Najuta kuoa Single mother, kila nikimtazama huyu mtoto wake Moyo wangu Unaumia kwa machungu makali. Nahitaji msaada

Kichwa Cha habari kimejieleza kabsa Mkuu labda kama hujasoma, umekimbilia kutoa comment.

Kuhusu upande wazazi. Niwe Mkweli wazazi wangu hawakuridhia nioe huyu mwanamke ni ukaidi wangu tu ndiyo umepelekea yote haya.
Siyo kwamba sikusoma kichwa, iko hivii?

Kwa vijana wa siku hizi, kile kitendo cha kuishi na mwanamke kinyumba wanaita 'kuoa' ndiyo maana nikatupia maswali yangu ya dodoso ambayo kiuhalisia hauhayajibu itakiwavyo.
 
Hali yako ya kiuchumi ikoje?
 
Kama mwanaume anaweza kucontrol mambo na ana akili za kupitiliza iweje huyu mwenzenu aoe mwanamke mwenye mtoto halafu imepita mwaka tu anataka kubadili maamuzi bila sababu yoyote ya msingi. Hizi akili ni za kimama kabisa
 
Sasa mkuu hoja yako ni nzuri Ila Sasa mimi nawaza kitu kimoja hapo je bibi wa Huyu akifariki mtoto ataenda wapi?

2.mtoto Huyu akienda kwa baba ake itakuaje? Endapo mama wa jambo yule hayo penda mtoto wa mumeweπŸ€”
 
Single mama ni binadamu aliyeteleza tu...

Wengine hawatelezi ila ni ujeuri wao.

Kama alibakwa tena kwa kufosiwa, hapo ndio tunamuweka kwenye kipengele cha Kuteleza.

Kama mtu kafanya kwa ridhaa yake na alifurahia kandanda, hapo hauwezi kusema aliteleza.
 
Acha roho mbaya, wewe wakwako si anakelewa na baba wakufikia! Acha roho mbaya, utakuwa mtu wa kule wana roho mbaya kweli!
 
Mkuu najilazimisha sana kumpenda huyu mtoto lakini nafsi yangu imegoma kabsa. Na sijui nifanyeje.
Usiwe mbinafsi mkuu,
Ingekuwa mama yake ndio msumbufu, anawasiliana vibaya na mzazi mwenzake ningesema una haki ya kuongea.

Lea, hayo ndio majukumu yako, omba Mungu akuzalie pia ili maisha yasonge. Watoto ni baraka na hawana dhambi yoyote.
 
Akiwa mkubwa, atashirikiana na mama yake kukupiga
Acha kumtisha mwinzio,πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ huyo anaona wivu tu kuona yule mtoto katokea pale pale inamaana kuna mtu naye alikuwa anapita πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Mpende huyo mtoto, utaziona baraka za Mungu...

Single mama ni binadamu aliyeteleza tu...

Tuache kuhukumu, Mungu anasamehe
Uongo, kuna jirangu Kaolewa na Mzungu huyo mzungu kazaa nae watoto wawili kabla ya kuolewa na Mzungu huyu Mwanamke alishazalishwa mtoto mmoja kwahiyo jumla ana watoto watatu wawili wa mxungu, Sasa huyu Mzungu analea watoto wake tu aliowazaa huyu Mwingine hana habari nae, Mzungu akirudi kwa Ulaya anaondoka na watoto wake wa kuwazaa huyu mwingine ana muacha na Mama yake, tani ata akitaka kwenda kutembea anachukua watoto wake tu na kusomesha ada analipa za watoto wake wawili huyu mwingine ada analipwa na Mama yake.
 
Sambaza upendo mkuu.......usimkatie tamaa kiumbe kiitwacho binadamu as long as hakijakuja kwako kwa bahati mabaya.

Sambaza upendo kila kiumbe huja na riziki zake....
 
Ushauri namba moja ndiyo mzuri, Mimi mwenyewe Dada yangu alizalishwa nje ya ndoa akamleta mtoto wake Nyumbani Mzee wangu akawa ana mtimua mtoto ana mwambia Mama huyo mtoto sitaki kumuona Nyumbani mpelekeni kwao hapa siyo kwao. Wanaume tunapenda kulea watoto Yatima na siyo mitoto ya Mke.
 
Au hakumwambia mapema kama anamtoto kabla.
 
Wewe hustahili ushauri zaidi ya makofi ye Kelbu.

Unless otherwise huu uzi wako ni chai.

Mkiambiwa msioe single maza hamsikiagi.
 
Ila mnapenda wake zenu walee watoto mliozaa huko nje nakumleta hapo nyumbani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…