Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Huyu huwa anafurahisha genge tu japo sometime thread zake zina mantiki. Akiona thread inapoa anapost sentensi moja ya kuvutia Watu wanatiririka. Na ni maarufu wa kufufua thread zilizokufa
Haaahaaa[emoji16]nilimstukia
 
NJE YA MADA:

MAPINGA, KEREGE, ZINGA, KIROMO, KITOPENI, UKUNI (MAENEO YALIYOPO BARABARA KUU YA DAR - BAGAMOYO)
NI MAENEO AMBAYO YANAONEKANA KEKI SANA KWA MTU KUMILIKI ARDHI,
NA
HIVYO WATU WENGI KUTOKA DAR ES SALAAM NA MAENEO MENGINE KUMIMINIKA BAGAMOYO KWA WINGI KWENDA KUNUNUA ARDHI (VIWANJA & MASHAMBA).

NOTION HIYO IMEIBUA WIMBI KUBWA LA MATAPELI (WANAOJIITA/KUJIFANYA MADALALI) NA KUPELEKEA WATU WENGI KUTAPELIWA NA MADALALI HUKO,
AMA KWA KUUZIWA MAENEO YASIYOWAHUSU AU KUWAUZIA MAENEO YENYE MIGOGORO,
YAANI UNAKUTA ENEO MOJA WAMEUZIWA WATU 6 TOFAUTI,
NA WOTE WANAZO NYARAKA-

SASA HAPO ZINAANZA KESI MAHAKAMANI SASA-
THE STRONGEST DO SURVIVE,
THE WEAKEST END UP TO PERISH.

UNAPOENDA KUNUNUA ARDHI BAGAMOYO,
KUWA MAKINI SANA-
SANA NA SANA, NA TENA ZAIDI YA SANA!!!
WEKA AKILI YAKO MBELE, KISHA PESA NYUMA,
NA SIO PESA YAKO MBELE, KISHA AKILI NYUMA.

(Kama umemaindi herufi kubwa, unaweza sema nikupe mwongozo).
Kama kuna mtu anauza kiwanja chake Mapinga kama mmiliki, na serikali ya mtaa inamtambua hivyo, jee unashauri tahadhari gani kwenye hii scenario? Kiwanja kimepimwa na kipo kwenye mchakato wa kupewa title.
 
Mkuu vumilia zamani hata Kimara palikuwa shamba na mbali na mji.Tulikuwa tunapishana na viboko na nguruwe.
Usiuze hiyo nyumba utajuta baadae cha kufanya tafuta chumba panga karibu na kazini kwako.Hiyo nyumba ya Kerege tafuta mwenyeji mswahili wa huko muache akae hata bure akulindie mji.
Mimi sijuti kununua viwanja Kimara mwaka 1969 sasa hivi mimi ni kamfalme kadogo
Maendeleo ya majengo na miundo mbinu yanamfuata mtu sio kinyume chake
Ulinunua kiwanja 1969? Well well...
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.

View attachment 1259979
Kaka usijute wala nini, yakupita tu, wenzako tupo BunjuB, tulishavamiwa tukagongwa sana sana, ila tumejaa tumejipanga na ulinzi shirikishi na nini sasa tupo kama oysterbay...
Mafuta ni nini kama unakaa kwako?!
Achana na Sinza, yale ni maisha ya ujana tu kaka...
Jipangeni mtaani, umoja ni nguvu amini usiamini...
 
Kaka usijute wala nini, yakupita tu, wenzako tupo BunjuB, tulishavamiwa tukagongwa sana sana, ila tumejaa tumejipanga na ulinzi shirikishi na nini sasa tupo kama oysterbay...
Mafuta ni nini kama unakaa kwako?!
Achana na Sinza, yale ni maisha ya ujana tu kaka...
Jipangeni mtaani, umoja ni nguvu amini usiamini...
Poa. But in the mean time wacha nijibanze kwanza kinondoni
 
Sisi hatusemi ule umri wa balehe...namanisha umri ule umemaliza chuo unaweza oa! Sio utoke form 4 uoe![emoji39][emoji39][emoji39]
Kwani umri wa kuoa kidume ni upi! Mane bhana, hata wewe nakuzaa ukikaa vibaya [emoji39][emoji39][emoji39]
 
Mane kwani kila mtu anafika chuo? Wengine wanamaliza la saba wanaoa
Mwambie, tena kama ningeishia la saba ningekuwa na watoto wapo chuo na wengine washaolewa na kuoa. Hizi formal education system zimeharibu mfumo wa maisha ya mwafrika.
 
Back
Top Bottom