Najuta kuwa na huyu mwanaume katika maisha yangu. Ameharibu ndoto zangu, najiona si binadamu tena

Najuta kuwa na huyu mwanaume katika maisha yangu. Ameharibu ndoto zangu, najiona si binadamu tena

Sasa unakomaa nini hapo? Unachokitafuta kwa hyo mwanaume sasa hivi ni kuonewa huruma. Achana na mtu wa mwenyewe dada
 
Unakosea unapowaza kwamba Lazima akuoe kwasababu mmezaa, usilazimishe hiyo ndoa Unaweza kuja kuishia kwenye magunia ya mkaa, au manyanyaso makubwa kuliko hayo.
 
Pole sana inabidi ukubali matokeo hamna sababu ya kuumiza moyo wako huyo ni binadamu kama wewe na siyo Mungu wako, songa mbele endelea na masomo Mungu akusaidie.
 
Eti akakuzalisha au ulitega mimba, dah wanawake msipojielewa daily mtalia kutwa kufuraisha wanaume badala ya kutimiza ndoto zenu
 
Wewe embu acha hizo, soma nakuambia soma nakuambia soma endelea na degree yako, na ukimaliza degree specialise kwenye fani yako kuwa proffessional

Hakikisha una life time qualification, hakikisha jina lako linaanza na tittle kama vile "wakili msomi Ma BOBO " au "engineer Ma BOBO " .

Achana na huyo mburukenge kwa sasa, hasira hamishia kwenye kutengeneza maisha yako.

Dogo tengeneza career yako itakulinda na kukusaidia.

Kwa sasa huyo mburukenge msahau kabisa muhimu ahudumie mwanae tu, wakati wako ukifika utapata bonge la bwana na utafurahia mapenzi na maisha kwa ujumla.
Neno la wiki
 
Muamini Mungu katika maisha yako, nilikuwa na mwanaume ambaye tulipendana sana tukaahidina mambo
Endelea kuteseka mkuu...
It's a cold world kutafuta sympathy

Unazaa hujaolewa unategemea Nini..huna wakubwa wakuwaheshimu au uliwaona mazwazwa wwkat unabebeshwa mimba..Yani Kuna wanawwke kama mlijambwa hamna ndugu wakusikiliza makwenu..ukipata mwanaume bas we ndo alpha na omega..shenz
 
Hebu kwanza badilisha jinsi unavyofikiria.
Tatizo liko jinsi unavyochukulia mambo .

1.kukuzalisha sio kwamba kakuharibia maisha.(weng wamezalishwa hawana hata hiyo certificate wala mume na maisha yanaenda).

2.Ameshasema mlee mtoto, na pia sio mwanaume wako wa ndoa, kwanini unganganie? Na kuteseka?.
Alee mtoto na ww pambana na maisha yako umalize chuo, utafute kazi uje ukae na mwanao.

3. Uko huru kuwa na mwanaume mwingine.
Maisha ndio haya haya, utakufa na stress bila sababu za msingi.

Hebu fikiria sahihi.
 
Pole sana ndugu! Hata hivo mateso na furaha yako vyote viko mikononi mwako, ukiamua kujitesa ni wewe kuendelea kumuwaza huyo mwanaume ambaye tayari kisha chukua time zake! Lakini pia ukiamua kujipa furaha ni wewe kufanya umsahau na kumfagia kabisa moyoni mwako, fanya kama vile umepoteza pesa mchangani na umetafuta bila mafanikio!

So muache aende zake, nawe shika time zako! Kwa vile unae wa kukutunzia mtoto basi wewe shusha nguvu zote kwenye kitabu, ukifanikiwa hapo mambo yote yatanyooka na huyo X wako hutokujamkumbuka tena! Endelea kumtegemea kumtegemea Mungu nasi twazidi kukuombea!
 
Muamini Mungu katika maisha yako, nilikuwa na mwanaume ambaye tulipendana sana tukaahidina mambo mengi sana ya kufanya katika maisha mwezangu ikaonekana ana elimu ya juu yaani PHD Mimi certificate, nilivyoona ndugu zake wanaongea ongea juu ya elimu yangu kuwa ni ndogo siendani na mtoto wao nikawaza
Kosa kubwa sio yeye.. Ni wewe kukubali kuzini kabla ya ndoa. Unatumia muda mwingi kulaumu badala ya kupiga goti na kutubu. Unamtaja taja sana Mungu wakati huoneshi majuto yeyote ya kosa lako. Mbele ya Mungu huwa hakuna dhambi uliyotenda kwa sababu ya mwingine. Melendez ya Mungu ni kutibu wewe peke yako kwa majuto kuwa Mungu nilikukosea kwa kutozitii amri na maagizo yako.. Mpaka nikajikuta nimeangukia huku utumwani niliko kwa sababu ya dhambi zangu.

Ndipo utapata msamaha wa kweli na Mwenyezi Mungu atakusaidia kwa haraka.. Kwanza kwa kukupa Amani kubwa moyoni.. Pili njia na alternative ya kusonga mbele.. Baadaye utapata the right person wa maisha.. Lakini kwa kuheshimu amri zake sio kwa uzinzi tena.

Wanawake wengi wanapenda kusema fulani ameniharibia maisha bila kutafakari kwa kina nafasi yake katika kuharibika kwa hayo maisha.. Hasa kiimani na kimaadili. Kama ungezingatia.. Imani yako.. Mafunzo.. Maadili.. Tamaduni zinazofuatwa au taratibu zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuoa ungeharibiwaje maisha.

Tubu jinyenyekeze mbele ya Muumba wako uone milango itakavyo funguka. Ila ukibaki na fikra zako hizo za kufikiria yeye tuu ndio kakuharibia utateseka mpaka kufa. Funguo za Amani na furaha ya maisha yako unazo mwenyewe. Ni uamuzi tuu.
 
Kwenye mada kama hizi ndio pahala pazuri pa kujua iwapo jf kuna wabeijing.Maana kwenye mada kama hizi huwa wanachomoza kwa wingi kama uyoga kipindi cha mvua
 
Uzi closed
 
Komaa na maisha yako. Uvumilivu ukikushinda mroge asifanikiwe huyo jamaa. Mroge asidindishe
 
Ila kuna mda unaweza kuwa mjinga bila kujitambua kuvumila upumbavu nawe pia n mpumbavu tu
 
Story yako haijakamilika.Tueleze ulimkosea nini? Hakuna mwanaume anapenda kuona mtoto wake akipata malezi bila wazazi wote kuwa pamoja.Lazima utakuwa na kasoro kubwa kitabia.Jichunguze
 
Back
Top Bottom