Najuta kujenga kibanda changu uswahilini. Mswahili ni mtu duni sana

Nakumbuka wakat nmpanga iringa nilikuwa na tabia ya kuweka biskut za chocolate na juice kweny trei ya vyombo kwa juu

Sasa siku ya kwanza kale katoto ka jiran kameingia kamenikuta nacheki movie nkainuka na kumpa biskut ya chocolate kikasepa

Sasa imepita siku 2 natoka kuoga asubh nisepe....mlango nliegesha tu....kale katoto kakafungua(bila salam) moja kwa moja pale nnapowekaga biskut....!!

Nilikageukia nkampa kofi mpk majiran walisikia....!!

Mpaka nahama hajaingia teena ndan
 
Safi sana
 
Nilichogundua wewe ni (Mchumi ) Ila ungeweza hata kumjumulisha kwenye bajeti yako ya msosi lakini kwasababu huna bajeti naye,; Nikushauri weka uzio hata wa mabati chakavu funga kabisa ubakize mlango ambao utakuwa unaufunga mida ya msosi!

pia zingatia Kama Watoto wako wanapenda kwa watu Basi na kwako watakuja wa watu, Zuia watoto wako kuzurula!

Lakini mwisho wa siku Kero ni sehemu ya jamii! njia nyingine ya kuondoa kero Ni kuivumilia
 
Dawa ni kumpa laivu Tu. .. Mimi Huyo mtoto SASA hivi akija nyumbani hata kama chakula kimeiva nakwambia nenda ukale Kwa mama. Sitaki kabisa mazoea na hawa watu wanakera Sana.
Kwamba akale kwa mama[emoji23]
 
Kwanza ni kosa kumlisha mtoto wa mtu kwako bila uwepo wa wazazi wake. Iwe ulaya, au uswahilini, usiwe unapenda kulisha watoto wa watu.

Muda wa msosi ukikaribia kasindikize kwao, na kasikuletee mazoea hapo ya kuwabana watoto wako wasienjoy mema ya baba yao......
 
Sina MKE bro Mimi ni msela. Hawa watoto kila mtu na mama Yao. Sipendi tu watoto wangu kufanyiwa kero. Toto linakuja na mikono yake michafu huko halijaogeshwa linanuka mikojo linakuja kusumbua watoto wangu.
too harsh mtoto wa mwenzio kumwita "litoto" ila hata mimi sipendagi kero.
 
Mbona ww ndo unaonekana mswahili zaidi? Mtu mwenye ustaarabu hawez mpiga mtoto wa jirani kisa chakula. Ungeweza mueleza mamake kistaarabu au ungeweza mpa chakula mpaka mpaka maamake ajistukie, mtoto ni innocent, wazyngu wanapima ustaarabu wa mtu namna unavyoweza kudeal na watoto na wanyama, mm kwangu kitu ambacho si deal nacho kabisaa ni chakula na namuelezaga wife fanya uchoyo/roho mbaya kwenyw vingine vyovyotw ila si chakula.
 
Na ww unaonekana mswahili huna haja ya kupiga vijembe kupitia muziki ili wakuelewe.
mm kama ningekuwa ww. Na nina hela huyo mtoto wa jirani angekuwa anakuta nimemuwekea mabakuli ya nyama.
Hujaelewa mkuu sipigi vijembe. Nasikiliza muziki mgumu ili wajue Mimi ni MTU WA Aina gani. Unajua Aina ya muziki unao usikiliza unaweza kukutambulisha wewe NI MTU WA Aina gani. Mwanaume ukiwa unasikiliza taarabu watu wata amini wewe NI shoga. Ukiwa unasikiliza blues utaonekana romantic. Gospel Mtakatifu Mathayo na Hip-hop mhuni msela. Mimi ninacho kifanya nasikiliza Ngoma ngumu za hip hop Kwa Sana ili wajue Mimi mhuni. Mwanzoni nilikuwa nasikiliza Sana gospel so wakawa wananiona sijui Emmanuel Mbasha.
 
Wewe hujaelewa mkuu. Halafu hayo maisha ya kijamaa ndio yanawaponza watanzania wengi.

Nimesema kama Wana shida ya chakula waje wanikope niwape hela wapike nyumbani kwao sio kuja kuwasumbua watoto wangu
 
Naona tatizo sio chakula, tatizo ni huyo mtoto kulia lia kuwa msumbufu , akiwekewa chakula chake bado analilia cha wenzio

Sijaruhusu huo ujinga Yani mtoto wa jirani aje nyumbani kwangu halafu awekewe chakula chake MWENYEWE? Akipata madhara ? Utaambiwa umemuwekea sumu kwenye chakula. Waswahili watu WA hovyo sana mkuu Bora wakuone Una roho mbaya kuliko kushirikiana nao kwenye baadhi ya mambo
 
Nime "note" kitu;

1. Biblia inasema mwenye nacho huongezewa hivyo unastahili sababu nawe una USWAHILI...utawezaje kutukana hivyo?
Unashindwaje kumwita mamake ukamweleza lwa hekima na sio kwa shari kihivyo?
2. Jenga ukuta hii ni sindano ya moto.
Unahakikisha mageti yamefungea muda wote isipokuwa kwa ruhusa maalum.
3. Mkeo naye mswahili?
Mswahili hutembelewa na waswahili wenzie
 
The way unavyo jiexpress hapa it's obviously wewe ni mtu fulani selfish sana (samahani ni maoni yangu tu) ukizingatia huyo ni mtoto hata bado hajakuwa na uwezo wa kutambua kama ana kukwaza au laa sasa kitendo cha wewe kuanza kumwita alien sijui na majina mengine ya ajabu sio vizuri kabisa.

Watu wenye maisha unayotaka wapo washajizungushia fensi na mageti makubwa yenye walinzi. Pia hizi case ndogo ndogo za ujirani waachie wakina mama wenyewe watamalizana wewe weka tu bajeti ya kutosha. Na kuwakataza watoto wako wasijichanganye na watoto wengine sio dawa kabisa ya kuzuia wasiwe na tabia mbaya interaction between children is inevitable sababu hata wanavyo soma shule bado watakutana na watoto wengine. Zipo njia za kuwafunza watoto tabia njema lakini sio kwa style hiyo yako tena hapo wewe ndio kabisa unawaharibu.
 
Sawa mkuu nimekuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…