Najuta kuhamia kwangu Kerege

hiyo nyumba picha zaidi zipo wapi nikuletee mteja kama bado unauza, ama nipe link ya zoom ulikopost nikacheki
 
Investment ya nyumba siielewi. Labda wajuvi watusaidie. Ukiacha maeneo premium kama Masaki, Obay, Mikocheni na Mbezi (ambako madon wa mji walishagawana) wengine huku kwetu ni kuumizana tuu. Unajenga nyumba standard ya 200M. Halafu uipangishe kwa laki tano....hiyo hesabu kwangu ni ngumu. Mtu unakuta kajipinda na ghorofa lake la maana Bunju au Mapinga..ukiangalia pesa ya kodi kwa mwezi unachoka. Hapo hujaweka wear and tear/uchakavu nk...

Hiyo biashara hapana ngoja tuwaachie wenyewe. Nyumba ambayo haiwezi kuniingizia 1M, minimum, kwa mwezi naona bado ni changamoto kubwa...
 
Hiyo nyumba tafuta mtu wa kukaa akulindie. Wewe panga mjini karibu na kazini kwako au karibu na shule ya watoto kama unao. Ikifika weekend kama ijumaa jioni hivi unaenda kwako unakaa mpaka jpili jioni unarudi town. Huko utakaa mambo yakibadilika au ukishastaafu.
Hongera kwa kujenga nyumba!
 
Kerege mmekumbukwa na Bandari ya Bagamoyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…