Najuta kwanini niliuza gari yangu

Najuta kwanini niliuza gari yangu

Nilikua na kagari kangu IST kalikua kananisaidia sana hapa mjini (DSM) mambo yangu yalikua safi kidogo,, visafari vidogo vidogo na kukutana na warembo ilikua simple sana...

Sasa nikajikoroga kuitamani MARK X ,,Aliku nayo rafiki angu,, nilimuona anafaidi sana
Kwanini mimi niwe na IST alafu yeye MARK X,,, nikaona bora niiuze gari yangu ili niongezee pesa na mimi nichukue Mark X

Kilicho tokea nikafanikisaha kuiuza gar yangu na hapo nikawa nimekaribisha matatizo
Mpaka sasa sijafanikiwa kununua iyo MARK X niliyo itamani na sijui nitainunua lini,, pesa yenyewe naona giza, Kwani nimeitafuna

Naandika huu uzi kwa uchungu sana ninapo jiona nipo standi ya mwendokasi na kila gari inayo kuja imejaa


Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha ....dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wabongo tunapenda sifa sana, Mark X hapa mjini unafanyia nini? ENgine kubwa, matumizi ya mafuta makubwa, bei yake kubwa. Unaponunua gari cha kwanza jiulize kwa nini unanunua gari, au hii gari itanisaidia kwa shughuli zipi? 1. Movement kwenda ofisini na mishe za hapa town gari IST ilitosha kabisa. 2. Kama una shughuli kubwa kubwa za pori pori kidogo kama shamba tafuta gari kubwa lenye 4WD.

Pole sana sifa zimekuponza. Mimi nitafia na corolla yangu cc 1500
Sasa Corolla hapo una gari au kamkebe ka kukukinga na jua/mvua,
 
Kumbe umekula mwenyewe safi tu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu kutoka IST mpaka kwenye Mark X utapata shida sana, umezoea kutumia 1L kwa 12KM unataka uende 1L kwa 6-7KM utapata shida sana tuachie wakali wa town tunavuta 3000CC 1L kwa 4.5KM na mambo yanakwenda swalama kabisa...
 
Sasa Corolla hapo una gari au kamkebe ka kukukinga na jua/mvua,

You can imagine kila mtu akinunua V8, maisha yangekuwaje.
Yaache maisha yaende kila mbuzi akiwa anakula kwa urefu wa kamba yake.
Wakati unaidharau corrolla kumbuka kuna mtu hana miguu ya kutembea, mwingine ana miguu lakini hana baiskeli, mwingine ana baiskeli lakini hana pikipiki, Mwingine ana pikipiki lakini hana gari walau hata starlet. Mwingine ana corrola lakini hana Prado, V8, Mwingine ana uwezo wa kuwa na kila aina ya gari, lakini hana furaha, ni mpweke. Mwingine ana vyote, ana mke lakini hana mtoto.

And that makes life enjoyable.
 
Mark X ina cc 2500. IST aliyoiuza ina cc 1490. Hilo wese kwa level yake asingeweza
Kweliiiii kabisa. Hii ndio maana yangu. Hapo kuna tofauti ya 1000Cc
Hilo ni gari jingine ,[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Back
Top Bottom