweke kukwepa Kodi aweke km Rasilimali
MMikoani ndio hakufai kabisa maendeleo yatachelewa kwani km Dodoma viwanja ni milioni 15 Moshi na Arusha ndio hakuna kabisa ni vya urithi
kwa hiyo ajifunze Ardhi haichezewi
hapa nina safari ya kuhamia Kilosa hata miezi 6 Waziri Lukuvi kaachia maekari huko, najua sitapewa ila nitanunua na hicho cha KEREGE naingia PM yake
 
Kwa Dar kwa mfanyakazi wa kawaida kutaka ujenge nyumba kiwanja utapata kilomita 40 au zaidi nje ya mji ujenge.

Mbaya zaidi ofisi nyingi ziko posta hivyo itakulazimu uwe unaamka sa 9 ili kufika ofisini sa 2, na kurudi nyumbani ukitoka sa 11 unafika sa 3. Hii sababu ni moja tu ya miundombinu mibovu kwa hapa Dar es salaam, barabara ya kuja na kutoka mjini ni zile zile hakuna njia mbadala na kama zipo ni za hovyo sana.

Mimi Dar siwezi kujenga, ni hasara tupu, ggharama za usafiri kutoka kwako hadi kazini ni zaidi ya 200,000 kwa mwezi, hujaja chakula, uusumbufu mwingine alafu niwe najisifu tu eti kisa nakaa kwangu.

Nenda kinyerezi, mbezi makabe, goba, mabwepande na kwenda huko Mapinga, mbweni, kitopeni, nk watu wametelekeza nyumba nzuri kule kwa sababu ya adha ya usafiri.

Bora upange jirani na mjini uishi kwa raha kuliko kua na kwako huku unaishi kwa shida kisa unaishi kwako. Kuna mshikaji wangu kajenga huko kimara porini imebidi akimbie nyumba, akapange apartment kariakoo.

Mimi nimepanga jirani tu na kazini kwangu, kilomita 8, hata sa 1:30 natoka kwangu na nafika kazini kabla ya ya 2:00 na maisha ni matamu sana.

Maisha ni hesabu, ukifanya miscalculation maisha yako yatakua magumu sana.
 
Kuna viwanja vinauzwa 1.3milion huko kisemvule na vikindu, huwa najiuliza kiwanja cha 1.3milion si kitakuwa mbali sana na mjini..yaani kila siku una drive 70km kwenda na kurud kazini..lakin hongera kwa kuwa na Nyumba
nilidhani unasema Milioni 13 kumbe milioni 1
Dodoma huku unapata eka moja porini kilomita 18 kutoka mjini kwa 1,3M, kiwanja kinafika 20m maeneo ya kujenga, ambayo joshua_ok anafananisha na KEREGE
mm nitafutieni kiwanja aua shamba iwe Kibaha, Chanika au Bunju najua barabara zipo
 
Huko inabd shuhuli zako Ziwe marneo hayo hayo sio utoke vikindu had posta kila siku utapata kichaa
Kuna viwanja vinauzwa 1.3milion huko kisemvule na vikindu, huwa najiuliza kiwanja cha 1.3milion si kitakuwa mbali sana na mjini..yaani kila siku una drive 70km kwenda na kurud kazini..lakin hongera kwa kuwa na Nyumba
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Kujenga sio tatizo kinachotakiwa usijenge maadamu umepata kiwanja.Kabla ya kujenga zingatia yafuatayo:
1.Kiwanja kipo wapi
2.umbali na huduma muhimu km.mjini,ofisini,hospital n.k
3.Miundo mbinu umeme,maki na Barbara
4.Je ukijenga nyumba inapangishika au kuuzika siku ukiamua?
Hivyo ni baadhi ya vitu vya kuzingatia.
 
Hujakosea Ila ukifikiria kwa haraka haraka utakosea zaidi hakuna kosa kubwa kama kuuza ukiuza iyo nyumba kufuatana na mzunguko wa pesa ulivyo kwa sasa utajuta kuzaliwa pengine unaweza kuja kuwa chizi note sio lazima uokote makopo! Chizi wa mawazo yasio kwisha!! Me nime jenga sehemu tuliyokuwa tunaita nje ya mji Sala Sala Ila ninatarajia kuamia huko shamba huko unako paona umekosea! Kwa kiwete kama utakuwa unapajuwa!!
 
Mkuu uza hiyo gari tafuta Toyota hiace ya 15milion, Asubuhi unapokuja mjini beba abiria, unaporudi kerege pia beba abiria. weekend aamka asubuhi piga trip kazaa tegeta bagamoyo.. Hapo utakuwa umejiongezea kipato lakini pia utakuwa umepata hela ya mfuta kila siku ya kuendea kazini..
 
