Najuta kwanini niliuza gari yangu

Pole sana, wewe umeenda kinyume na utaratibu lazima ukwame. Ulitakiwa utafute hela ya kuagiza hio Mark X yaani CiF, halafu ukishainunua iko kwenye meli unatangaza kuuza hio IST, gari yako ikifika bongo (baada ya mwezi au miezi miwili) unakuwa ushauza hio ist na kupata hela ya ushuru.
 
Ahahahahah.. Jamaa post yako inafundisha huku inaburudisha. Pole sana.
Anza kujipanga upya.
 

Mkuu dont lose hope. Cha kufanya njoo Zenji na hizo hela zako zilobaki utapata gari Mark X au GX100 au Verossa. Hizi gari zimeshuka bei hapa milioni 4 au 5 unapata gari nzuri tu yenye kuhitaji marekebisho madogo madogo na ambayo unaweza kuileta Dar bila gharama kubwa.

Yuko jamaa juzi tu kanunua nafikiri mpaka ikifika Dar itakua imegharimu kama mil 6 tu. Ni pm no. Yk nikutumie picha
 
Tatizo wabongo tunapenda sifa sana, Mark X hapa mjini unafanyia nini? ENgine kubwa, matumizi ya mafuta makubwa, bei yake kubwa. Unaponunua gari cha kwanza jiulize kwa nini unanunua gari, au hii gari itanisaidia kwa shughuli zipi? 1. Movement kwenda ofisini na mishe za hapa town gari IST ilitosha kabisa. 2. Kama una shughuli kubwa kubwa za pori pori kidogo kama shamba tafuta gari kubwa lenye 4WD.

Pole sana sifa zimekuponza. Mimi nitafia na corolla yangu cc 1500
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…