Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Kutokana na hela kuwa ngumu nimeweka ukuta mfupi, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
"Houses are for banks, its bullshit if you pay for your house and your house doesn't pay you..unless its so beautiful that it gives you happyness and the peace of mind!"
 
Mkuu shukuru hata umejenga japokuwa ulikuwa hujajipanga, ila naamini ulijipanga ndo maana ukajenga....kuna vijana hata chumba cha kupanga ni utata..
kuna kitu kikubwa anakisema ...Ila ingawa hakijawa wazi... Unaweza sema anamaisha... hata kama amejenga bado nyumba imekuwa mzigo kwake..Inampunguzia kipato... ndiyo maana baadhi ya nyumba na hasa za kuishi ni liability.

Pili anamaanisha hiyo hela aliyojenga , badala ya kuwahi Kerege ambako ni nje ya Dar na mbali angeweza kufanya maamuzi tofauti na hela yake ikaenda mbali zaidi.

Vile vile anamaanisha kujenga siyo suluhisho, au kukaa kwenye nyumba yako mwenyewe..Ingeweza kuwa na maana kama angejenga maeneo mengine akaitumia nyumba kwa biashara au shughuli nyingine za kuingiza kipato.

Anamaanisha ameishia kujenga na sasa hawezi kunufaika na hiyo nyumba au kuyabadilisha maamuzi yake aliyofanya siku za nyuma alipokuwa amejenga.

Anamaanisha angeweza kujenga eneo jingine ambalo, kuna uwezekano wa kubadilisha matumizi ya makazi, kuwa kitu kingine.

Huyu ndugu ameweka ujumbe muhimu sana, tuufakari zaidi na hasa maeneo tunapojenga nyumba tuangalie mambo mengi ,kuliko nimejenga mimi niko kwangu silipi kodi.
 
Utaishije nje ya mji kwa kigezo cha kukimbia gharama wakati usafiri wa daladala tu unakucost 150000 kwa mwezi na ukiforce kuendesha gari unatumia laki 4 kwa mwezi?.
Bora upange apartment city centre,nyumba weka mradi wa mifugo na nyumba yako akae msimamizi kama hakuna wapangaji
Ndivyo ilivyo mkuu..Hakuna njia ni kurudi mjini kati
 
kuna kitu kikubwa anakisema ...Ila ingawa hakijawa wazi... Unaweza sema anamaisha... hata kama amejenga bado nyumba imekuwa mzigo kwake..Inampunguzia kipato... ndiyo maana baadhi ya nyumba na hasa za kuishi ni liability.

Pili anamaanisha hiyo hela aliyojenga , badala ya kuwahi Kerege ambako ni nje ya Dar na mbali angeweza kufanya maamuzi tofauti na hela yake ikaenda mbali zaidi.

Vile vile anamaanisha kujenga siyo suluhisho, au kukaa kwenye nyumba yako mwenyewe..Ingeweza kuwa na maana kama angejenga maeneo mengine akaitumia nyumba kwa biashara au shughuli nyingine za kuingiza kipato.

Anamaanisha ameishia kujenga na sasa hawezi kunufaika na hiyo nyumba au kuyabadilisha maamuzi yake aliyofanya siku za nyuma alipokuwa amejenga.

Anamaanisha angeweza kujenga eneo jingine ambalo, kuna uwezekano wa kubadilisha matumizi ya makazi, kuwa kitu kingine.

Huyu ndugu ameweka ujumbe muhimu sana, tuufakari zaidi na hasa maeneo tunapojenga nyumba tuangalie mambo mengi ,kuliko nimejenga mimi niko kwangu silipi kodi.
Sawa kutafakari ni muhimu...ila unapojenga mahali pa kuishi fikiria miaka 30 mbele...miji inapanuka Sana...hiyo kerege ni sehemu sahihi kabisa kwa siku za usoni na hasa kwa vijana ambao miaka 30 ijayo watakuwa wazee...nyumba ni aset ya kudumu Kama unaitunza..gari ni takataka tu...mpaka amenunua kerege bila Shaka Ana eneo kubwa kwa hiyo afuge na alime...asilogwe kuuza..atakuja kujuta miaka siyo mingi ijayo..
 