Nina ushuhuda: Pale Sinza, miaka ya nyuma kulikuwa ni pori. Chuo kikuu enzi hizo wakachukuwa eneo kubwa na kuwagawia ma-lectrurers wao. Kuna waliokataa wakasema ''huku porini kwenye madimbwi ya maji ni nani atakuja kukaa huku. Leo hii Sinza imegeuka na kuwa eneo tofauti kabisa. Hapo ulipozunguzumzia Sinza makaburini na maeneo yote ya karibu yalikuwa na pori na ndiyo kisa cha kuyafanya yawe sehemu ya kuzikia.
Iko hivo hata bunju miaka ya nyuma palionekana kijijini lami ilikuwa inaishia nyaishozi kuja huku kidongo chekundu hakuna umeme leo hapashikiki
 
Bei tunazonunulia viwanja dsm ni bora ukaenda mkoani utapata kiwanja karibu kabisa na mjini unajenga nyumba yako safi na ukiipangisha hukosi kodi ya 200k au 150k kwa mwezi. Mfano mkoa kama Tanga ukiwa na million 6 au 7 unaweza kupata kiwanja within 15 kilomita kutoka mjini, ukijenga nyumba nzuri kupata mpangaji ni uhakika. Kodi utakayopata mkoani unaitumia kupanga sinza au magomeni

Asante sana, umeongea kitu rahisi na halisi.... mwenye utimamu atachukua hili.
 
Watanzania huwa Hatupigi hesabu za mafuta na muda tunaopoteza ndo maana tuko radhi tukajenge mbali kuliko kupanga. Tukipiga hesabu bora kupanga karibu ma shughuli zako kuliko kuishi mbali hata kama ni kwako
 
Kwa Dar kwa mfanyakazi wa kawaida kutaka ujenge nyumba kiwanja utapata kilomita 40 au zaidi nje ya mji ujenge.

Mbaya zaidi ofisi nyingi ziko posta hivyo itakulazimu uwe unaamka sa 9 ili kufika ofisini sa 2, na kurudi nyumbani ukitoka sa 11 unafika sa 3. Hii sababu ni moja tu ya miundombinu mibovu kwa hapa Dar es salaam, barabara ya kuja na kutoka mjini ni zile zile hakuna njia mbadala na kama zipo ni za hovyo sana.

Mimi Dar siwezi kujenga, ni hasara tupu, ggharama za usafiri kutoka kwako hadi kazini ni zaidi ya 200,000 kwa mwezi, hujaja chakula, uusumbufu mwingine alafu niwe najisifu tu eti kisa nakaa kwangu.

Nenda kinyerezi, mbezi makabe, goba, mabwepande na kwenda huko Mapinga, mbweni, kitopeni, nk watu wametelekeza nyumba nzuri kule kwa sababu ya adha ya usafiri.

Bora upange jirani na mjini uishi kwa raha kuliko kua na kwako huku unaishi kwa shida kisa unaishi kwako. Kuna mshikaji wangu kajenga huko kimara porini imebidi akimbie nyumba, akapange apartment kariakoo.

Mimi nimepanga jirani tu na kazini kwangu, kilomita 8, hata sa 1:30 natoka kwangu na nafika kazini kabla ya ya 2:00 na maisha ni matamu sana.

Maisha ni hesabu, ukifanya miscalculation maisha yako yatakua magumu sana.
Bora uwashauri wenzio wenye mawazo kama yako ili wasikimbilie kujenga maana sisi wenye majumba mjini tunawahitaji kama wapangaji wetu kutuingizia kipato, sasa kila mtu akijenga sisi tutakula wapi? Bora uwashauri wenzio mbaki kuwa wapangaji tu hivyo viwanja tutanunua sie na tutajenga mijengo wengine mbaki tu kuwa wapangaji.
 
Bro sehemu kibao kulikua pori hata tabata, kimara ,tegeta ila hizi sehemu angalau zipo karibu na na posta mjini ambako ofisi nyingi zipo huku tunapoelekea sie vijana wa miaka y 80 kazi ipo mana tunazidi kuuacha mji tu...

Hiwezi fananisha mapinga na wazo hata ka kulikua pori au kifuru na tabata bima au kisemvule na mbagala rangi tatu yani kisanga
Iko hivo hata bunju miaka ya nyuma palionekana kijijini lami ilikuwa inaishia nyaishozi kuja huku kidongo chekundu hakuna umeme leo hapashikiki
 
Vipi kuhusu usalama
Usalama ni changamoto isiyo na solution ya kuaminika. Kuna jamaa alikuwa maeneo hayo, ana uwezo, ameweka ukuta wenye nyaya za umeme na ving'ora na mbwa ndani lakini bado alikuwa target ya majambazi mara kwa mara. Mara wamtegeshee wakati anaingia kwenye geti au wakati mwingine waje mchana.
 
Yah..watu wanakusubiri wakati unaingia..wanakufanyia unyama wanamaliza wanapika na msosi wanakula wanasepa..majitani hadi waje kujua inakua too late.
 
Back
Top Bottom