Najuta kuwekeza kwenye kiwanja na nyumba ya mwanamke

Najuta kuwekeza kwenye kiwanja na nyumba ya mwanamke

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2019
Posts
442
Reaction score
1,655
Wana MMU,

Naandika huu uzi kwa masikitiko na kujuta bora ile pesa ningenywea tu bia na kula kitimoto.

Nina mke na watoto, mke alikopa hela bank na kazini kwao akanunua uwanja. Ushauri huu nilimpa mimi

Nikasimamia ujenzi nyumba ikasimama ingawa kuna vitu vilikuwa havijakamilika nikaanza kuingia gharama kumalizia nyumba.

Kipato changu cha kuunga unga ila kwa kutambua nyumba ni ya familia tuna watoto na ndoa tumefunga nikaona niendeleze ukarabati.

Sasa bwana umetokea mgogoro mdogo mimi na mke wangu kanitamkia hapa sijachangia chochote kodi yote anakula yeye.

Basi nimeamua nianze mdogo mdogo kujitoa kwenye hii nyumba.

Mchango wangu hajauthamini kabisa mwanamke amekua mbinafsi ghafla sana.

Wakuu tuwe makini kuwekeza hela na muda wako kwenye mali ya mwanamke ni kujichimbia kaburi.

KATAA NDOA
NDOA NI UTAPELI
 
Mkuu unazira mali yako kabisa.......[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu kiwanja aliandika jina lake maana yeye ndo alikopa hela ya kununua mimi nimechangia kwenye ujenzi lakini leo hii ananiambia sijachangia chochote hela yote ya kodi za wapangaji anakula pekeake so sitaki kuforce umiliki ila inaniuma tu pesa zangu nlizotupa hapa bora ningeenda kutafuta kiwanja changu hata kijijini huko
 
Back
Top Bottom