Najuta kuhamia kwangu Kerege

Sawa lakini kerege kwenda posta ni karibu kilomet 40 au 50 sasa unafanya kazi Posta kwenda nakurudi km 70 au 80 bora hiyo dodoma km 18 tu na foleni hakuna
 
Ni wazo zuri lakini atapumzika saa ngapi jamani kama na weekend yuko barabarani.
 
Wewe shukuru umejenga kibanda chako hata kama hukuwa umejipanga usicheze na maisha ya kupanga ndugu
 
Uza we mimi mbona niliuza yangu toa ngoja nikamtoa mtu pale flat za ilala kwa 4m tu sasa hv foleni siijui hata nn kudadadeki kilichobakia natafuta nyumba za mjini hasa tabata walizoshindwa kulipa madeni yao benki niwalalie dadadeki zao
 
Jana nilikwenda huko Kinzudi asee kuna watu wanaishi mbali. Nikawaza mtu kama hana gari inakuwaje?
 
Hahahahahhhha nimeipenda hii... Hii ni formula nzuri kwenye maisha wengi wanaiogopa, usipunguze matumizi eti hali ngumu bali ongeza mbio uongeze kipato kucover matumizi yake..

Unawaza kama mm....ingawa kuna changamoto sana kwenye usimamizi...!unaweza kuwa daily unakimbizana tu...eish !
 
Sawa lakini kerege kwenda posta ni karibu kilomet 40 au 50 sasa unafanya kazi Posta kwenda nakurudi km 70 au 80 bora hiyo dodoma km 18 tu na foleni hakuna
hiyo sehemu inaitwa Mbalawala, Mpamatwa Mbande nk hakuna barabara ni njia za Baiskeli na pikipiki hatutarajii Mwendokasi ni mapori ya kukata mkaa, ndipo wazi km huko Kerege
Ardhi yote huku imepimwa ni kuanzia 8.5m kwa makazi, ukitaka mashamba ukajipimie na Balozi ndio hayo ya 3m au 1.3m
Sasa Kerege nauli haivuki 2,000. kerege Baobao 500/ Baobao naona mpaka sokoni anapata ya Kawe mpaka Stesheni au mwendokasi 650/ Mwenge stesheni, Mm nimesoma Temeke kwenda Ubungo lazima tupitie Posta kubadili Chai maharage au UDA, Leo Posta hadi Kibaha Mwendokasi bure, hata Posta Bagamoyo rd haitachelewa
avumilie tu asiiachie ardhi akapange Manzese, lkn akishakuwa mstaafu atapakumbuka kina Assad wanalima Bamia Ardhi haimtupi mtu
 
Service ya gari si unaijua mzee..hiyo 14 haitaweza kuservice gari..otherwise labda kama umeamua tu kuwasaidia watu
 
Nimegundua wengi waliomshaul ni wanafunzi wa chuo wanaopenda maisha ya kwenye video, dume zima ukaona kerege mbali na watu wanakaa moro wanafanya kazi dar nimewazalau kwelikweli
Dar moro masaa mawili hadi matatu kwa private ..lakini Posta Chanika inaweza chukua hadi saa tano kutegemeana na barabara ilivyo hiyo siku. So sijaelewa point yako unaongelea umbali au matumizi ya muda barabarani.
 
Unaposema nunua kisha usubiri, unakuwa unamsubiria nani au unasubiri nini?!

Maisha yako binafsi, lakini unawasubiri wengine?!

Hao unao wasubiria wakifika mnaishi nao kwenye nyumba zao, mnakula pamoja au mnafanya kazi pamoja?!

Sijaelewa unakuwa unamgonja nani na ili iweje?
 
Kumbe wapo wengi nina ndugu yangu kajenga huko naye kakimbia amerudi mjini
Yaan ukijenga huko ukiwa kijana ni lazima utarudi tu mjini!

Huyo sista angu, nilijisemea moyoni tu hivi huyu du, atapaweza kweli[emoji16]

Maana mwanzo anahamia mbwembwe kibao, miezi 6 kageuza, yuko K' nyama, nyumba kaachia mlinzi[emoji87]
 
Mmh [emoji849]

Ikawaje sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…