Unachoshindwa kuelewa wewe na wenzako wenye mawazo kama yako ni kwamba...Kwahyo akiwa sio mwanae ndio kinabadilika kipi
Sa akiwa sio mtoto wake ni vibaya kumsaidia kukua?
Diamond alimsaidia harmonize je Mond alikua baba wa Harmo?
Ronaldo alisaidiwa pasi ya mwisho na rafiki yake ambae alikua na nafasi ya kufunga ili aende sporting cp, je yule rafiki alikua baba wa Ronaldo?
Baloteli kalelewa na wazee wa italia je walikua wazazi wa kumzaa wale?
Hivo ni mifano baadhi kati ya mingi ya watu waliofanikiwa kutokana na watu baki na baba zao wakiwepo.
Sometimes fanya wema tu haijalishi utarudishiwa nini kikubwa ushafanya.
Unapoanza kuishi na huyo single mother suala la kumpa mahitaji huyo mtoto wake itafika muda litakuwa sio msaada tena bali itakuwa ni wajibu wako kwa kipindi chote utakachokuwa unaishi na huyo mwanamke...
...Na pia kwa sababu ni wajibu wako atakuwa na ile entitlement ya kukulalamikia pale anapoona utimizi wajibu wako kwa usahihi na kasoro yoyote ile itakayojitokeza katika kuwajibika kwako itatafsiri kwamba wewe humpendi mtoto wake, labda nikupe mfano hili uelewe vizuri hii point hapa.
wewe unaweza ukampeleka huyo mtoto wa single mother private school ambayo labda ada kwa mwaka ni 4m, lakini yeye huyo mwanamke akikuangalia kifedha una uwezo wa kumsomesha mwanae hata shule zenye ada ya 10m. Kwa hiyo akilini mwaka atakuwa anajiuliza kwanin umempeleka mtoto wake shule ya school fee ya 4m na wakati una uwezo wa kumpeleka kwenye shule nzuri zaidi ambayo ada yake ni 10m tu?
Kwa hiyo akilini mwaka atahitimisha kuwa wewe humpendi mwanae ndio maana umempeleka kwenye shule ya ada nafuu ya 4m na endapo kama angekuwa ni mtoto wako wa damu basi lazima ungempeleka kwenye hiyo shule ya 10m.
Kwa hiyo licha ya wewe kumsaidia Kusomeshea mtoto wake kwenye shule ya gharama bado hawezi kurudhika na wewe na huo msaada wako hautokuwa na maana kwa sababu tu haujafanya to the maximum level kulingana na kipato chako na hii yote ni kwa sababu wanawake kiasili huwa wana entitlement mentality ukiwafanyia jambo lolote lile kama msaada inafika stage wanaona ni haki yao ya msingi, na ukisitisha wanakuona una roho mbaya.
Naona umetoa mpaka mifano ya akina Daiamond na Harmonize sijui Ronaldo na Rafiki yake, mara Baloteli na wazazi wake walio mu adopt... asiee kijana hii mifano yako yote haina relavance yoyote na hii mada, kwa ufupi tu umetoa mifano mfu isiyofaa kabisa kwenye hii mada.