Siwezi vumilia mi ni mtu wa kujirusha yeye anakata tushinde ndani tu wkend zote
mwanagu, ulitaka uingie kwenye ndoa na tabia za kujirusha????
Kumbuka ndoa ni heshima, na Adabu, kama ulikuwa unataka kujirusha kwa nini ulikubali kuolewa?
Biblia inasema mwanamke mwenye Adabu ni taji kichwani mwa mumewe.
Wacha utoto. Badilika wacha tabia za kuambatana na watu wasio na hekima.
Msikilize mume wako. Maana mume ni kichwa cha nyumba, sikio Halizidi kichwa.
Wengi wenu wameachika kwa sababu za kudhani ndoa ni kama kilabu cha mbege.
Usiwaingize mashosti zako katika ndoa yako, utaivunja kwa mikono yako mwenyewe.
Usidhani ni ufahari kuachana kumbuka mwanaume hana cha kupoteza.
Bali kwa mwanamke ni istoria mbaya, kwamba umeachwa.
Tulia tena uwe na Adabu, jiheshimu heshimu ndoa yako.
Tena mimi nampongeza huyo mumeo maana anakupenda na hapendi kuona huna Unakuwa mcharuko.
Ni mwanaume gani anashinda wikiendi nyumbani na mkewe?
Kama hujui kaulize wenzio Ambao mwazo wa mwaka mwisho wa mwaka wanakuja nyumbani usiku wa manane.
Tulia binti acha kuishi kwa kuiga iga tabia zisizo na maana kwenye ndoa yako wewe ni mke wa mtu sasa.
wambie hata mashoga zako wanao kutia kiwewe mpaka unataka kuachika ili jujirushe kwamba sasa wewe ni MRS.