Najuta kwanini niliuza gari yangu

chemri

New Member
Joined
Jan 19, 2019
Posts
3
Reaction score
163
Nilikua na kagari kangu IST kalikua kananisaidia sana hapa mjini (DSM) mambo yangu yalikua safi kidogo, visafari vidogo vidogo na kukutana na warembo ilikua simple sana.

Sasa nikajikoroga kuitamani MARK X, Alikuwanayo rafiki angu, nilimuona anafaidi sana
Kwanini mimi niwe na IST halafu yeye MARK X, nikaona bora niiuze gari yangu ili niongezee pesa na mimi nichukue Mark X

Kilichotokea nikafanikisawa kuiuza gar yangu na hapo nikawa nimekaribisha matatizo. Mpaka sasa sijafanikiwa kununua hiyo MARK X niliyoitamani na sijui nitainunua lini, pesa yenyewe naona giza kwani nimeitafuna.

Naandika huu uzi kwa uchungu sana ninapojiona nipo standi ya mwendokasi na kila gari inayokuja imejaa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani si wewe tu yamewatokea wengi hata kuuza nyumba kwa ahadi ya utajiri au kuliwa fedha ya pension yote. Pole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…