Najuta kuhamia kwangu Kerege

Hivi unaanzaje kujenga maeneo kama hayo then unategemea kuja mjini kazini!? Only mjinga asiejitambua..
Kujenga maeneo hayo labda wewe unataka ufugaji na umejiajiri mwenyewe sio ajira ya kuajiriwa utafeli sana
 
Mkuu nikupongeze kwa uamuzi wa kujenga na kuhamia kwako. Hongera sana.

Mkuu shida moja mentality yako umei tune kwenye kuepuka kodi ya nyumba which is minor factor unapotathini suala la kukaa kwako au kupanga.

Kukaa kwako ni zaidi ya kukwepa kodi, yaani ukikaa nyumba ya kupanga kuna uhuru unaukosa kabisa, imagine hata unataka kuning'iniza Flat TV yako ukutani unamwaza mwenye nyumba akisikia unafanya drilling kuweka ile stand ya TV ukutani (huu ni mfano mdogo sana) majumba ya kupanga yana vingi sana mkuu kubali kuishi kwako.

Kuhusu gharama naomba nikushauri jipinde uimarishe ulinzi, kujenga ukuta, install electic fence, funga camera japo haizui wezi ila inapunguza ushawishi wa wezi. Ni gharama lakini ni jambo ambalo litasaidia kuona uko sehemu salama.

Lkn kama una eneo kubwa hebu tenga eneo fuga hata kuku chotara ambao watapunguza gharama za maisha kidogo lkn kama kuna eneo krb hapo hebu wekeza mifugo kama biashara baadar utaona maisha yanasonga kabisa na uta enjoy maisha ya Kerege zaidi ya maisha yalivyokuwa Sinza.

Binafsi napenda kuishi sehemu mbali na mji yaani asubuhi unasikia tu sauti za ndege.
 
Watanzania huwa Hatupigi hesabu za mafuta na muda tunaopoteza ndo maana tuko radhi tukajenge mbali kuliko kupanga. Tukipiga hesabu bora kupanga karibu ma shughuli zako kuliko kuishi mbali hata kama ni kwako
Kweli kabisa usemayo, mfano kama yeye anatumia usafiri wake na mahitaji yake kaini yanafikia Laki 4 wakati akitafuta madalali kama Magomeni ama Ilala ambapo sio mabli na posta anapata nyumba ya kupanga kwa laki 2 na nusu hadi tatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…