Mbona wahindi hawajuti japo wanakaa maghorofani toka nimekuja mjini miaka ya mwishoni mwa 1980s?
 
Kuna Rafiki yangu mmoja mnyarwanda aliwahi kuniambia kama unataka kujenga nyumba basi isizidi Km 20 kutoka City Centre otherwise gharama za Maisha zitakuwa kubwa sana. Wakati naanza kujenga miaka hiyo nilizingatia ushauri wake nikapata eneo Km 17 from City Centre ndipo nikajenga. Faida naziona sasa maana hainigharimu sana kwenda na kurudi mjini kila siku.

Ushauri kwa mtoa mada

Hiyo nyumba ya Bagamoyo weka Electric Fence kisha funga Camera na pia tafuta kijana awe House Boy kama hayo mawili ya mwanzo yakishindikana. CCTV Camera bei ni rahisi sana. Mie nimefunga kwangu na nimeweka tangazo ila kuna madogo wa kitaani walikuja ingawa mbwa waliwakimbiza lakini niliwaona na nikaenda kuonyesha zile picha kwa majirani na bodaboda wote wa mtaani. Kuna mmoja anaitwa Baba Sele alihama kabisa kitaa maana watu walikuwa wanataka kuwachoma.

Hiyo nyumba kaa nayo itakusaidia umri wa kustaafu na sio kuiuza maana cha mtu kitu na mwenye nacho sio sawa na asiye nacho
 
Nina maoni haya: Kujenga na kuishi sehemu ya mbali na mji kama hiyo yako kwangu mimi ni jambo zuri sana. Na zaidi niseme sehemu za Kerege ni nzuri sana na kuna hewa safi na mtu unakuwa mbali na rabsha za mjini. Na kingine ni kuwa una uhuru wa kufanya mambo mengi kama bustani na ufugaji. Changamoto yake kubwa ni security. Maeneo kama hayo yanakuwa hatari hasa wakati wa usiku kwa sababu hakuna watu wengi. Kuishi maeneo kama hayo inatakiwa mtu uwe na uwezo mkubwa. Vitu kama gharama za usafiri visiwe issue, na uwe na ulinzi madhubuti (japo majambazi wakidhamiria wanakuwa huru zaidi kwa sababu ya kukosekana msaada wa haraka). Miaka ya nyuma kuna jamaa mmoja alijenga karibu na shule ya Bunju B. Watu wengi walikuwa wanamcheka na kusema amehamia porini. Leo hii hakuna anayemcheka na eneo limekuwa mji. Ushauri wangu: Hayo maeneo ni mazuri na siyo muda mrefu sana kutakuwa mji wenye watu wengi. Kama huna shida sana usiuze. Tafuta mbinu nyingine tu za kujikwamua na baadae utaona faida yake.
Umenena points,
Kama anauwezo wa kutumia 400000 kwa mwezi, inamaana hata uwezo wa kuimarisha ulinzi wake upo hasa kwa vibaka
Nashauri nunua mbwa ( Trained) hata wawili kukabiliana na vibaka, lakini pia kupitia bughudha ya vibaka kaa na serikali ya mtaa wakupitishie kibali ununua siraha.
Kuhusu galama za usafiri, nunua pikipik TV's Lita 2 kwenda na kurudi kwa umbali huo.
Pia usiuze Wala kupangisha zaidi buni mradi mdogo mdogo Kama kufuga kuku ili wakusupport kwenye running cost za pikipiki hasa mafuta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona wahindi hawajuti japo wanakaa maghorofani toka nimekuja mjini miaka ya mwishoni mwa 1980s?
Usiwaige hao watanzania wenye asili ya kiasia...tukio la kutaifishwa nyumba zao mwaka 1967 Hadi 1970 liliwaumiza kisaikolojia...hawana hamu ya kujenga nyumba Tena..halafu baadhi yao wana pasipoti mbili...
 
Back
Top Bottom