Mamii ilikuwa rahisi kwa kuwa huyo mtoto ulimkuta to be frank nizungumze nikiwa ni mwanamke ni ngumu sana kukubali kulea mtoto aliyekukuta.maana kupitia kwake unauona uovu wa mumeo,kupitia kwake unjiona labda pengine kuna sehemu hukukamilika,kupitia kwake unazidi kujihisi una mapungufu si unajua siye wanawake tunavokimbilia kujilaumu katika kila makosa ya waume zetu,so please tusilinganishe mtoto wa nje ya ndoa na mtoto wa kabla ya ndoa hawa ni watoto tofaut KABISA,na justification zake pia ni tofauti,mimi mume wangu aniletee hata watoto kumi ambao aliwapata kabla ya kunijua mimi nitawalea maana inawezekana mimi ndiye sababu ya mama yao kuachwa,lakini walio chini ya umri wa ndoa yangu please!mwanaume anapaswa kuwa na busara sana tena sana PLUS MAOMBI!vinginevyo akiendekeza zile za kidume dume za "HAYAISHI,YANI BADO UMEKASIRIKA TU,MKE WANGU SI UNISAMEHE,MBONA HATA KAKA NAE ANA MTTOT MWINGINE NA HAJAMWAMBIA MKEWE SI BORA MI NIMESEMA,!''mambo yanaweza kuwa mabaya sana.nimejaribu kuvaa viatu vya huyo mke though najua siwezi kuimagine atareact vipi!